Waziri kizimbani kwa kumdunda afande

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,462
154,332
WAZIRI Mwadini (38), mkazi wa Oysterbay, amefikishwa katika Mahakama ya Mwanzo Kinondoni kujibu shitaka la kumshambulia askari na kumtukana matusi ya nguoni.

Imedaiwa na Karani Fatma Khatibu Mbele ya Hakimu Mary Matoi kuwa Januari 1, mwaka huu, mshitakiwa alimshambulia askari namba G 789 Konstebo Alfred na kumsababishia maumivu.

Mshitakiwa amekana mashitaka na kesi hiyo itatajwa tena Februari 18, mwaka huu.

Pia, Marco Maiko (31), mkazi wa Masaki amefikishwa katika Mahakama ya Mwanzo Kinondoni kujibu mashitaka ya shambulio.

Mbele ya Hakimu Mariamu Masamalo imedaiwa na Karani Emakulatha Philipo kuwa Novemba 24, mwaka jana, mshitakiwa alimshambulia mlalamikajiMusa Abdallah na kumsababishia maumivu.

Mshitakiwa amekana mashitakana kesi hiyo itatajwa tena Februari 16, mwaka huu.
 
Kumbe ujatulia wewe acha hizo tutaanza kuzipuuza post zako!
 
bujibuji pse, umestua moyo wangu, nikajua ngereja kaenda kumdumda yule mgambo tena, aah not fair.
 
yaani nilidhani ni waziri fulani hivi, kha kumbe ni jina la mtu...waziri....toba!
 
Daa....nilitaka kushangaa Waziri gani huyo apelekwe kizimbani bila mimim kuzipta hizo nyeti kwani mimi nimsikilizaji mzuri wa News za hapa kwetu.
 
Bujibuji pliiiiiiiiiiiiiiiiiiiizzzzzzzzzzzz...u break my heart,,utaniuwa bana kwa mstuko
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom