MGODI wa madini ya rubi unaomilikiwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Profesa Juma Kapuya, uliopo wilayani Longido, mkoani Arusha, umeibiwa mashine ya kupulizia hewa ndani ya mgodi (compressor).
Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Basilio Matei, zinaeleza kuwa wizi huo ulitokea Septemba 16, mwaka huu, wakati wa usiku katika mgodi huo uliopo katika Kijiji cha Kiseeriani.
Kamanda Matei alisema kwamnba kutokana na tukio hilo, watu wanne wanashikiliwa na polisi. Aliwataja watu hao kuwa ni Nyinyila Mwambasa (31), dereva wa gari aina ya Fuso lenye namba za usajili T 826 AJT, mkazi wa Makao Mapya, Arusha, Daniel Barnabas (2, mkazi wa Lendikinya wilayani Monduli, Lomayani Kalea (25), mkazi wa Buguruni Namanga na Jumanne Ramadhani (26), mkazi wa Arusha.
Akielezea tukio hilo, Kamanda Matei alisema kwamba watu hao baada ya kuiba mashine hiyo walitoroka kwa kutumia gari hilo, lakini walikamatwa walipofika maeneo ya Namanga.
Alisema kwamba wizi huo ulipangwa kwa muda mrefu na baadhi ya watumishi wa mgodi huo kwa kuwa si rahisi kwa watu wa nje kuweza kuingia ndani ya mgodi bila mwenyeji.
Katika tukio jingine, Kamanda Matei alisema kwamba majambazi watatu wakiwa na silaha za moto, jana, walimjeruhi kwa risasi Mhasibu wa kampuni ya Utalii ya Abacombe and Kent ya Arusha, Fabiana Mhindi, wakati akiwa katika gari la kampuni hiyo lililokuwa na fedha alipokuwa akitokea benki ya NBC.
Alisema tukio hilo ambalo majambazi hao hawakufanikiwa kupora fedha zilizokadiriwa kuwa sh milioni 2.8 lilifanyika jana saa 9.45 alasiri, nje ya lango kuu la kuingilia ofisi za kampuni hiyo.
Alisema baada ya mhasibu huyo kufika katika lango hilo akiwa na dereva Athuman Mnyombe (35), aliyekuwa akiendesha gari aina ya Toyota Land Cruiser yenye namba za usajili T869 AFL wakisubiri kufunguliwa lango hilo, ghafla walitokea watu watatu wakiwa katika pikipiki yenye namba T199 AMB na kuwavamia.
Baada ya kuvamia walifyatua risasi moja hewani ili kuwatisha kabla ya kupiga risasi nyingine katika kioo cha mbele cha gari hilo, iliyomjeruhi mhasibu huyo begani.
Mara baada ya kutokea kwa jambo hilo mhasibu huyo alitoa taarifa polisi waliofanikiwa kuwakamata majambazi wawili kati ya watatu katika eneo jirani na hoteli ya kitalii ya Impala.
Aliwataja watu wanaoshikiliwa kuwa ni Samuel Lucas (23), mkazi wa Sakina Kiranyi na Emmanuel Willium (23), mkazi wa Ekenywa wilayani Arumeru.
What is so special kwa Kapuya kuibiwa. Watanzania wangapi wanaibiwa kila siku?
Nia hasa ya kupost article hii ni hiyo habari kwamba mgodi huo unamilikiwa na Waziri. Je mawaziri na Vingunge wangapi katika nchi yetu wana migodi yao binafsi? Je ni halali kwa mtu binafsi kuwa na mgodi wake badala ya rasilimali hizi kuwa za Watanzania wote?
Waandishi wana "sense of news" wanapima na kuona kuwa ni kitu gani kinaweza kufanya jambo kuwa habari. Kwa harakaharaka mimi naona aliyeandika habari hiyo ana high sense of news; Bila shaka kaangalia mambo/vigezo matatu kutengeneza hiyo habari 1. Kapuya ni waziri 2. Alipata ajalijuzijuzi 3. Suala la kumiliki mgodi. Tukianza na kigezo cha kwanza, kwa kuwa Prof. Kapuya ni waziri, tena wa ulinzi anajulina na ana uzito katika jamii, kwa hivyo hata kama angeibiwa nyumbani kwake ingeandikwa na bado ikawa na uzito. Kigezo cha pili kinaweza kutumika kwa lengo la kuionesha jamii juu ya namna gani anazidi kuandamwa na masahibu. Na Kigezo cha tatu bila shaka kinazingatia ukweli kuwa suala la migodi/madini kwa sasa linazungumzwa/liko katika mjadala mkubwa katika jamii yetu.
Kuhusu kumiliki kwake mgodi kama waziri mimi sioni kama kuna tatizo sana. Kwa jinsi ninavyoelewa, mara nyingi madini ya rubi yanachimbwa na wachimbaji wadogo wadogo na mtu yeyote kwa nafasi yake nadhani anaweza kufanya hivyo.
Jamani na mimi nataka Plot huko Longido kwenye madini in particular, nifanyeje nipate, au mpaka niwe kwenye Cabinet
What is so special kwa Kapuya kuibiwa. Watanzania wangapi wanaibiwa kila siku?
Du Mzee naona sasa baadhi ya watanzania tumeingiwa na sumu. sikukufikiria haraka hiyo thread on that angle. Kweli, nadhani mwandishi angesema tu Kapuya naye anamiliki mgodi!
Jamani na mimi nataka Plot huko Longido kwenye madini in particular, nifanyeje nipate, au mpaka niwe kwenye Cabinet
August Migodi Ipo Kama Mchingoma Alivyosema Aacha Kulaliwa Mpaka Uteme..usishangae Kuambiwa Ukamkate Kichwa Mama Yako Au Ndugu Yoyote Chimbo Liteme Utaweza ,,anachofanya Kapuya Na Jk Na Ra Wanajua Wenyewe Wewe Utaweza?????karibu
Hakuna jipya lolote Mh. Kapuya kumiliki mgodi, wala hakuna ubaya wowote, labda tu mwandishi kaamua 'kutuuzia' gazeti.
Mwaka 1995 nilibahatika kutembelea sehemu za 'machimbo' ya madini kule Tunduru, enzi hizo jiwe lilokuwa linatoka lilikuwa ALEXANDERLITE, na kule maeneo ya babati -KANGALA ambako vijana walikuwa wanachimba RODLITE. Niliyoyaona huko mpaka leo nimeamini jinsi watu wakiamua, wanavyojituma na migodi yao kuitafuta shilingi. (Japo kuna waliokufuru mfano jamaa mmoja ambaye baada ya kuuza mawe yake ya ALEXANDERLITE kwa Tshs 500,000,000/=, YES, Millioni Mia tano!, jamaa alinunua Landrover hapo hapo Tunduru, na kulikosha kwa bia!)
Wajemeni, Tanzania imebarikiwa madini ya kila aina kwa aina, na sehemu zote hizo nilizokwenda kuna wachimbaji wadogo wanaoendesha maisha yao kwa huo uchimbaji 'wa kubahatisha', na kuuza 'mawe' yao kwa wa-thai kuanzia kule kule Tunduru mpaka pale Upanga, nk.
Biashara ya madini ngumu wazee asikwambie mtu. Ukiona Sunda, au Askofu nk waliibua 'mawe' ya TANZANITE ya mamilioni ya shilingi jua cha moto walikiona, kwani kazi hiyo hawakuifanya kwa siku au mwezi mmoja! (Askofu alipochanganyikiwa na kuanza kuzimwaga pesa toka ghorofani pale Palsons Hotel, ilikuwa ni mfano tosha wa 'wazimu' wa mawe!)
Sehemu nyingi nchini Tanzania bado kuna wachimbaji wengi wadogo walojianzishia 'migodi' yao,... na serikali sana sana inatumia watendaji wa vijiji ku control, kwani kinachopatikana sana sana kinamfaa huyu mchimbaji na kidogo mfanyabiashara (middle man) anayelipeleka kuuza jiwe mjini.
Kwahiyo ndugu yangu AUGUST kama kweli unataka plot, jifungashe ukaweke kambi huko Longido,...ila ujue mgodi mpaka 'uteme', kazi umeifanya, na kati ya hayo mawe utayoyapata tegemea ma rejekti kibao na kulaliwa kwa sana na wa thailand.
Kwa maoni yangu kuna tofauti kubwa ya wachimbaji wadogo wadogo kujitafuria riziki na viongozi wa juu wa Chama na Serikali kuwa wanahodhi machimbo ya madini ya aina yeyote. Leo wanaown machimbo ya Rubi kesho itakuwa machimbo ya almasi na dhahabu. Hii rasilimali ni ya Watanzania wote hivyo pato lake linastahili kuingia kwenye mfuko wa Taifa badala ya watu binafsi. Kwa maoni yangu si haki kwa watu binafsi kuown rasilimali za Watanzania (migodi ya madini) Si tulishasikia hapa kwamba Yona na Mkapa wanaown Kiwira Coal Mining? Je nani aliwapa haki ya kuown KCM? Walilipa kiasi gani na kwa nani?
Kiswahili kinakuwa tatizo hata kwa waswahili wenyewe... WAZIRI KAPUYA AIBIWA! mbona taarifa nilizonazo ni kuwa waziri Kapuya leo kapelekwa India kwa matibabu zaidi sasa ataibiwa vipi naomba ufafanuzi hapo..
Kilichoibwa ni hivyo vitu sio waziri...
Teh teh teh teh