VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,007
Tangu aukwae Uwaziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Waziri William Vangimembe Lukuvi amekuja na mpya.Amekuwa akisafiri mikoani kwa nia ya kutatua migogoro mbalimbali ya ardhi iwahusuyo wananchi. Amekuwa akifanya mikutano ya ana kwa ana na wananchi;kuwasikiliza kero zao na kuzitolea majibu. Ni nia njema. Lakini,Waziri Lukuvi upunguze mwendo na kuwa makini.
Migogoro ya ardhi kati ya mtu na mtu humalizwa kimahakama. Si kiserikali. Kuna Mabaraza ya Ardhi na Nyumba, Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi na Mahakama ya Rufani kama vyombo vya kuitatua migogoro ya ardhi. Humo wananchi huwasilisha migogoro yao, kusikilizwa na kuamuliwa.
Wakati Waziri Lukuvi atakapokuwa anadeal na migogoro ya ardhi huko anakozunguka,azingatie na kujua uwepo wa mahakama za ardhi. Apate muda kufanya tafiti za kama mgogoro unaowasilishwa kwake umeshawasilishwa mahakamani au la. Kinyume na hapo,anaweza kuamua jambo lililokwishaamuliwa kimahakama. Utakuwa utata usio na utatuzi. Serikali si chombo cha kutoa haki kikatiba. Chombo husika ni mahakama.
Taratibu ndiyo mwendo!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Aione: Paul Makonda

Last edited by a moderator: