Habari za Zanzibar
JF-Expert Member
- Dec 18, 2024
- 260
- 199
๐ช๐๐ญ๐๐ฅ๐ ๐๐ข๐ ๐๐ข ๐๐ฆ๐๐๐ฅ๐๐๐ ๐๐๐๐๐ข ๐๐๐ ๐๐๐ฅ๐๐ญ๐ ๐๐ ๐๐ ๐๐ก๐ ๐ก๐ ๐จ๐ฆ๐๐๐๐ ๐ ๐๐๐ ๐๐จ, ๐๐จ๐ก๐๐ ๐ ๐๐ข๐ก๐ข ๐๐๐ง๐๐๐๐๐ ๐ญ๐ ๐๐ ๐๐ก๐ ๐ฆ๐ข๐ ๐๐๐๐
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb) ameshiriki kwa njia ya mtandao Mkutano wa 1324 wa Baraza la Amani na Usalama wa Umoja wa Afrika (AU) kutokea katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.
Mkutano huo, umefanyika Januari 06,2026 na kuhudhuriwa na Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi wanachama wa AU, umejadili ajenda za kulinda na kuheshimu Mipaka, Mamlaka na Umoja wa Kitaifa ya Jamhuri ya Shirikisho ya Somalia.
Akizungumza katika kikao hicho, Mhe. Waziri Kombo amesema Tanzania inaunga mkono kikamilifu juhudi za AU katika kutatua mgogoro wa Somalia na inapinga vikali vitendo vyovyote vinavyolenga kuigawa na kudhoofisha mamlaka, au kuathiri mipaka ya nchi hiyo.
Aidha, ameunga mkono tamko la Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, Mhe. Mahmoud Ali Youssouf, lililotolewa Desemba 26, 2025 na akisisitiza kuwa jaribio lolote la kudhoofisha umoja na mamlaka ya Somalia linapingana na misingi ya AU na linaweza kuhatarisha amani kwenye eneo la Pembe ya Afrika na bara zima la Afrika.
Mhe. Kombo pia alisisitiza umuhimu wa umoja na mshikamano miongoni mwa nchi wanachama wa AU, ambapo alinukuu maneno ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwamba, โUmoja hautatufanya tuwe matajiri, lakini unaweza kufanya iwe ngumu kwa Afrika na watu wake kudharauliwa ama kutoheshimikaโ akihimiza Afrika kuzungumza kwa sauti moja katika masuala muhimu yanayoathiri bara.
Kwa ujumla, ushiriki wa Tanzania katika mkutano huo umethibitisha dhamira yake ya kuendelea kuunga mkono juhudi za kikanda na kimataifa za kudumisha amani, usalama na mshikamano barani Afrika, hususan katika kukabiliana na changamoto zinazolikabili eneo la Pembe ya Afrika.
Mkutano huo ulifunguliwa na Mwenyekiti wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika (PSC) kwa mwezi wa Januari 2026, Mhe. Thรฉrรจse Kayikwamba Wagner ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Mkutano huo ulihudhuriwa na Mawaziri wa Mambo ya Nje kutoka Somalia, Djibouti, Algeria, Misri, Ethiopia, Botswana, Angola, Sierra Leone, Uganda, Gambia na Cameroon.