Mgeni wa Jiji
JF-Expert Member
- Jul 27, 2017
- 10,484
- 19,987
Habari wana JF
Leo ni siku nyingine tena, natumaini mnaendelea vizuri kwa wale wenye changamoto basi Muumba awafanyie wepesi.
Leo sina mambo mengi sana zaidi ya kuyatafakari maadili yetu yanayozidi kuporomoka kwa kasi. Na nitoe pongezi kwa Waziri Dr. Dorothi Gwajima kwa kuchukua hatua za awali na kuonesha kuguswa na video ya wanafunzi wanaonengua kwa mtindo unaohoji maadili yetu inayosambaa mitandaoni (ikiwa ni video ya shule nchini Tanzania basi tutafakari zaidi).
Wakati tunaendelea na hili la wanafunzi kunengua naomba kutoa duku duku langu juu ya kile kinachoitwa sanaa ya uchekeshaji na upotoshaji wa maadili yetu.
Kwa mujibu wa takwimu za jeshi la polisi zinaonesha kwa kipindi cha mwaka 2017 - 2021 jumla ya matukio ya ukatili dhidi ya watoto 70,997 yaliripotiwa sawa na wastani wa matukio 14,199 kila mwaka. Huku upande wa ukatili wa kingono inaonekana wasichana 3 kati ya 10 wamebakwa wakiwa chini ya miaka 18 huku 13.4% ya wavulana wenye umri huo wakiripotiwa kulawitiwa.
Hizi sio habari nzuri hata kidogo. Lakini inapasa tujiulize haya yote yanatokea vipi?. Katika tafiti zangu huko mitandaoni hususa Tiktok, Facebook na Instagram nimekutana na mzee mmoja anayefanya maudhui ya uchekeshaji (japo hayafurahishi hata kidogo).
Huyu mzee (jina simjui) video zake zipo sana mitandao ya Tiktok na Instagram, huyu mzee amekuwa akirekodi vipand vifupi vya video na vijana wawili wakiume na maudhui yao ni kuwa huyu mzee anawatamanishakwa vitu na kuwaambia ili wavipate basi na wao wampe kitu kwa maana ya awalawiti.
Aina hii ya kinachoitwa uchekeshaji ni hatari kwa maadili yetu na hasa kwa watoto wadogo na vijana walio kwenye balehe.
Huu sio uchekeshaji, na hakuna kichekesho kwenye ukatili wa kijinsia na tabia za kibazazi zinazooneshwa kwenyevideo hizo.
Waziri Dkt. Gwajima D utakubaliana na mimi kuwa haya yote yanafifisha juhudi za sera ya ulinzi na usalama wa mtoto inayopambaniwa kueleweka na kutekelezwa mashuleni na mitaani alipo mtoto.
Ni ombi langu hasa kwako kwakuwa ni waziti unayeonesha kuyafanyia kazi mambo mengi yanayoendelea mtandaoni, ni ombi langu mzee huyu na vijana hao waitwe na kuhojiwa vizuri juu ya agenda yao na pia angalau wizara itoe tamko juu ya tabia hii inayozidi kusambaa ya utoaji wa maudhui yanayopotosha maadili yetu na kumuweka mtoto kwenye hatari ya ukatili wa kingono.
Nimeambatanisha picha ya mzee huyo pamoja na akaunti ya Tiktok kwa ajili ya kufanyiwa mapitio na rejea.
Ahsanteni wana jamvi.