Waziri Innocent Bashungwa: TBC inatazamwa na wananchi wengi ndani na nje ya nchi

Rufiji dam

JF-Expert Member
Feb 20, 2020
3,803
8,796
WAZIRI: TBC INATAZAMWA NA WANANCHI WENGI NDANI NA NJE YA NCHI

Serikali imelipongeza Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kutokana maboresho makubwa iliyofanya kwenye vipindi vyake mbalimbali na kuahidi kuendelea kutenga bajeti ya kutosha kwa ajili ya kugharamia uendeshaji wa shirika hilo.

Pongezi hizo zimetolewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa wakati wa ziara yake katika ofisi za TBC jijini Dar es salaam.

Amesema maboresho makubwa yaliyofanywa na TBC katika vipindi vyake mbalimbali, yamesababisha vipindi hivyo kuwa na wapenzi wengi ndani na nje ya nchi.

"Kwa kweli TBC inatazamwa na watu wengi, mfano wa wazi ni Rais wa Uganda Yoweri Museveni, mara kadhaa amekuwa akiisifia TBC, hii inaonesha kupendwa kwake ndani na nje ya nchi," amesema Waziri Bashungwa.

Akiwa ameongozana na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Abdallah Ulega na Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dkt Hassan Abbasi, Viongozi hao wamepata fursa ya kutembelea vitengo mbalimbali vya TBC na kupatiwa maelezo ya utendaji kazi wake.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TBC Dkt Ayub Rioba Chacha amesema shirika hilo litaendelea kuboresha vipindi vyake mbalimbali, pamoja na kuboresha usikivu wa matangazo yake.

"Pamoja na kufanya vizuri kwa kipindi hiki, lakini bado tuna changamoto, na kubwa ni kutokuwa na bajeti ya kutosha ya maendeleo," ameongeza Dkt Rioba.

Shirika la Utangazaji Tanzania linamiliki vituo vitatu vya televisheni na vitatu vya redio.
 
Natamani kufanya kazi hapo TBC, naomba connection tafadhali kwa wenye uwezo wa kunisaidia.
 
Huyu waziri anaonekana Kama ana asili ya Rwanda vile.
Waziri wa habari hajui Tbccm ndio tv ya hovyo kuliko hata hizi za You Tube
 
WAZIRI: TBC INATAZAMWA NA WANANCHI WENGI NDANI NA NJE YA NCHI

Serikali imelipongeza Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kutokana maboresho makubwa iliyofanya kwenye vipindi vyake mbalimbali na kuahidi kuendelea kutenga bajeti ya kutosha kwa ajili ya kugharamia uendeshaji wa shirika hilo.

Pongezi hizo zimetolewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa wakati wa ziara yake katika ofisi za TBC jijini Dar es salaam.

Amesema maboresho makubwa yaliyofanywa na TBC katika vipindi vyake mbalimbali, yamesababisha vipindi hivyo kuwa na wapenzi wengi ndani na nje ya nchi.

"Kwa kweli TBC inatazamwa na watu wengi, mfano wa wazi ni Rais wa Uganda Yoweri Museveni, mara kadhaa amekuwa akiisifia TBC, hii inaonesha kupendwa kwake ndani na nje ya nchi," amesema Waziri Bashungwa.

Akiwa ameongozana na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Abdallah Ulega na Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dkt Hassan Abbasi, Viongozi hao wamepata fursa ya kutembelea vitengo mbalimbali vya TBC na kupatiwa maelezo ya utendaji kazi wake.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TBC Dkt Ayub Rioba Chacha amesema shirika hilo litaendelea kuboresha vipindi vyake mbalimbali, pamoja na kuboresha usikivu wa matangazo yake.

"Pamoja na kufanya vizuri kwa kipindi hiki, lakini bado tuna changamoto, na kubwa ni kutokuwa na bajeti ya kutosha ya maendeleo," ameongeza Dkt Rioba.

Shirika la Utangazaji Tanzania linamiliki vituo vitatu vya televisheni na vitatu vya redio.
Nyumbani kwangu TBC marufuku. Ni Kama shetani asivyothubutu kuchungulia mbinguni.
 
Hivi tbc nayo ni channel ya kuangalia? Na wafanyakazi wa pale nao watasimama mbele ya watu wakiwa wamekaza misuli ya matako wakijinasibu ni wafanyakazi wa tbccm!!

SMH! Vibweka haviishi dunia hii
 
Back
Top Bottom