Waziri Kombo afungua Mkutano wa 27 wa MCO- SADC

Waziri Kombo afungua Mkutano wa 27 wa MCO- SADC

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,770
Reaction score
1,173
Waziri Kombo afungua Mkutano wa 27 wa MCO- SADC

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo (Mb.), amefungua Mkutano wa 27 wa Kamati ya Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ya Masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama (MCO), katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere, Dar Es Salaam.

Mhe. Kombo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo amesema mkutano huo unajadili na kutathmini hali ya usalama, mafanikio na maendeleo ya kisiasa na kijamii, utekelezaji wa maamuzi ya vikao vilivyopita, pamoja na mikakati ya kuimarisha taasisi na mifumo ya usalama wa kikanda.

“Tunapotathmini mafanikio yaliyopatikana, tuendelee kuongozwa na misingi ya mshikamano, ushirikiano wa pamoja, na tukubali kuwajibika kwa dhati kwa mujibu wa Mkataba wa SADC na Dira 2050. Nina imani kuwa kupitia majadiliano yetu, tutajizatiti upya na kuthibitisha nafasi ya SADC kama kinara wa amani, umoja, na mchakato wa kuunganisha bara la Afrika” amefafanua Mhe. Kombo.

Amesema dhamira ya SADC ni kuendelea kudumisha mshikamano, amani na utulivu kupitia usuluhishi wa migogoro, kuimarisha mifumo ya tahadhari za mapema, pamoja na kushirikisha makundi maalum kama wanawake na vijana katika juhudi za upatanishi.

Mhe. Kombo pia ameukaribisha Ujumbe wa Waangalizi wa SADC -SEOM kuja kushuhudia Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025 na kutoa salamu za heri kwa Jamhuri za Malawi na Seychelles, ambazo zinatarajia kufanya Mkuu mwezi Septemba.

Aidha, ameeleza kuwa SADC imeanza kutekeleza mkakati wa kupambana na rushwa kwa kuanzisha Kielelezo cha Juhudi za Kupambana na Rushwa, ambacho tayari kimejaribiwa katika nchi mbili wanachama ambazo ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Mauritius na kuonesha mafanikio makubwa.

Naye Katibu Mtendaji wa SADC Mhe. Elias Magosi amezisihi nchi wanachama kutekeleza majukumu yao sambamba na utekelezaji wa sera na mipango muhimu inayolenga kuimarisha amani, utulivu, na utawala bora katika ukanda wa SADC.

“Katika dira yetu ya kuleta mshikamano wa kanda na maendeleo endelevu, dhamira yetu kuu ni kuhakikisha amani na usalama vinadumu,” amesema Mhe. Magosi.
 

Attachments

  • 54675226267_5005d481cc.jpg
    54675226267_5005d481cc.jpg
    52 KB · Views: 18
  • 54676140456_e0e1bbb55f.jpg
    54676140456_e0e1bbb55f.jpg
    89.2 KB · Views: 24
  • 54676140516_91f989b181.jpg
    54676140516_91f989b181.jpg
    82.9 KB · Views: 14
  • 54675221892_2c0bb654bb.jpg
    54675221892_2c0bb654bb.jpg
    83.5 KB · Views: 22
  • 54676285039_12998b5fa4.jpg
    54676285039_12998b5fa4.jpg
    71.6 KB · Views: 18
  • 54676283183_a238b7a457.jpg
    54676283183_a238b7a457.jpg
    43.6 KB · Views: 18
  • 54676283088_8f3956137a.jpg
    54676283088_8f3956137a.jpg
    55.3 KB · Views: 21
  • 54676283623_e7b3383291.jpg
    54676283623_e7b3383291.jpg
    44.4 KB · Views: 19
  • 54676283453_fa7b808103.jpg
    54676283453_fa7b808103.jpg
    98.9 KB · Views: 15
  • 54675224657_e35836ab3e.jpg
    54675224657_e35836ab3e.jpg
    77.4 KB · Views: 20
  • 54676285133_64ffd81222.jpg
    54676285133_64ffd81222.jpg
    62.2 KB · Views: 19
  • 54675225337_3a338ed3c7.jpg
    54675225337_3a338ed3c7.jpg
    72.3 KB · Views: 18
  • 54676381360_a7afec7a72.jpg
    54676381360_a7afec7a72.jpg
    69.5 KB · Views: 20
  • 54676286269_7c97cbd63e.jpg
    54676286269_7c97cbd63e.jpg
    59.2 KB · Views: 18
  • 54676383145_873ea93d8e.jpg
    54676383145_873ea93d8e.jpg
    69.3 KB · Views: 21
  • 54676383035_03847d63e2.jpg
    54676383035_03847d63e2.jpg
    48.2 KB · Views: 16
  • 54675226012_3fb14e41be.jpg
    54675226012_3fb14e41be.jpg
    63.9 KB · Views: 19
  • 54675225597_2cf374992f.jpg
    54675225597_2cf374992f.jpg
    65.4 KB · Views: 20
  • 54676383705_87a7273d49.jpg
    54676383705_87a7273d49.jpg
    96.9 KB · Views: 19
  • 54676289139_9fa552fa14.jpg
    54676289139_9fa552fa14.jpg
    64.3 KB · Views: 19
  • 54676383680_ca67dd5b93.jpg
    54676383680_ca67dd5b93.jpg
    72 KB · Views: 17
  • 54676058671_9e7c4a859b.jpg
    54676058671_9e7c4a859b.jpg
    70.9 KB · Views: 15
  • 54676287154_7ab9f6f235.jpg
    54676287154_7ab9f6f235.jpg
    81.4 KB · Views: 18
  • 54675308292_34eacfdc5d.jpg
    54675308292_34eacfdc5d.jpg
    83.4 KB · Views: 18
  • 54676466125_93f91e55d2.jpg
    54676466125_93f91e55d2.jpg
    123 KB · Views: 18
  • 54676281968_5a33e6683e.jpg
    54676281968_5a33e6683e.jpg
    85.9 KB · Views: 20
  • 54676281803_6bf5edda3f.jpg
    54676281803_6bf5edda3f.jpg
    78.7 KB · Views: 18
  • 54676055916_d1c782b90d.jpg
    54676055916_d1c782b90d.jpg
    76.6 KB · Views: 18
  • 54676285164_bb200dcd9d.jpg
    54676285164_bb200dcd9d.jpg
    90.5 KB · Views: 20
  • 54675308107_69e52ccf2e.jpg
    54675308107_69e52ccf2e.jpg
    108.7 KB · Views: 18
Back
Top Bottom