Ojuolegbha
JF-Expert Member
- Sep 6, 2020
- 1,770
- 1,173
WAZIRI KOMBO AMUAGA BALOZI WA ANGOLA
Balozi wa Angola anayemaliza muda wake, Mhe. Sandro De Oliveira amekutana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo (Mb) kwa madhumuni ya kuaga.
Katika kikao hicho kilichofanyika jijini Dar es Salaam Juni 21, 2025, Mhe. Balozi Sandro De Oliveira alitumia muda huo kuishukuru Wizara na Serikali kwa ujumla kwa kumpa ushirikiano uliomuwezesha kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi katika kipindi chote cha uwakilishi nchini.
Viongozi hao pia walijadili masuala mbalimbali ya kisekta kuhusu ushirikiano kati ya nchi ya Tanzania na Angola, ikiwemo sekta ya Gesi na Mafuta, Madini, Uchumi wa Buluu, usafirishaji kwa njia ya reli na Ushoroba wa Lobito.