issenye
JF-Expert Member
- Feb 2, 2011
- 3,795
- 5,255
Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amesema akifa anatamani azikwe na Ilani ya uchaguzi wa CCM itakayokuwepo wakati huo.
Lugola ametoa kauli hiyo leo Jumapili Julai 8, 2018 katika mahojiano maalum na MCL Digital baada ya kutembelea ofisi za kampuni ya Mwananchi Communications Ltd (MCL) inayochapisha magazeti ya Mwananchi, The Citizen na Mwanaspoti.
Amesema hakuna ilani kama ya CCM miongoni mwa vyama mbalimbali vya siasa nchini, anapenda kutembea nayo kila wakati akiwa anatekeleza shughuli mbalimbali za Serikali.
Amesema alikabidhiwa ilani hiyo na Rais John Magufuli wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 katika mkutano wa hadhara uliofanyika jimboni kwake, Mwibara Wilaya ya Bunda mkoani Mara.
“Alinikabidhi na kunieleza nihakikishe ninakwenda kuisimamia. Tangu nimekabidhiwa nikasema muda wowote nitakaowatumikia Watanzania Ilani hii itakuwa kitendea kazi namba moja,” amesema.
“Muda wote ilani hii itakuwa kitabu rejea kwa sababu muda wote nitakuwa kazini hivyo lazima nipate rejea kwa ajili ya kutekeleza.”
Chanzo: Mwananchi