Waziri Luhaga Mpina Aagiza Kuvunjwa Kwa Mkataba Na Wawekezaji Watatu

Kwa waziri kutekeleza mpango huu nampa tick ya asilimia 100 ya utendaji unaoangalia maoni ya wananchi.

Kila uchao ni vita kati ya wakulima na wafugaji wakati kuna maeneo ambayo Ng'ombe na mbuzi wangeweza kukaa na kuondoa kero ya kuharibu mazao na vita visivyokwisha


Kwa mipango ipi?

Huwezi ukawanyanganya watu mashamba kwa ajili ya kuwapa watu wengine mashamba kiholela tu bila mikakati ya kuyagawa.
Ni kiki za kisiasa. Wananchi watashangilia kweli kweli kuwa tumepewa mashamba lakini aliyekuwa ameyahifadhi kwa ajili ya uwekezaji mkubwa aliona mbali.
Hatuna viongozi wenye maono ya miaka 50 ijayo kama mwalimu Nyerere.

Kama umewahi kutembelea mkoa wa Morogoro,Tanga ,Lindi,Mtwara, Dodoma ,Arusha n.k utagundua kuwa mikoa hiyo ina maeneo makubwa sana mazuri ambayo yakilimwa yatakuwa mazuri kuliko hata hayo wanayowanyang"anya wawekezaji bila mipango.
Wakulima na wafugaji nao pia hawana mipango kwa kuwa serikali na wanasiasa wanawatumia kama mitaji yao ya kupata kura.
Wakati wa uchaguzi ukifika ni rahisi sana kuwarubuni wafugaji au wakulima kuwa una uchungu na matatizo yao na ukiingia madarakani utawanyanganya wageni wote mashamba ili uwape mashamba ; utapata vigelegele vingi sana lakini kiuchumi taifa bado halitanufaika zaidi ya kuzalisha migogoro mingine na kueneza ukame kwenye nchi.

Ningekua mimi ndio waziri.

Kwanza ningekutana wafugaji 50 kila mkoa wanaomiliki ng'ombe ng'ombe zaidi ya 1000 kila mmoja.
Kwa ng"ombe .
Ng"ombe 1000 kwa bei ya sh. 500000 itakua ni 1000 x 50 x500000 = 25,000,000,0000/-
Hao wafugaji 50 nawekeana nao makubaliano na kuwapa maeneo hayo maalum kwa mkataba wa kuyaendeleza kwa namna ya kutengeneza ushirika wa watu 50 ,fedha walizopata bil.25 waziweke benki na wazitumie kuwekeza miundo mbinu na kuanza ufugaji wa kisasa .

Kwa mikoa kumi tunawekeza kwa namna hiyo hiyo kwa wafugaji kwanza . Kwa mwaka mmoja tutakua na uwekezaji wa ndani wa sh. Bil.250 ambazo zitakua pia zimeingia kwenye mzunguko wa kibenki.

Nikitoka hapo nashuka kwa wale wenye ng'ombe 100 mpaka 800 . hivyo hivyo mpaka wa ng'ombe 50. Wote watapewa ardhi kwa mfumo wa uwekezaji tu sio kuhama hama kama wamachinga huku wakiuana na kiharibu mazingira.

Kwangu mimi ni mkulima na mfugaji mmoja mmoja atapata ardhi isiyozidi ekari 10 tu ,tena baada ya kuonyesha uwezo na mtaji vinginevyo wajiunge vikundi wapatiwe ardhi wadhaminiwa na serikali wapate mikopo benki.
Sio kupeleka mil. 50 kila kijiji bila mipango.


Ili tuendelee tunahitaji mambo manne:
Watu
Ardhi
Siasa safi
Uongozi bora.

Kwa nini hatuendelei?
Tunakosea wapi?
 
Amini usiamini kuna mtu anawekwa kati.Mzeri ranch au Mkata ranch,stay tuned!!
Hapa anatafutwa EL tuu hakuna mwingine......pia Kigoda , JK wana ranchi pia....tutaona na kusikia mengi awamu hii visasi na komoana......
 
Ingependeza wakafufua Tanganyika Perkers,mpaka wazungu wanatushangaa kilivyobaki magofu.Mheshimiwa Waziri pita pale Kawe Tanganyika Perkers utoe tamko.
 
Asante sana Magembe Makoye. Nimekuelewa sana. Umeonyesha uzoefu katika kutoa suluhisho kwa namna moja.

Asante popote ulipo Kula Balimi kumi naja kulipa
 
Back
Top Bottom