Hansard
JF-Expert Member
- Jan 4, 2014
- 842
- 247
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA WAZIRI MKUU
TAARIFA KWA UMMA
KAULI YA SERIKALI KUHUSU MAPENDEKEZO YA NAULI ZA MABASI YAENDAYO HARAKA (DART)
Tarehe 25 Novemba 2015 niliwaagiza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART), Wakala wa Barabara na Uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam wapitie masuala yote ya kisheria yanayohusu Mradi na kuhakikisha kuwa miundombinu inakamilika ili Mradi uanze kutoa huduma tarehe 10 Januari 2016.
Baada ya kupitia mikataba na nyaraka mbalimbali imebainika kwamba:
a) Hakuna Mpango wa Biashara ulioandaliwa na Mwekezaji yaani Kampuni ya UDART iliyopewa jukumu la kutoa huduma za mpito (ISP);
b) Gharama za uwekezaji (ununuzi wa magari, vifaa vya kutozea nauli na gharama nyingine) haziko bayana.
Pamoja na kuwepo kwa kasoro hizi kubwa tarehe 05 Januari 2016 Mwekezaji aliwasilisha kwa Mamlaka ya Kudhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) ombi la nauli za Mabasi Yaendayo Haraka kama ifuatavyo:
i). Mbezi-Kimara 700/= (Mwanafunzi nusu ya nauli)
ii). Mbezi-Kivukoni 1,200/= (Mwanafunzi nusu ya nauli)
iii). Mbezi-Kimara-Ubungo-Mwenge 1,400/= (Mwanafunzi nusu ya nauli).
Kigezo kikubwa cha kupanga nauli pamoja na mambo mengine ni gharama za uwekezaji (capital costs) na gharama za uendeshaji (operational costs). Hivyo kwa kukosekana gharama halisi za Uwekezaji ni dhahiri kuwa viwango hivyo vya nauli vinavyopendekezwa havina uhalisi.
Tafsiri ya viwango hivi vya nauli kwa mtumishi mwenye kima cha chini cha mshahara cha 260,000/= kwa mwezi na amabaye ana mke na watoto wawili wanaosoma atatumia zaidi ya robo tatu (75%) ya mshahara wake kwa kulipa nauli.
Serikali haikubaliani na mapendekezo hayo ya nauli kwa sababu gharama za uwekezaji za Mwekezaji huyo hazifahamiki na hakuna Mpango wa Biashara unaoeleza mtiririko wa biashara ya Mabasi Yaendayo Haraka.
Kwa kuwa viwango hivyo vya nauli vilivyopendekezwa havikutokana na misingi halisi ya gharama za uwekezaji na uendeshaji na kwa vile watumiaji wa huduma za mabasi hayo wameonesha kutomudu viwango hivyo vya nauli, Serikali hairidhishwi na viwango hivyo kwa kuwa havina uhalisia.
Imetolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu