Waziri Kairuki atoa tamko nyongeza ya mshahara

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
28,013
Reaction score
64,054
Kwa ufupi
Serikali ya Awamu ya Tano tangu iingie madarakani imekuwa ikifanya uhakiki wa watumishi wa umma na kukagua vyeti ili kubaini vilivyo bandia.

Dodoma. Serikali imesema bado haijapandisha mishahara lakini hilo litafanyika wakati wowote kuanzia sasa.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki amesema Serikali haikupandisha mishahara kutokana na sakata la watumishi hewa na vyeti feki ambalo mchakato wake sasa umekwisha.

“Tayari Serikali imeshatenga Sh600 bilioni kwa ajili ya kuanza kupandisha madaraja wafanyakazi wote ambao wanastahili,” amesema.

Kairuki alikuwa akijibu swali la mbunge wa Viti Maalumu Chadema, Susan Masele ambaye pia ametaka kujua kuhusu idadi ya vibali vya ajira vilivyotolewa na Serikali.

Waziri amesema Serikali imeshasaini vibali 10,000 kwa ajili ya kutoa ajira na vingine 4,000 viko mbioni kusainiwa.

Amesema sehemu itakayoangaliwa kwanza katika kuajiri ni nafasi za walimu na idara ya afya ambazo ndizo zilionekana kuathiriwa zaidi na vyeti feki.

Chanzo: Mwananchi
 
Huyu Dada naye angekaa kimya tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maymosi mkuu mwenyewe alitamka

Ila mwaka mpya wa fedha umesha anza na miezi isiyopungua miwili imekata lakini hakuna chochote sembuse kauli ya kairuki?

Yes hatukatai kuwa wataongeza. Swali ni je wanaongeza kwa wakati kama taratibu na kanuni za kiutumishi zinavyo taka?
 
Mawaziri wote wanatekeleza matakwa ya bosi wao. Wa kulaumiwa baba J.
 
Kwa ufupi
Serikali ya Awamu ya Tano tangu iingie madarakani imekuwa ikifanya uhakiki wa watumishi wa umma na kukagua vyeti ili kubaini vilivyo bandia.

Dodoma. Serikali imesema bado haijapandisha mishahara lakini hilo litafanyika wakati wowote kuanzia sasa.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki amesema Serikali haikupandisha mishahara kutokana na sakata la watumishi hewa na vyeti feki ambalo mchakato wake sasa umekwisha.

“Tayari Serikali imeshatenga Sh600 bilioni kwa ajili ya kuanza kupandisha madaraja wafanyakazi wote ambao wanastahili,” amesema.

Kairuki alikuwa akijibu swali la mbunge wa Viti Maalumu Chadema, Susan Masele ambaye pia ametaka kujua kuhusu idadi ya vibali vya ajira vilivyotolewa na Serikali.

Waziri amesema Serikali imeshasaini vibali 10,000 kwa ajili ya kutoa ajira na vingine 4,000 viko mbioni kusainiwa.

Amesema sehemu itakayoangaliwa kwanza katika kuajiri ni nafasi za walimu na idara ya afya ambazo ndizo zilionekana kuathiriwa zaidi na vyeti feki.

Chanzo: Mwananchi

Amri ya Tisa ya Mungu inasema Usimshuhudie jirani yako uongo ningemshauri huyu mama asizungumzie ishu hii tena, hakuna aliyemdai nyongeza...............tunapambana na hali yetu.
 
Back
Top Bottom