Waziri Kigwangalla: Watanzania jitokezeni kuwekeza katika sekta ya Utalii

mkiluvya

JF-Expert Member
May 23, 2019
802
725
1593700458657.png

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla ametoa wito kwa watanzania wajitokeze kuwekeza katika biashara ya Utalii kwa kuwa masharti ya kuwekeza katika biashara hiyo yamerahisishwa tangu Serikali ya Awamu ya tano ilipoingia madarakani. Dkt. Kigwangalla ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam wakati akizindua Mkakati wa Kukuza Utalii wa ndani unaolenga kutoa ajira na kuwahamasisha watanzania washiriki na kuwekeza katika sekta ya utalii na kuvitembelea vivutio vya utalii vilivyopo hapa nchini.

Amesema tangu kuingia Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli yamefanyika mabadiliko mbalimbali yaliyolenga kuleta tija na kuifungamanisha sekta ya utalii na maendeleo ya watu kwa kuhakikisha wananchi wananufaika na sekta hiyo.

Dkt. Kigwangalla amesema Serikali ilifanya jitihada za makusudi za kulegeza masharti na kushusha viwango vikubwa vya tozo vilivyokuwepo ambavyo vilikua vinawazuia wafanya biashara wadogo hasa wazawa washindwe kuingia katika sekta hiyo. Amesema tangu kuondolewa kwa masharti hayo watanzania wazawa wanaofanya biashara ya huduma za utalii wameongezeka kutoka 1100 hadi kufikia 2000 wengi wao wakiwa watanzania.
 
Kwa vijana hasa serikali ingetumia bank ambazo zina hisa kubwa kuwapa mikopo ya riba nafuu vijawa wanunue magari ya wageni. Haya magari bei inaenda mpaka Milioni 60 kwa gari moja au serikali itoe punguzo la kodi kwa haya magari wakiyaingiza kutoka nje.
 
Hakuna miundombinu, hakuna mfumo mzuri, hakuna mwongozo unaoeleweka, hakuna watalii; waziri unawakaribisha watu wawekeze kwa hasara?
Ndyo maajabu.
Hoteli nyingi tu zinakufa, sijui wako dunia gani bila kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji.
 
Kuna wakati unajiuliza, hawa viongozi wanateuliwa kwa kuzingatia nini?

Awamu iliyopita utalii ulikuwa unakua kwa 15%, awamu hii inakua kwa 3.6%, halafu bado unaamini kuna wajinga watakaoamini kuwa masharti ya uendeshaji biashara ya utalii, yameboreshwa!

Kwa hili ya sasa, kuhamasisha watu kuwekeza kwenye sekta ya utalii, ni lazima ujitoe akili kiasi.

Mwanadamu mwenye akili, kukiwa na uhaba wa fedha, huamua kupunguza matumizi, na matumizi ya mwanzo kabisa kupunguzwa, ni matumizi ya anasa. Utalii ni necessity au anasa? Hivi unaweza kwenda wodini ukawatangazia wagonjwa uwepo wa tamasha la mwanamuziki mashuhuri usiku wa leo kwenye ukumbi wa Diamond?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom