Watumishi CCM wanolewa kuhusu fursa za masomo nje ya nchi

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
1,149
745
WATUMISHI CCM WANOLEWA KUHUSU FURSA ZA MASOMO NJE YA NCHI

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia Idara ya Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI), kimefanya mafunzo kwa watumishi wa chama na jumuiya zake kuhusu umuhimu wa kujiendeleza kielimu kupitia fursa zinazopatikana kimataifa.

Mafunzo hayo yamefanyika Oktoba 3, 2024 katika ukumbi wa ofisi za Makao Makuu ya CCM, Dodoma na kuhudhuriwa na watumishi wa CCM, Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Jumuiya ya Wazazi (WAZAZI) na Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM).

Akifungua mafunzo hayo ya siku moja, Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. John Mongella amewataka watumishi wa CCM kuchangamkia fursa za kujiendeleza kielimu ili kuwa weledi katika nafasi wanazozitumikia ndani ya chama na jumuiya zake.

Amesema chama kupitia idara ya SUKI, kitajitahidi kutafuta fursa hizo, lakini mtumishi mmoja mmoja hana budi kuzitafuta kwa njia mbalimbali ikiwemo kutumia mitandao ya kijamii.

Naibu Katibu Mkuu, Ndg. Mongella alifuatana na Katibu wa NEC, ambaye ni Mkuu wa Idara ya SUKI, Ndg. Rabia Abdalla Hamid na Katibu wa NEC, Organaizesheni, Ndg. Issa Gavu.

Kwa upande wake, Ndg. Rabia amesema kujiendeleza kielimu ni muhimu kwa kuwa kunamfanya mtumishi kujipatia maarifa mapya kulingana na mabadiliko mbalimbali yakiwemo ya sayansi na tekinolojia.
Ndg. Rabia alizishukuru nchi ambazo zimekuwa zikitoa fursa za mafunzo kwa watumishi na makada wa CCM, ikiwemo Uingereza ambayo kupitia Taasisi ya Chevening imekuwa ikitoa ufadhili wa masomo kwa Watanzania.

Ndg. Rabia amewapongeza watumishi wa CCM, UWT, WAZAZI na UVCCM kwa kuhudhuria mafunzo hayo, ambayo yamewaongezea mwanga kuhusiana na ufadhili wa masomo unaotolewa na Taasisi ya Chevening kwa kushirikiana na serikali ya Uingereza.
 

Attachments

  • IMG-20241004-WA0154.jpg
    IMG-20241004-WA0154.jpg
    1.2 MB · Views: 6
  • IMG-20241004-WA0150.jpg
    IMG-20241004-WA0150.jpg
    53.6 KB · Views: 7
  • IMG-20241004-WA0151.jpg
    IMG-20241004-WA0151.jpg
    78.7 KB · Views: 6
  • IMG-20241004-WA0152.jpg
    IMG-20241004-WA0152.jpg
    57.2 KB · Views: 6
  • IMG-20241004-WA0153.jpg
    IMG-20241004-WA0153.jpg
    995.9 KB · Views: 7
  • IMG-20241004-WA0149.jpg
    IMG-20241004-WA0149.jpg
    52.7 KB · Views: 4
  • IMG-20241004-WA0148.jpg
    IMG-20241004-WA0148.jpg
    75.5 KB · Views: 6
Wapendwa,

Kwanza, nawashukuru nyote mlionifariji. Pili, nawaomba radhi niliowakosea kwa sababu at times, I became emotional, and sometimes even more so kutokana na mauaji ya Korogwe.

Hata hivyo, sina maneno sahihi ya kuelezea uzito wa maumivu yangu, na kwa kweli, sikukusudia kuandika bali nimejikuta nimeshika tu simu nikaanza kuandika. Nimeandika mengine mengi, na nikayafuta kwa wingi huo huo, lakini nimeona hili la sasa nisilifute. Siku kama ya leo, Jumatatu iliyopita, Septemba 23, saa 3:30 usiku, ndipo watu wasiojulikana walimteka dada yangu na familia yake nyumbani kwake, wakaenda kuwaua. Ni siku ambayo sitapenda kuikumbuka kamwe, lakini najua sitaweza kuisahau hadi hapo ubongo wangu utakapokuwa haufanyi kazi tena.

Nimewahi kusikia habari nyingi za watu kutekwa na kuuawa, lakini siku zote nilidhani ni mambo ya mbali, yasiyoweza kunigusa familia yangu moja kwa moja. Niliishi na imani hiyo ya uongo, nikidhani kuwa mimi na watu wangu wa hatuwezi kamwe kuhusika wala kuhusishwa katika matukio haya ya kikatili. Lakini sasa, nimeujua ukweli huu, ambao umeniumiza kuliko nilivyowahi kufikiria. Ni wazi sasa kuwa maovu haya yako karibu zaidi nasi kuliko tunavyodhani na kutaka kuamini.

Dada yangu Jonais, ulikuwa dada rafiki yangu wa karibu, na ulinitazama kwa macho yenye upendo usiojificha, usio na unafiki. Sisikitiki sana kwamba ulikufa, lakini Zaidi ulikufa kifo cha kikatili, mikononi mwa watu waovu walioamua kuua ndoto zako na za mwanao Dedan, mtoto asiye na hatia wala makosa.

Mpwa wangu, Dedan, ulikuwa na miaka minane tu, mtoto mdogo usiyejua lolote kuhusu uovu wa ulimwengu huu. Walikuangamiza bila huruma. Niliona machozi ya kaka zako, Bright na Derick, yakituacha wengi katika huzuni kuu. Niliona wanafunzi wenzako wa Shule ya Msingi Good Foundation, Korogwe, wakikulilia kwa uchungu usio na kifani. Walimu wako walilia kwa uchungu mkubwa, machozi yao yakiwa kama ujumbe wa masikitiko kwa kila aliyeshuhudia. Nakuhakikishia, kwa Imani yangu, machozi haya hayajapotea bure. Kama inavyosema Zaburi 56:8, Mungu huhifadhi machozi ya waja wake kwenye chupa Yake.

Ni vigumu sana kuelezea maumivu niliyopata nilipoona kuona miili yenu ikiteremshwa kwenye makaburi yenu. Sauti ya udongo ulipokuwa ukiwagubika ndipo nikawa na hakika huo ni mwisho wa kila kitu, mwisho wa matumaini, mwisho wa ndoto zenu. Wao waliwaua, sisi tumewazika, lakini tutaendelea kuishi na upendo wenu. Iliniumiza sana kiasi kwamba siwezi kuelezea kwa maneno, lakini moyo wangu ulivunjika. Nawe mpwa wangu Dedan, sauti yako ya furaha bado inazunguka kichwani mwangu, sauti niliyoisikia kwa mara ya mwisho mwaka jana nilipokuja kusabahi nyumbani, ukanikimbilia ukipiga kelele za "Mjomba Willy! Mjomba Willy! Mjomba Willy!" Hakika, ni sauti nitakayoikumbuka maisha yangu yote hadi hapo ama kumbukumbu zitakaponitoka au nitakapoondoka katika maisha ya dunia hii.

Kuna wakati nilichukulia kwa wepesi fulani habari za kutekwa na kuuawa kwa watu. Sasa maumivu haya yananiambia hazipaswi kuchukuliwa kwa wepesi, maana leo ni kwetu, kesho inaweza kuwa kwa mtu mwingine. Watu wengi wanapuuza, wakidhani hawahusiki, lakini dhambi ya kutokujali inaweza kumrudia yeyote.

Mithali 17:15 inatufundisha kuwa wale wanaoona waovu kuwa wana haki, na wale wanaowahukumu wasio na hatia, wote wawili ni chukizo kwa Mungu. ”Yeye asemaye kwamba asiye haki ana haki; naye asemaye kwamba mwenye haki hana haki; Hao wote wawili ni chukizo kwa Bwana.” Na haya yanayotokea sasa ni wazi kuwa ni maovu yanayofumbiwa macho na baadhi ya watu katika jamii yetu. Tunakumbushwa pia katika Isaya 5:20 kuwa "Ole wao wasemao kwamba uovu ni wema, na kwamba wema ni uovu; watiao giza badala ya nuru, na nuru badala ya giza; watiao uchungu badala ya utamu, na utamu badala ya uchungu!" Na kila nikiitafakari aya hiyo, naona maovu yaliyomwangamiza dada yangu na mpwa wangu.

Katika kitabu cha Waefeso 5:11, tunaambiwa tusishirikiane na matendo ya giza, bali tuyakemee. "Wala msishirikiane na matendo yasiyozaa ya giza, bali myakemee..." Na ni lazima tuyakemee matendo haya kwa nguvu zetu zote, kwa sababu kifo cha Jonais na Dedan si cha kwanza, na labda hakitakuwa cha mwisho kama tusipokemea haya sasa.

Kwa wale wanaodhani matendo haya hayawahusu, wakumbuke historia inatufundisha kuwa ukimya mbele ya dhuluma huleta maangamizi kwa wengi, kama alivyosema Mwanatheolojia wa Ujerumani enzi za Adolf Hitler, Mchungaji Friedrich Gustav Emil Martin Niemoller, alipowakumbusha watu jinsi walivyokuwa wakipuuzia matendo ya unyanyasaji mpaka yalipowafikia wao wenyewe—na yeye mwenyewe.

Shairi lake lasomeka hivi: "First they came for the socialists, and I did not speak out — because I was not a socialist. Then they came for the trade unionists, and I did not speak out — because I was not a trade unionist. Then they came for the Jews, and I did not speak out – because I was not a Jew. Then they came for me — and there was no one left to speak for me."

Maumivu haya ninayoyahisi leo, yanaweza yakamgusa mwingine leo, au kesho, au keshokutwa. Na kwa wale wanaoamini kuwa hawawezi kukutwa au kuathiriwa nayo, nawapa changamoto waangalie historia na kuyasoma maandiko. Wakati huponya, lakini kumbukumbu ya uchungu na maumivu haya haitaondoka milele.

Dada yangu Jonais, mpwa wangu Dedan, na binti wa kazi aliyeuawa pamoja nanyi, mlidhulumiwa maisha yenu na watu wasiojulikana, lakini ninatumaini kuwa Mungu amewapokea kwa amani. Haya ni maombi yangu, hata wakati maumivu yanapokuwa hayavumiliki.

Rest in peace.

William Shao
Septemba 30, 2024
 
Back
Top Bottom