Waziri Mkuu acha kujificha chukua hatua, kuokoa mali ya umma

VIKWAZO

JF-Expert Member
Apr 9, 2011
1,899
580
KATIKA kile kinachotafsiriwa kuwa ni kuwatega mawaziri na viongozi wa Serikali wanaotumia magari ya kifahari na yenye gharama kubwa, Waziri Mkuu,Mizengo Pinda ameanza kuachana na matumizi ya magari yenye gharama kubwa.

Hatua hiyo inadaiwa kuwa inalenga kuwafanya mawaziri na viongozi wengine wa juu
wa Serikali, kupima, kutafakari na kuchukua hatua juu ya matumizi ya magari
ya gharama kubwa wanayotumia sasa ambayo yamekuwa yakipigiwa kelele na
baadhi ya wabunge na wananchi.

Uchunguzi wa gazeti hili ambao ulithibitishwa pia jana jioni na Katibu Mkuu wa
Wizara ya Fedha na Uchumi, Ramadhan Khijjah, ulibaini kuwa Waziri Mkuu,
ameacha kutumia magari ya kifahari aina ya Mercedes Benz na Toyota
Land Cruiser VX na kuanza kutumia Toyota Land Cruiser GX.

Katika mahojiano maalumu na HABARILEO, Khijjah amethibitisha Pinda kuanza
kutumia aina hiyo ya magari katika misafara yake ambayo alisema ni ya gharama ya
chini ikilinganishwa na Benz na VX ambayo gharama yao ni kubwa sana.

“Ni kweli Mheshimiwa Pinda sasa ameamua kutumia magari haya ya GX, hajatangaza
popote juu ya uamuzi wake huu, lakini nahisi ni kama ujumbe kwa viongozi wengine
wa juu wa Serikali wanaotumia magari ya gharama kubwa ili kuwafanya nao wapime
na kuchukua hatua,” amesema Khijjah.

Katibu Mkuu huyo wa Hazina, alisema ipo mikakati kabambe iliyowekwa na Serikali
ili kudhibiti matumizi holela ya fedha za umma, lakini akasema si kila kitu lazima kisemwe bungeni, kwani mambo mengine yanahitaji utekelezaji wa moja kwa
moja.

“Mfano hatua hii ya magari ya msafara wa Waziri Mkuu kuwa ya gharama ya chini
unaonesha dhamira ya dhati ya kuanza kuokoa fedha za umma kwa matumizi yasiyo na sababu. Kama Waziri Mkuu anatumia gari kama hili kuna haja gani kwa kiongozi wa
chini kuagiza gari la thamani zaidi, haiwezekani,” alisema Khijjah.

habari leo
 
yeye waziri mkuu anaamua kuonyesha mfano ili watu waige lakini bado ana nafasi ya kutoa agizo ili watu watekeleze
 
yeye waziri mkuu anaamua kuonyesha mfano ili watu waige lakini bado ana nafasi ya kutoa agizo ili watu watekeleze
Mwenzenu anasubiri muda ustaafu kwa kwa amani nyie nanyi mmeanza kumchambua chambua kila siku - alishawaambia mafisadi wana nguvu kuliko serikali, sasa mnataka maelezo gani tena zaidi ya haya?
 
Anaboa sana huyu PM...
Hivi anadhani ikiwa yeye peke yake ataacha kutumia magari ya fahari kuna anacho'save?...after all, je magari anayoyaacha yanakwenda wapi?, si yanatumika ofisini kwake?..
Dawa ni kuuza hayo magari kwa watu binafsi wanaoyataka, na kutumia fedha kununua mafuta ya kuendesha mitambo ya IPTL kule Tegeta.
Lakini pia anategemea mawaziri wa chini yake wataiga bila kukaliwa kooni?

Ukondoo wa huyu jamaa unakera sana!
 
Mwenzenu anasubiri muda ustaafu kwa kwa amani nyie nanyi mmeanza kumchambua chambua kila siku - alishawaambia mafisadi wana nguvu kuliko serikali, sasa mnataka maelezo gani tena zaidi ya haya?

hii umesema kweli ni muoga
lakini kwa nini asitoke kwenye hicho kitu kama anaogopa
 
Anaboa sana huyu PM...
Hivi anadhani ikiwa yeye peke yake ataacha kutumia magari ya fahari kuna anacho'save?...after all, je magari anayoyaacha yanakwenda wapi?, si yanatumika ofisini kwake?..
Dawa ni kuuza hayo magari kwa watu binafsi wanaoyataka, na kutumia fedha kununua mafuta ya kuendesha mitambo ya IPTL kule Tegeta.
Lakini pia anategemea mawaziri wa chini yake wataiga bila kukaliwa kooni?

Ukondoo wa huyu jamaa unakera sana!

sidhizani kama anajitambua kwamba yeye ni waziri mkuu kauli zake zinaonyesha ni muoga sana
au analipa fadhila kwa mkweree kwa kumpa kapost
 
uyo pinda kapinda adi akili eti mtoto wa mkulima ambae hana uchungu iga ya mboye kama una uchungu? we ni nyani wa mkulima si mtoto wa mkulima maay be molinge sokoine
 
USANII TANZANIA.jpg

hawa ni wasanii tu
 
Back
Top Bottom