Waziri Mhagama Apokea Mchango wa Parokia ya Kiwanja cha Ndege Dodoma Kuwkaumbuka Waathirika Hanang'

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944

WAZIRI MHAGAMA APOKEA MCHANGO WA PAROKIA YA KIWANJA CHA NDEGE KUWAKUMBUKA WAATHIRIKA HANANG'

Padre Emmanuel Mtambo wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowaska amesema Kanisa linawajibu wa kuchangia watanzania wenzetu waliopata janga la mafuriko ya Mawe na Matope kutoka Mlima Hanang’.

Alisema Parokia ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowaska Kiwanja cha Ndege kupitia kamati ya Caritas ambayo inashughulikia wanaohitaji, leo tarehe 17/12/2023 jijini Dodoma imetoa hundi ya shilingi milioni 5 ikiwa ni sehemu ya kushirikiana na serikali kusaidia waathirika.

“Kama Parokia na Kanisa; tunapaswa kufanya sehemu yetu, kupitia michango yetu tunayotoa katika akaunti ya Caritas” alifafanua

Mchango huo umepokelewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya waziri Mkuu, (Sera Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama.
 

Attachments

  • 4165d856c0d27423840ec9c239b98586.jpg
    4165d856c0d27423840ec9c239b98586.jpg
    243.9 KB · Views: 1
  • GBjbg9qXEAA2odu.jpg
    GBjbg9qXEAA2odu.jpg
    210.3 KB · Views: 1
  • GBjbikVXMAAuRzK.jpg
    GBjbikVXMAAuRzK.jpg
    209 KB · Views: 1
  • GBjbhzTXAAAdp4e.jpg
    GBjbhzTXAAAdp4e.jpg
    242.6 KB · Views: 1
Sio haba

Hongera kwa Kanisa kujali tena watu wa Hanang'

Juzi kanisala TAG walitoa pia misaada
 
Back
Top Bottom