Waziri Mbarawa komaa na hili katika taa

mbuta likasu

Senior Member
Feb 29, 2016
155
87
Tunashukuru sana mh.waziri Mbarawa kuweza kufika mamalaka ya viwanja vya ndege Tanzania na kugusia kitengo cha rasilimali watu cha mamlaka hiyo,kitu ambacho watangulizi wako hawakuwahi kukifanya pamoja na kutawaliwa na madudu ya kila aina kitendo hicho kinatupa faraja sana mh.waziri ,tuna imani yale yote ambayo yamekuwa ni tatizo kwa juhudi zako tuna imani yatafika ukomo komesha yafuatayo mheshimiwa:

1.Utitiri wa ajira za muda zizizokua na tija kwa mamlaka.
kumekua na watu ambao wana ajiriwa kwa kipindi cha mwaka mmoja moja ambao ni renewable,hawa watu upewa nafasi hizo bila kufuata taratibu za kiutumishi na wengi wao ni ndugu au jamaa wa vigogo wa mamlaka,watu hawa waliingizwa kazini enzi za utawala wa mkurugenzi aliyefariki. Pia vibarua hawa wengi hawana sifa stahiki za kufanya wanachokifanya,mbaya zaidi pamoja na kuwa na sifa zenye kutia shaka lakini wamepewa nafasi na fursa mbalimbali kama mafunzo.hii ufanyika makusudi kwakua mamlaka ina watumishi wengi wenye elimu ya kutosha lakini wamekuwa wakiipuuzwa kutokana na viubarua hawa kupewa nafasi na 'vigogo' wa TAA.

2. Upandishaji vyeo kwa upendeleo
Suala la kupandisha vyeo watumishi limekua ni shida kubwa sana hasa katika nafasi za umeneja,mpaka sasa haijulikani sifa inayotakiwa mtu awenayo ii aweze kufikiriwa katia nafasi za umeneja nadiriki kusema hilo limefanywa makusudi ili kuweza kupachika watu wao wasio kuwa na elimu ya kutosha katika nafasi hizo. hali hii imepelekea kuwa na mamneja wengi wenye elimu isiyoridhisha na uzoefu wa ovyo lakini wamepewa nafasi based on nepotism.
Pia kuna kasumba ya kupandisha vyeo haraka kwa baadhi ya watu ambao wana mahusiano yanayolitiliwa shaka na baadhi ya vigogo wa mamlaka. juzijuzi kuna dada kapandishwa cheo lakini uwezo wake ni mdogo mno lkini wakongwe wengi wenye uwezo wa usiotia shaka wameachwa.

3. Mafunzo kutolewa kwa kuangalia 'sura'
Kumekua na ubaguzi mkubwa sana katika kutoa mafunzo kwa watumishi,kumekua na watu ambao mamlaka inajua ilivyowapata yenyewe wao wamekua wakipewa fursa za mafunzo ndani na nje ya nchi lakini asimilia kubwa ya watu hao wamekua hawana mchango wowote chanya kwa mamlaka na mmoja ya watu hao kaachia ngazi juzijuzi watu wenye 'potential' hawapewi nafasi.

4. Kubana bila sababu za msingi ruhusa ya watumishi kujiendeleza kielimu.
mamlaka kwa muda mrefu imekua haitoi mchango kwa watumishi wanaopenda kujiendeleza kielimu hasa pale mtumishi ambaye anaomba kujiendeleza kielimu akiwa hana'godfather'. Hata wale ambao wamekuwa wakijiendeleza kwa kusoma chuo kikuu huria cha Tanzania hawapewi ushirikiano wa maana mamlaka.

Hayo ni baadhi ya mambo machache ya ovyo ambayo yamekua yakiwakwaza wafanyakazi wengi hasa wale wa kudumu,na yanasababiswa na kitengo cha utumishi,udhalimu huo unaongozwa na DHRA akisaidiana na moja wa mameneja wa rasimilimali watu ambao wamefanya watu wafikie hatua ya kujipendekeza kwao hili mambo yao yawe safi ndani ya mamlaka..kwakua watu wana imani ukipendwa na watu hao wawili utafurahia maisha ndani ya mamlaka ya viwanja vya ndege Tanzania.

Tuna imani na Mkurugenzi mkuu aliyepo lakini peke yake ni vigumu kuisafisha idara ya rasilimali watu ya TAA ndio maana tumepata faraja mh. waziri ulipoligusia hili suala. Idara ya rasilimali watu ikiboreshwa itarudisha morale ya wafanyakazi wengi iliyopotea miaka mingi,ni ugumu wasoko la ajira ndio unafanya watu wengi kuendelea kudumu katika mamlaka hii ,vinginevyo kungekua na turnover ya kutisha kila mara.

MUNGU AWATIE NGUVU WOTE MLIO NA DHAMIRA YA DHATI KATIKA KUKOMESHA 'NEPOTISM' KATIKA MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE TANZANIA.
 
Back
Top Bottom