Waziri Hamza: Mapato ya Muungano ukitoa matumizi kinachobaki ndio Tugawane Zanzibar na Bara na siyo hii 4.5% tunayopata sasa!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,013
142,048
Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar mh Hamza amesema ndani ya miezi 6 kikokotoo cha Mapato ya Muungano kinaweza kubadilika kufuatia mazungumzo yanayoendelea Kati ya Serikal ya JMT na SMZ

Hamza amesema kwa sasa Zanzibar inapata 4.5% ya Mapato ya Muungano kitu ambacho siyo sahihi kabisa

Hamza amesema kimsingi inatakiwa Uchukue Mapato ya Muungano Utoe Matumizi ya Muungano na kinachobaki yaani Salio ndio ligawanywe kwa Zanzibar na Bara

Source ITV Dakika 45
 
Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar mh Hamza amesema ndani ya miezi 6 kikokotoo cha Mapato ya Muungano kinaweza kubadilika kufuatia mazungumzo yanayoendelea Kati ya Serikal ya JMT na SMZ...

Hakuna muungano. Huu ni uvamizi wa Nyerere uliopewa jina la muungano.

Hakuna chochote kitachokwenda ikiwa Hao wanaosema hayo wamewekwa madarakani na Jeshi la Tanganyika
 
Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar mh Hamza amesema ndani ya miezi 6 kikokotoo cha Mapato ya Muungano kinaweza kubadilika kufuatia mazungumzo yanayoendelea Kati ya Serikal ya JMT na SMZ...
Huyo waziri hafahamu alisemalo, ana kurupuka na kuhororoja bila uelewa.

Tanzania toka lini mapato yanabaki (surplus)?

Bajeti yenyewe mpaka leo miaka zaidi ya 60 baada ya Uhuru bado tunasaidiwa bajeti yetu.
 
Kwa structure ya Muungano huu, ndo hawatopata hata shilingi. Huyu fundi cherehani Hamza ni kilaza mmoja hivi ambaye hawezi kujua impact ya akisemacho.

Kabla ya kujadili namna ya kugawana mapato ya Muungano, yabidi kwanza kubaini hayo mapato ya Muungano. Yeye akiambiwa atofautishe mapato ya Muungano na yasiyo ya Muungano ataweza?

Zanzibar shouldn't take an advantage of having a union president from Zanzibar to push for "unresolved" issues. Watamharibia maza na wao wasipate chochote.
 
Hakuna muungano. Huu ni uvamizi wa Nyerere uliopewa jina la muungano.
Hakuna chochote kitachokwenda ikiwa Hao wanaosema hayo wameweka madarakani na Jeshi la Tanganyika
Lakini mkumbuke Nyerere alisema ndani ya muungano ndio watasema sisi ni wazanzibari na wao ni watanganyika lakini nje ya muungano watu watasema sisi ni wapemba na wao ni waunguja 😅😅🙏🙏 ! Utata !!
 
Back
Top Bottom