Waziri Kawambwa funguka! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri Kawambwa funguka!

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by MziziMkavu, Aug 15, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Aug 15, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Jana Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi iliwasilisha makadirio ya matumizi kwa mwaka wa fedha wa 2012/13 huku ikieleza kuwa inajipanga kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoikabili.

  Miongoni mwake ni kuboresha ubora wa elimu nchini; kuongeza upatikanaji wa samani na miundombinu kwa shule nchini, vifaa vya kufundishia hasa masomo ya sayansi na kubuni vyanzo vipya vya mapato kwa ajili ya kugharimia elimu ya juu.

  Katika makadirio hayo yaliyowasilishwa na Waziri wake, Dk. Shukuru Kawambwa, kwa mwaka wa fedha huu fedha za mkopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu kupitia Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu zimeongezeka kutoka Sh. bilioni 91.72 za mwaka wa fedha uliopita hadi Sh. bilioni 306 mwaka huu, kwa maana hiyo kuwa na uwezo wa kuwakopesha wanafunzi wengi zaidi.

  Katika hotuba hiyo ambayo pia ilionyesha mafanikio katika kupunguza pengo la walimu na wanafunzi kutoka mwalimu mmoja kwa wanafunzi 51 (1:51) kwa mwaka jana, hali imekuwa bora zaidi mwaka huu kwani sasa ni mwalimu mmoja kwa wanafunzi 46 (1:46), ikimaanisha kuwa mzigo kwa walimu unapungua, lakini pia nafuu inapatikana kwa wanafunzi kwa kumsikia mwalimu kwa karibu zaidi.

  Hata hivyo, pamoja na kueleza mafanikio na changamoto hizo, bado Waziri ama alikwepa au alipuuzia kuzungumzia kwa kina suala zima la mgogoro wa walimu na serikali juu ya nyongeza ya mishahara yao kwa asilimia 100, nyongeza ya posho ya kufundisha ya asilimia 55 kwa walimu wa sayansi na asilimia 50 kwa walimu wa sanaa, pia posho ya mazingira magumu ya asilimia 30 kwa walimu wote nchini.

  Pamoja na ukwepaji huo, Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii pamoja na hutuba ya kambi ya upinzani kwa wizara hiyo, ilieleza kwa mapana yake madhara ya mgogoro wa walimu na hatima ya elimu ya taifa hili.

  Tunajua serikali kwa nyakati tofauti, akiwamo Waziri Kawambwa mwenyewe walikwisha kuzungumzia suala la mgogoro wa walimu juu ya nyongeza ya mshahara, lakini kwa hakika haikuwa kitu cha kuwekwa pembeni katika uwasilishaji wa makadirio yake bungeni kwa kuwa ndiyo fursa muhimu na ya pekee ya kujieleza kwa wabunge na hatua ambazo zimechukuliwa na ambazo zinatarajiwa kuchukuliwa kujenga mustakabali mwema wa walimu kwa ajili ya kuokoa elimu ya taifa hili.

  Kamati ya Bunge yanye wajibu wa kusimamia na kupitia bajeti ya wizara husika hata kabla ya kuwasilishwa bungeni, imetambua kuwa kuna shida katika sekta ya elimu kwa jinsi mgomo wa walimu ulivyomalizwa kwa amri ya mahakama. Imesema wazi kuwa ni vema serikali ikarejea kwenye meza ya mazungumzo na walimu ili kujenga maelewano.

  Hoja kama hiyo ilijengwa pia na kambi ya upinzani kwani hali ilivyo sasa ni kama walimu wameingia katika mgomo baridi ambao madhara yake ni makubwa zaidi kuliko mgomo halisi. Kwa hiyo, kukwepa au kupuuza tu kuzungumzia hali ilivyo hakuondoi tatizo, kinyume chake ni kuzidi kujenga hali ya uhasama baina ya walimu na serikali na waathirika ni wanafunzi ambao ni nguzo ya taifa hili hapo kesho.

  Kadhalika, Waziri alizungumzia juu ya ongezeko la kufaulu kwa wanafunzi wa darasa la saba kwenda sekondari, lakini pamoja na kufurahia takwimu nzuri bado hakuona haja ya kugusia japo kwa mstari mmoja tu janga la wanafunzi zaidi ya 5,000 ambao walijiunga na elimu ya sekondari katika shule za sekondari za kata ilhali hata hawajui kusoma wala kuandika!

  Inawezekana suala la kughushi wanafunzi waliongia kidato cha kwanza ni dogo kwa wizara kwa ujumla wake, lakini ni moja ya kielelezo kuwa mfumo wa elimu nchini una matatizo makubwa, uwajibikaji hauna tena nafasi, ndiyo maana kuna watumishi wa umma tena walimu wanakuwa na ujasiri wa kufanya kituko kama hicho wakiamini kuwa hawatakamatwa. Ni jambo la bahati mbaya kwamba waziri na hili alilikwepa.

  Tunasema tena kama ambavyo tulikwisha kusema huko nyuma, wizara hii ni sawa na mshipa mkuu wa fahamu, uzembe, kubweteka au aina nyingine yoyote ya kutokujali ikiruhusiwa ndani yake, hakika anayeangamia siyo mwalimu au mwanafunzi, ila tunalizika taifa zima kwa ujumla wake, ni wakati wa waziri wa wizara hii kuwaza kwa mapana anapowasilisha hotuba ya matumizi ya wizara yake bungeni ili kuomba kungwa mkono kwa kuwa muwazi na changamoto zinazomkabili.
  CHANZO: NIPASHE

   
 2. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #2
  Aug 15, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Ahsante kwa habari muruwa yenye kuonesha muelekeo mzuri.
   
 3. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #3
  Aug 15, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Wakujenga shule za kata ambazo hazina walimu? Wakati watoto wao wanasoma nje ya nchi kweli wewe ni zomba la misitu ya pande
   
 4. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #4
  Aug 15, 2012
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  mbona hajaelezea malimbikizo ya mishahara ya walimu maana hua tunashangaa wanasema wameshatulipa wakati wilaya kibao bado zinadai yaani hizi siasa bana zinatisha kiukweli kwa sasa hii migomo baridi haitaisha wasiojuakusoma na kuandika hadi vyuo vikuu watafika yaani kuna vitu vinafichwa kabisa na viongozi hawa hawavisemi kiukweli sisi tuliopo mashuleni ndio tunaoona kila kitu
   
 5. msnajo

  msnajo JF-Expert Member

  #5
  Aug 15, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 2,464
  Likes Received: 331
  Trophy Points: 180
  Elimu yetu ipo icu.
   
 6. mansakankanmusa

  mansakankanmusa JF-Expert Member

  #6
  Aug 15, 2012
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 4,092
  Likes Received: 603
  Trophy Points: 280
  kuna jamaa anafundisha kibaha, amemshangaa sana waziri, eti mkoa anaotoka waziri walimu hawadai
   
 7. m

  medalgal Member

  #7
  Aug 15, 2012
  Joined: Aug 1, 2012
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Maisha magumu Dodoma tu na ndo maana wanalipana 2,000,000 kwa cku ilhali mwalm analipwa laki 2 kwa mwezi.
   
 8. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #8
  Aug 15, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Watoto wa kina Mbowe ndio wanasoma shule za kata au sio? kwi kwi kwi teh teh teh!

  Mabwepande patamu, muulize Ulimboka, kishakuwa addicted na leo yuko huko anajidai amekwenda bagamoyo, yule na bagamoyo wapi na wapi? aseme kweli tu. Kapenda.
   
 9. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #9
  Aug 15, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Mkuu naona unataka kuniharibia swaumu yangu hujui leo ni chungu cha 26 kwi! kwi! kwi! teh
   
 10. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #10
  Aug 15, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,333
  Likes Received: 1,796
  Trophy Points: 280
  Huyu jamaa alikuwa mwalimu mzuri sana wa sub-department ya energy, mechanical engineering department au IPI ya enzi hizo. I dont think ni politician...but he is a nice chap!
   
 11. F

  Fredmaty Zach. Member

  #11
  Aug 15, 2012
  Joined: Jul 26, 2012
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  walimu tunahali ngumu, ingawa tunao umuhimu. hii secta nyeti na ndiyo njia na mwanga wa secta zingine zote. bila walimu we mtanzania ungekuwa mgeni wa nan? hata waziri wa secta huska anashindwa kutetea walimu wake, tutazidi kuangamiza taifa kwa uroho na ubwanyenye wa viongozi wachache, hiyo elimu bora inayopatikana huko nchi za wenzetu ni kwa sababu ya masirahi mazuri ya walimu, kwanini isiwe Tanzania? eti madai ya walimu hayalipiki, walimu endeleen kuandaa F hao wachache mliotoa wametosha, na matokeo yake ndo hayo, wanawazomea.
   
Loading...