Waziri Kabudi amteua Patrick Nyembera kuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa nchini (TPBRC)

Waziri Kabudi amteua Patrick Nyembera kuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa nchini (TPBRC)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,499
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Palamagamba Kabudi, amemteua mtangazaji wa Azam TV Patrick Nyembera kuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa nchini (TPBRC), baada ya kamati ya awali kumaliza muda wake.

1755245430582.png
Nyembera ataiongoza Kamati hiyo ya muda ya TPBRC, yenye jumla ya wajumbe sita ikiwa na Mwenyekiti na Makamu wake.

Soma > Waziri Prof. Kabudi aufuta Uongozi wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBRC) kutokana na tuhuma mbalimbali

Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara iliyotolewa leo, Profesa Kabudi ameipa kamati hiyo siku 90 (kuanzia Julai 29 hadi Oktoba 29) kukamilisha marekebisho ya katiba na kuitisha uchaguzi mkuu.

Wajumbe wapya walioteuliwa ni:
i. Patrick Nyembera(Mwenyekiti)
ii. Jackobu Mbuya (Makamu Mwenyekiti
iii. Gordon Nsajigwa(Katibu)
iV. Shafii Dauda (Mjumbe)
V. Irene Mwasanga (Mjumbe)
Vi. Ibrahim Abbas Kamwe (Mjumbe)
 
  • Thanks
Reactions: K11
Kwa sasa nimeacha kufuatilia michezo hiyo baada ya kuona washindi wa mchongo kila awamu.
 
Na vipi kuhusu uchaguzi wa TFF! Bado uko palepale pamoja na ukweli kwamba rais wa sasa wa TFF anataka kupindisha sera ya Taifa ya michezo kwa viongozi wake kuhudumu kwenye nywzfa zao kwa vipindi viwili pekee?
 
Back
Top Bottom