Waziri Maghembe awasimamisha kazi Vigogo Kilimanjaro National Park

Manyerere Jackton

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
2,438
4,454
Waziri Maghembe mwenye dhamana ya Maliasili na Utalii, kawasimamisha kazi Chief Park Warden, Mhifadhi wa Utalii na maofisa wengine kadhaa kutokana na tuhuma mbalimbali, zikiwamo za ufisadi, njia za panya zilizobuniwa na kuratibiwa na wakubwa, uchafu katika Mlima Kilimanjaro, vifo vya wapagazi, nk.

Chanzo: Mfanyakazi wa KINAPA-mchana huu.

=====
1.jpg

Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe amemuondoa Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Kilimanjaro (Kinapa), Erastus Lufungulo na kutoa maagizo mazito kwa kampuni za wazawa.

Maghembe amemuondoa Lufungulo Kinapa na kumrudisha makao makuu ya Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa) baada ya kufanya mabadiliko kwenye baadhi ya hifadhi hizo nchini na nafasi yake kuchukuliwa na Betrita Loibooki aliyekuwa Mkuu wa Hifadhi ya Arusha.

Pia, Maghembe ametoa muda hadi Mei, mwaka huu kwa kampuni za wazawa zinazohudumia watalii wanaopanda Mlima Kilimanjaro kuboresha huduma, vinginevyo ataruhusu ushindani wa kibiashara.

Vilevile, amezitaka kampuni za utalii kuwalipa wapanda mlima mishahara waliyokubaliana na Serikali na hataki kusikia wanapunjwa ujira wao.

Waziri huyo alitoa maagizo hayo katika kikao cha wadau wa utalii wanaohudumia watalii Mlima Kilimanjaro na kusisitiza kuwa wasipoboresha huduma kwa kiwango cha kimataifa, ataruhusu ushindani na kampuni za nje.

Mbali na kufanya mabadiliko hayo, ameuagiza uongozi wa Tanapa kufanya haraka mabadiliko ya watumishi waliopo sehemu za kuingilia watalii za Kinapa.

Profesa Maghembe alisema sababu nyingine iliyochangia kushuka kwa idadi ya watalii ni wageni kupata huduma duni ikiwamo chakula ambacho hakina hadhi ya kimataifa.

“Nataka niwaambie, kuanzia mwezi Mei kama hamjaboresha chakula kwa watalii, mishahara kwa wapanda milima na kuwapa mavazi ya kujikinga na baridi nitaruhusu ushindani,” alisema.

Mkurugenzi Mkuu wa Tanapa, Allan Kijazi, aliahidi kuitisha kikao cha wadau wote wa utalii kabla ya Mei ili kujadili changamoto na maagizo hayo ya waziri.

Msemaji wa Wapanda Mlima Kilimanjaro na Meru, James Mwamatego alisema kwa muda mrefu wameomba kupatiwa mikataba ya ajira, lakini baadhi ya wamiliki wa kampuni za utalii wamegoma.

Mwenyekiti wa Chama cha Huduma za Utalii Mkoa wa Kilimanjaro (Kiato), Amos Lufungilo alisema wapo baadhi ya raia wa kigeni wanaomiliki nyumba ‘bubu’ za kulala wageni na kufanya biashara ya kuongoza watalii.
 
Waziri Maghembe mwenye dhamana ya Maliasili na Utalii, kawasimamisha kazi Chief Park Warden, Mhifadhi wa Utalii na maofisa wengine kadhaa kutokana na tuhuma mbalimbali, zikiwamo za ufisadi, njia za panya zilizobuniwa na kuratibiwa na wakubwa, uchafu katika Mlima Kilimanjaro, vifo vya wapagazi, nk.

Chanzo: Mfanyakazi wa KINAPA-mchana huu.

Hatimaye laana ya wapagazi imewakuta.Wamenyanyasika mno.Hongera Maghembe
 
Hivi alietoa kibali ndege ya jeshi la Quater
1. Kuingia nchin Tanzania

2. Kutua KIA

3. Kubeba twiga wakiwa hai kinyume na katiba

4. Kubeba swala nk kinyume na katiba

Huyu ninani na kachukuliwa hatuagani? Maana tunazunguuka na kukamata walalahoi mbona watoa fuhusa hawakamatwi?.....
 
Aingie ndani zaidi, huenda na Razaro nae kuna namna anahusika. Pia arudi nyuma zaidi, yupo yule Maige ambaye anamiliki nyumba yenye thamani ya zaidi ya 1.5bl.
 
Amulike na makampuni ya utalii yanawazulumu wapagazi!! Na waangalie posho ya kulala crater
 
Waziri Maghembe mwenye dhamana ya Maliasili na Utalii, kawasimamisha kazi Chief Park Warden, Mhifadhi wa Utalii na maofisa wengine kadhaa kutokana na tuhuma mbalimbali, zikiwamo za ufisadi, njia za panya zilizobuniwa na kuratibiwa na wakubwa, uchafu katika Mlima Kilimanjaro, vifo vya wapagazi, nk.

Chanzo: Mfanyakazi wa KINAPA-mchana huu.
Safi SANA. Baada ya kusimamishwa kazi inabidi uchunguzi wa kina ufanyike. Ili kubaini ukweli nini kinaendelea. Nani haswa wanahusika. ili wahusika wote wachukuliwe hatua na wasiohusika wasije kuingizwa kimakosa. Wapepelezi wana kazi mwaka huu.
 
Waziri Maghembe mwenye dhamana ya Maliasili na Utalii, kawasimamisha kazi Chief Park Warden, Mhifadhi wa Utalii na maofisa wengine kadhaa kutokana na tuhuma mbalimbali, zikiwamo za ufisadi, njia za panya zilizobuniwa na kuratibiwa na wakubwa, uchafu katika Mlima Kilimanjaro, vifo vya wapagazi, nk.

Chanzo: Mfanyakazi wa KINAPA-mchana huu.
Hizi habari za wafanyakazi kusimamishwa kazi tumeshazizoea tungefurah sana kusikia Habar kama wafanyakaz wa kampun fulan wamepandishwa mshahara. Au walimu wamelipwa posho zao au zile milion 50 kila kijiji zimetoka , kodi za kuingiza magari au bidhaa nnchini zimepunguzwa na mambo mengine mengi sio kila cku Habar mara kushtukiza, mara kuachishwa , Mara kufukuzwa hiz Habar zinachosha ukitegemea maisha yanazid kuwa magumu mfumuko wa bei kila kukicha bora ya Jana
 
Hayo yatakuja bado muda wake serikali inatafuta pesa kwanxa na kiziba mianya ya rushwa, izo sekta xikishakaa sawa mambo mazuri yanakuja
 
Amulike na makampuni ya utalii yanawazulumu wapagazi!! Na waangalie posho ya kulala crater
Hivi posho za wapagazi kwa siku ni ngapi, maana nina dogo yuko mlimani leo nilimuuliza unalipwa ngapi akasema hiyo kampuni inawalipa 15 elfu kwa siku! inaukweli hii mkuu!
 
Hivi alietoa kibali ndege ya jeshi la Quater
1. Kuingia nchin Tanzania

2. Kutua KIA

3. Kubeba twiga wakiwa hai kinyume na katiba

4. Kubeba swala nk kinyume na katiba

Huyu ninani na kachukuliwa hatuagani? Maana tunazunguuka na kukamata walalahoi mbona watoa fuhusa hawakamatwi?.....

Former...................................................................
 
Back
Top Bottom