Junior ambaye juzi Jumatatu alisaini mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia Azam, amesema Yanga ndiyo ilikuwa timu ya kwanza kumuhitaji, lakini aliona hawaeleweki ndiyo maana akatua Azam.
Mshambulizi huyo ambaye baada ya kusaini Azam amepewa jezi namba saba, amesema: “Nilienda Yanga, tukaongea, nikapiga picha na kombe, lakini mwisho wa siku nimekuja kuwa mchezaji wa Azam. Hii inatokea hata Ulaya.
“Yanga hawakuwa siriazi ndiyo maana sijajiunga nao, lakini pia Azam ilikuwa ni timu ya ndotoni kwangu kwamba siku moja nije kuichezea, sasa ndoto zangu zimetimia.”
Junior aliongeza kuwa, baada ya kuondoka John Bocco ndani ya Azam, atajitahidi kuhakikisha anavaa viatu vya straika huyo mkongwe na kuziba pengo lake.
Naye Ofisa Habari wa Azam, jaffar Idd, amesema usajili huo ni mwanzo tu, wanaendelea kufanya mambo kisasa kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri msimu ujao.
Chanzo: Salehe Jembe