Waziri Makamba, do the right thing to shame the devil!!

NIMEONA

JF-Expert Member
Aug 4, 2019
3,865
5,683
kama kuna wanasiasa vijana nchi hii ambao mimi binafsi nawakubali sana kutokana na uwezo wao wa kiakili, wewe ni namba moja mheshimiwa. iko hivyo kwangu muda mrefu tu. na si mimi tu, kuna wengine tu wanaouona umaridadi wako pia......ushahidi upo ulipoingia katika kinyang'anyiro cha uraisi na kushika namba tano. aisee si jambo dogo lile hata kidogo!

mheshimiwa raisi Magufuli (r.i.p) pia aliona uwezo wako na ndo maana akakukabidhi wizara kwa muda wa miaka minne na ushee (kama sikosei). miaka minne ni mingi mno na ni ushahidi kuwa kwa raisi kukaa na mtu kwa muda wote huo kipo anachokiona kwako.

bahati mbaya sana, katika siasa kupishana kimtazamo kwa baadhi ya maeneo ni jambo la lazima na kawaida sana (naamini (sina uhakika lakini) walipishana kikwete na mawaziri wake, mkapa na mawaziri wake, mwinyi nae na hata nyerere......kwa maana ya kutetwa n.k). bahati mbaya zaidi ni kuwa katika awamu ya tano uoga/ukatili ulitamalaki, hususani kwa watu waliokuwa hawaonekani kuwa na uadui na tawala iliyopita (ya kikwete) au wale walioonekana smart haswaa. wewe, uliangukia sehemu zote mbili.....hukuwa na uadui na uko vema upstairs (ref: kinyang'anyiro cha uraisi)!!

uliwekwa katika wizara iliyoonekana itakuwa na changamoto za kukushinda.....kwa miaka minne ukaitendea haki, haki ambayo ilijiimba yenyewe kwani isingewezekana kuimbwa. nafikiri hata mteuaji alishindwa kuelewa ni vipi 'hulikorogi' akutumbulie mbali.

baada ya kuona muda unakwenda tu bila 'kumkanyaga kwa bahati mbaya ili akulipue kwa makusudi', vijana kina makonda, musiba et al. wakaamuriwa waanze kazi ya nguvu mara moja, yaani bila kuchelewa. yes, wakaingia kazini (fedha, vifaa (vyombo vya habari) na ulinzi vyote vilikuwepo vya kutosha hivyo hakukuwa na shida yoyote). yafuatayo yakawa yanatangazwa na yanalazimishwa kuaminika;

-makamba mwizi, ameiba bilioni 1(kama sikosei) wizarani. musiba na gazeti lake ndo walichukua hii tenda vizuri sana. akaachia maclips meeengi akikuchafua. haukuwa na nafasi ya kujibu (na isingewezekana sababu ya juu), pekee kilichowahi kukisikia kutoka kwako ni kuwa 'si vema kubishana na mjinga'.

-makamba anashirikiana na kikwete (maskini mzee wa watu, Mwenyezi Mungu aendelee kumpa subra, uvumilivu na umri mrefu na aendelee kutoa 'dafrao' kwa maadui zake) kumhujumu raisi magufuli.

-kigogo2014 ni makamba na wenzake.

-namba zote zikawa hacked, maongezi mengi tu yakasikilizwa, nina uhakika yakiwemo na yale ya kifamilia (udhalilishaji wa hali ya juu kabisa kutoka kwa mwenye nguvu kuu dhidi ya asiye na chochote).

-mzee wako na marafiki zake wakadhalilishwa vibaya na kina musiba waliotumwa. na mengine mengi, list ya matukio ni ndefu sana. yalifanywa hayo yote ili kukuchanganya na kukumaliza kisiasa......using'ae tena, ukufilie mbali huko! ni kweli, ulikuwa unakufilia mbali huko; ulitumbuliwa na kwa vile jamii ya kitanzania (hata wasomi wenye phd ni oga, iliyosinyaa (si hojaji) n.k, iliaminika na imeaminika kuwa wewe ni mwizi, mhaini, hauna kitu kichwani n.k. kwa kifupi kila jina baya na tusi baya umepewa na kuna namba kubwa tu ya watu iliyoamini hivyo. ulishakuwa unakufilia mbali, kazi ilikuwa imekwisha....ukichanganya na mabadiliko ya katiba yaliyokuwa yanakuja, iliisha kabisa kazi!

kama wazungu wanavyosema kwamba 'many are the plans in a man's mind, but it's the God's purpose that prevails', kabla haujakufilia mbali huko kabisa, mabadiliko yanatokea. na aliyeshikia nchi katika chagua chagua zake za hapa na pale, amekuona......amekupa wizara. hili hukulitarajia, hatukulitarajia na hakuna aliyelitarajia. mathreads kadhaa wa kadhaa yapo humu yakielezea ni namna gani huwezi tena kuibuka kisiasa.....wengine walitamani hata ubunge usiupate tena. kimtindo, tulianza kuamini kuwa ni kweli wewe kushika hata nafasi wa uwaziri ndo basi tena.

maadui zako hawakulitegemea zaidi hili; hivyo wamestuka sana sana sana......sababu ni ile ile niliyoisema, uoga na wivu. katika hali ya kujaribu kuendelea kuuaminisha umma wa watanzania ubaya wako (infact, kuhamishia chuki kwa mama samia pia), wamekuja na lundo la very disturbing assumptions;

-mwizi (ingawa hakuna ajuae ni nini umeiba mpaka sasa) karudishwa serikalini, sasa hivi ufisadi kama kawa,
-mama msaliti wa jpm,
-makamba ataharibu hivi karibuni na mama atajuta kumteua,
-inakuwaje mhaini makamba anarudi serikalini?,
-kikwete ndo kamuweka makamba n.k

brother makamba,
nyuma ya matusi hayo kuna matamanio yasiyoelezeka ya kukutaka ushindwe, sio wewe tu bali na aliyekuteua......hilo ndo ombi lao kuu linalowanyima usingizi!

ili kuwaaibisha mashetani hawa, tafadhali fanya mambo sahihi yafuatayo, kwa mtazamo wangu;
1. ongeza ueledi maradufu wizarani......tuone matokeo siye wananchi,
2. weka wazi mikataba ikiwezekana wakome kuzusha zusha,
3. kuwa wewe kama ulivyo siku zote ambao tunaokufuatilia tunakujua.....busara, utulivu wa kuongea na kuelekeza (si vitisho vya hovyo hovyo vinavyoweza kuwanyima raha subordinates n.k)
4. pigania urahisi wa umeme kwa kadiri ya uwezo wako
5. potezea wajinga wajinga wa mitandaoni, piga kazi

ni hayo tu; naamini ukienda nayo sawa mashetani watakuwa wameaibika sana!!
 
Unatuandikia utumbo mtupu.Huyo mwizi wa mitihani ya kidato cha NNE ,Leo unakuja kumsafisha.Acha ubwege.
 
Nachojua regardless of everything hii nchi sio ya kifalme, habari ya usomi imepitwa na wakati, tunao wasomi wengi tu, na experience wanaipata wakishapewa majukumu, kama hamuwapi wengine hiyo experience wataipata wapi?

Kuendelea kuteua watu wale wale kila awamu ni mojawapo ya sababu za umasikini wa hili taifa ikionesha hata mamlaka za uteuzi zimechoka kufikiria, hazina mawazo/fikra mpya.
 
Kumlazimisha apiganie umeme wa bei rahisi ni kumlazimisha asiwe mweledi..
Aipangie Tanesco bei na sio Tanesco ijitegemee ifanye biashara...

Yale Yale ya Kalemani.. mwisho huduma inadorora kama sasa
 
Unatuandikia utumbo mtupu.Huyo mwizi wa mitihani ya kidato cha NNE ,Leo unakuja kumsafisha.Acha ubwege.
Ila tuwe wakweli, hebu jipime wewe kwanza na yeye 'aliyeiba'. Hata hivyo sifahamu lolote kuhusu hilo, mi nazungumzia siasa tu
 
Kumlazimisha apiganie umeme wa bei rahisi ni kumlazimisha asiwe mweledi..
Aipangie Tanesco bei na sio Tanesco ijitegemee ifanye biashara...

Yale Yale ya Kalemani.. mwisho huduma inadorora kama sasa
Sawa boss lkn nililenga zaidi kuhakikisha anahangaikia kikamilifu vyanzo vyote vya nishati vizalishe kikamilifu ili tupate kwa bei nafuu.......bei za units zishuke
 
Upewe smartphone bure halafu ushindwe kumpamba sponsor hata mimi nakunyang'anya smartphone yangu.

Njaa inaondowa utu hasa wa mtu mweusi.
Usilolijua ni sawa na usiku wa giza.....endelea kutoa habar maana inaonekanai 'unazozifahamu'.
 
Wewe ni mlawa utake usitake wewe ni mlawaaaaaa kama hutaki we ni mlamwa wa kenia
Umemaliza matusi kiongozi au bado kuna mengine? Km hapo ndo unajihisi umetukana vua kutosha mwenyewe, basi kajifunze zaidi.
 
Back
Top Bottom