Kalamu Nzito
JF-Expert Member
- Aug 13, 2015
- 376
- 850
Nimemsikiliza Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Yussuf Masauni akizungumzia masuala ya utekaji. Ameeleza kuwa nchi ipo salama na hakuna mambo ya utekaji.
Ameeleza zaidi kuwa masuala ya utekaji ni mambo yanayoibuliwa na watu wenye nia ya kupoteza dira ya Rais wa Awamu ya sita kwani "anaupiga mwingi."
Kwakweli huku ni kukosa taarifa sahihi. Zaidi, ni uthibitisho kwamba viongozi wengi hawachangamani na wananchi kujua kero na matatizo yanayowakabili. Wao kwasababu familia zao zipo salama, wanaamini watanzania wote wapo salama.
Hii ni aibu na ni wazi kwamba viongozi wengi hawana taarifa na mambo yanayoendelea kwenye wizara zao na wala hawawajibiki ipasavyo. Wanachofanya sasahivi ni kumpigia Rais kampeni tu na sio kutatua shida za wananchi.