VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,004
Nazungumza nawe Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Camilius Membe. Umekuwa na ari kubwa kukanusha kila suala la Tanzania linalojichomoza kimataifa. Unakanusha kila jambo hasa litangazwalo na vyombo vya habari vya kimataifa.
Ulianza na suala la Malawi kuhusu mpaka wa Ziwa Nyasa. Ukafuata suala la Balozi wa China aliyepanda jukwaa la CCM na kuhutubu. Tena,ukakanusha kuhusu ndege ya Rais wa China kubeba pembe za ndovu. Serikali yako pia ilikanusha kwa nguvu filamu ya Nightmare na uwindaji haramu.
Kubwa linaloisukuma Serikali ni kutangazwa habari zetu nje. Inadaiwa kuwa vyombo vya nje vinatuchafua na vina wivu. Sasa,nina taarifa kuwa kuna waandishi wa kimataifa wametinga Kiteto kurekodi dhahama ya kule. Wanatengeneza Documentary juu ya mauaji yanayoendelea Kiteto kati ya wakulima na wafugaji.
Wameshaanza kazi. Wanaendelea. Wakimaliza watatangaza mauaji hayo katika vyombo mbalimbali vya kimataifa vya habari kwa njia ya sauti na video. Nakuomba Waziri Membe uandae kanusho. Utalitumia punde. Usichelewe.
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam