figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,487
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa atema cheche bandarini, ashangaa kwanini watu wanahonga ili wafanye kazi bandarini? Asisitiza wote aliowaondoa dar wasirudishwe kwani wamekuwa wakimfuatafuata mwanza dodoma wakiomba Warudishwe, Je bandarini kuna mgodi wa Madini?
Atoa maagizo Mazito;
1.Lazima yard zote ziangaliwe
2.Lazima mchukue hatua kwa wanaokiuka taratibu
3.Flow meters zote lazima zifanye kazi
4.Kazi ya kwanza kwa Bodi ya TPA ni kubadili tender Board
5.Mfanyakazi wa TPA kuwa na kampuni inayofanya kazi ndani ya bandari mwisho
6.Ajira za ndugu Mwisho
7.Lazima malipo yanayofanywa kumbukumbu ziwepo
8.Makubaliano Lazima yafuatwe kwa benki zilizokubaliana na TPA kufanya kazi Masaa 24/7
=======
Waziri wa ujenzi uchukuzi na mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amewapiga marufuku baadhi ya wafanyakazi wa mamlaka ya bandari nchini wanaoendelea kumsumbua hadi hatua ya kwenda nyumbani kwake kwa lengo la kumrubuni ili awanasue katika tuhuma mbalimbali ikiwemo ubadhirifu wa mali za umma zilizoisababishia serikali hasara kubwa na kupoteza mamilioni ya shilingi.
Profesa Makame amesema hayo jijini Dar es Salaam wakati akifungua bodi ya mamlaka hiyo ikiwa ni siku chache tangu apokee ripoti ya bandari hiyo aliyosema kuwa na madudu na idadi kubwa ya wafanyakazi wakitajwa kuhusika na ubadhirifu wa mali za umma ambapo ameitaka bodi hiyo kuhakikisha inawahamisha wafanyakazi hao na kuwapeleka kwenye bandari za pembezoni mwa Nchi na kutahadharisha kutorudishwa kwa mfanyakazi yeyote aliyehamishwa Bandarini hapo kwa namna yeyote ile.
Mara baada ya uzinduzi huo Profesa Mbarawa alitembelea bandari hiyo na kujionea changamoto mbalimbali ikiwemo bandari kushindwa kufanya kazi masaa ishirini na nne kutokana na huduma za kibenki kukosekana tatizo ambalo limejibiwa na kaimu meneja wa bandari hiyo.
Baadhi ya wasimamizi wa vitengo mbalimbali vya kusimamia utendaji wa Bandari hiyo nao walishikwa na kigugumizi walipotakiwa kujibu maswali ya Waziri kuhusiana na namna ya kushusha makontena na magari bandarini hapo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Profesa Ignas Rubaratuka, akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (katikati), wakati wa uzinduzi wa Bodi hiyo jijini Dar es Salaam.Kulia ni Katibu MKuu wa WIzara hiyo, Sekta ya Uchukuzi, Dr. Leonard Chamuriho.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Profesa Ignas Rubaratuka (kulia), akimkabidhi Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Profesa Ignas Rubaratuka, vitendea kazi baada ya kuizindua rasmi bodi hiyo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akitoa maelekezo kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Profesa Ignas Rubaratuka (kushoto), wakati alipokagua eneo la kuhifadhia magari katika bandari ya Dar es Salaam.