Waziri Magembe anza na hili la mkaa mipakani

Tinde nsalala

JF-Expert Member
Feb 12, 2017
248
253
Ni jambo la kupongezwa kwa mapambano ambayo idara ya maliasili inayafanya sasa kuhusu kulinda misitu yetu.Heko kwenu.

Lkn papo pahali ambako wapambanaji hawa wanapasahau na panapitishwa sana mkaa-mipakani mwa nchi yetu.Eneo hilo ama limesahauliwa au kwa makusudi kabisa walio kabidhiwa kudhibiti wameamua kukaa kimya na kuendelea kunufaika kwa vi-rushwa na manufaa yao wayafahamuyo wao.

Kwa mfano,mpaka wa Tz na Rwanda (RUSUMO)mkaa mwingi unapitishwa huko na madereva!Afisa wa idara husika amekuwa akijihusisha na kupokea rushwa toka kwa madereva na wao kuuvusha toka Tz kwenda Rwanda.Huko kuna biashara kubwa ya mkaa!Ma elfu ya tani za mkaa hupita kila siku hapo.Afisa huyo na baadhi ya wenziye wa TRA hushirikiana ktk kufanikisha uhaini huo.

Shime ndg Maghembe,angazia eneo hilo.WanyaRwanda wamekuwa wanufaika wakubwa wa nishati ya misitu yetu huku yao(misitu)ikibaki salama na sisi tukibakiwa na jangwa.

Walivyo na akili hata hawajishughulishi na kuzuia uingizwaji wa nishati hiyo kwao kwani kwalo wao hiyo ndiyo nafuu ya uvunwaji wa ovyo wa misitu yako.

Wamekuwa wakali mno kuingizwa kwa mchele na mafuta ya alizeti na si mkaa.Ktk hilo chukueni hatua mapema japo ni tayari tumechelewa.
 
Back
Top Bottom