Mpinzire
JF-Expert Member
- Jan 18, 2013
- 7,224
- 12,944
Kalemani alikuwa mbobevu wa Sheria katika Nishati na Madini, yule Mkurugenzi wake wa Tanesco alikuwa mbobevu wa Electronic Engineering.Kuna muda unajizuia usiongee lakini inakwaza.
Wananchi wako kimya, hawaoneshi kwa vitendo kusikitishwa na hali ya kukatika kwa umeme, maisha kupanda gharama katika nyanja zote.
Karibia kila kitu kinategemea umeme. Bila ya umeme hakuna ajira viwandani. Kuna kiwanda flani nakihifadhi jina, kimeshusha uzalishaji na kuondoa watu 120 kazini. Jambo baya sana.
Hawa watu 120 walikua na watu wengi sana nyuma yao wanawategemea. Watu hawa wanaishije? Watu hawa waliambiwa umeme ukikaa sawa wataitwa kazini, sasa ni kauli ya baada ya miaka 2.
Hivi watanzania, tuna akili timamu kweli? Mtu mmoja anajiita waziri, umeme ukatike usikatike auathiri mshahara wake, tunakubali kauli za kizembe namna hiyo.
Ifike hatua, nayeye awajibike. Umeme ukikatika, asilipwe mshahara. Kashindwa kusimamia wizara.
Bila nishati ya umeme hakuna maendeleo, taifa lolote lile.
Kwa kauli aliyotoa leo, ningekua mwenye nchi, ningetengua uteuzi wake.
Hopeless and rubbish.
Atafutwe mtaalamu wa umeme ndani ya shirika la tanesco, apewe wizara, tuone kama kutakua na shida. Mhandisi ana njia mbadala za kufanya kazi na matengenezo huku huduma ya umeme ikiwa palepale.
Watu wafanye marekebisho usiku, mchana uzalishaji viwandani uendelee. Watu wapate ajira, uchumi ukue.
Sasahivi tuna mtu wa IT na yule muuza madishi ya DSTV ambae alimchagua yeye mwenyewe
Sent using Jamii Forums mobile app