Waziri Magufuli kulikoni!!

Waziri Magufuli kulikoni!!

Karibuni masijala

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2012
Posts
409
Reaction score
135
Wanajamvi heshima kwenu.

Ninaomba kuelimishwa kuhusu waziri mwenye dhamana ya miundo mbinu mhe. John Makufuli kwani anachoamua sicho kinachotendeka kama waziri mwenye dhamana kama kikitendeka hakichui round kinapingwa na watendaji wa ngazi za chini na hata boss wake.

Hebu tujifunze kwa haya machache tujibu swali kulikoni mheshimiwa ambaye anaonekana mtendaji inashindikana na kama ikiwezekana ni kwa muda mfupi kwani hamna mwafaka?
Alitaka kwa mujibu wa sheria ya TANROADS Iliyotungwa na Bunge na kupitishwa na Rais apige chini jengo la TANESCO alipingwa mpaka na Rais.
Akataka abomoe na asilipe nyumba zilizojengwa hifadhi ya barabara. Akapingwa na watawala na watawaliwa.
Ajabu akaona pia vyema stand ya ubungo near TANESCO Wafanyabiashara wadogo wasifanye biashara katika ile stand ni hatari akaungwa mkono na Polisi wakasimamia mamuzi hayo mpaka wakahama sasa wamachinga wamerudi wanajitafutia riski asb mpaka jioni kama kawaida huku watendaji ngazi zote wakiwa wanunuzi wazuri wa bidhaa zao

"Kulikoni"
 
tusisahau waliompinga mabango mpaka sasa hatuelewi magizo ya kuyangoa yalitekelezeka au yamejaribishwa maisha yanaendelea na kupiga dili za mabango maana alidai fedha hizo haziko wazi.
 
Nadhani misimamo yake imemfanya asielewana na mkuu wa kaya. halafu amekuwa kimya sana,wamemfix nini. hii nchi inahitaji consaltant
 
Huyo Magufuli sasa amechoka Je umewahi kumsikia anazungumza chochote kuhusu kucheleweshwa kwa ujenzi wa kipande cha kilomita sitini cha Barabara Kibiti Lindi kwa miaka zaidi ya Minane sasa? Mbona kwa zingine anazungumzia!!!
 
mpelekeni sugu labda ataweza kuliko dokta magufuri,sugu anauzoefu wa kutosha
 
Magufuli katulizwa baada ya chama kumuonya kujihusisha kwake na Raila Odinga. kaambiwa apunguze kiherehere vinginevyo watamvua uanachama.
 
Back
Top Bottom