Waziri Kairuki atoa tamko nyongeza ya mshahara

Kwa ufupi
Serikali ya Awamu ya Tano tangu iingie madarakani imekuwa ikifanya uhakiki wa watumishi wa umma na kukagua vyeti ili kubaini vilivyo bandia.

Dodoma. Serikali imesema bado haijapandisha mishahara lakini hilo litafanyika wakati wowote kuanzia sasa.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki amesema Serikali haikupandisha mishahara kutokana na sakata la watumishi hewa na vyeti feki ambalo mchakato wake sasa umekwisha.

“Tayari Serikali imeshatenga Sh600 bilioni kwa ajili ya kuanza kupandisha madaraja wafanyakazi wote ambao wanastahili,” amesema.

Kairuki alikuwa akijibu swali la mbunge wa Viti Maalumu Chadema, Susan Masele ambaye pia ametaka kujua kuhusu idadi ya vibali vya ajira vilivyotolewa na Serikali.

Waziri amesema Serikali imeshasaini vibali 10,000 kwa ajili ya kutoa ajira na vingine 4,000 viko mbioni kusainiwa.

Amesema sehemu itakayoangaliwa kwanza katika kuajiri ni nafasi za walimu na idara ya afya ambazo ndizo zilionekana kuathiriwa zaidi na vyeti feki.

Chanzo: Mwananchi
Huyu kafunika kombe mwanaharamu apite,nyongeza haipo hadi Yesu atakaporejea ingawa kuna lijamaa linadai eti Yesu alikula nauli.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna lolote. Hakuna cha bilioni 600 wala nini. Waziri alishatoa matamko mengi kama hayo na hakuna lililotekelezwa. Kifupi watumishi wamekata tamaa maana hata haki zao za msingi kama increments nazo zimezuiwa. Na kama uhakiki umemalizika kipi kinachomzuia kutoa tamko linaloeleweka?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa ufupi
Serikali ya Awamu ya Tano tangu iingie madarakani imekuwa ikifanya uhakiki wa watumishi wa umma na kukagua vyeti ili kubaini vilivyo bandia.

Dodoma. Serikali imesema bado haijapandisha mishahara lakini hilo litafanyika wakati wowote kuanzia sasa.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki amesema Serikali haikupandisha mishahara kutokana na sakata la watumishi hewa na vyeti feki ambalo mchakato wake sasa umekwisha.

“Tayari Serikali imeshatenga Sh600 bilioni kwa ajili ya kuanza kupandisha madaraja wafanyakazi wote ambao wanastahili,” amesema.

Kairuki alikuwa akijibu swali la mbunge wa Viti Maalumu Chadema, Susan Masele ambaye pia ametaka kujua kuhusu idadi ya vibali vya ajira vilivyotolewa na Serikali.

Waziri amesema Serikali imeshasaini vibali 10,000 kwa ajili ya kutoa ajira na vingine 4,000 viko mbioni kusainiwa.

Amesema sehemu itakayoangaliwa kwanza katika kuajiri ni nafasi za walimu na idara ya afya ambazo ndizo zilionekana kuathiriwa zaidi na vyeti feki.

Chanzo: Mwananchi
Hivi huyu ni mmoja ya wale mkulu alowaita wa.pu.mb.avu?
 
Porojo mwaka wa tatu sasa

Mwaka wa tatu wa nani au wa nini. Tulia fanya hesabu then post. September 5, 2017 - November 5, 2015 = Mwaka mmoja (1) na miezi kumi (10) sasa hiyo miaka mitatu umeipataje? Ok, tumejua tatizo lako, asante kwa kupost
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom