Waziri Chami: Tusiombeane vifo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri Chami: Tusiombeane vifo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Feb 17, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Feb 17, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,600
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Cyril Chami


  Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Cyril Chami, ameibuka na kusema suala la kifo ama uzima anayelijua ni Mwenyezi Mungu huku akisema afya yake ni nzuri na hana ugonjwa wowote unaomsumbua kama baadhi ya watu wanavyosema.

  Dk. Chami ni miongoni mwa mawaziri watatu wa serikali ya Rais Jakaya Kikwete, ambao wanatajwa kuwa afya zao sio nzuri na wanahitaji kupumzishwa kazi.

  Alisema afya yake ipo vizuri na kuwataka Watanzania wasiombeane vifo kama inavyofanyika sasa kwa kuwa suala hilo anayelijua ni Mwenyezi Mungu pekee.

  Aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam kwa nyakati tofauti alipofanya ziara kwenye kiwanda cha Nondo kilichpo Mikocheni na kile cha kutengeneza Saruji cha Twiga kilichopo Wazo Hill.

  “Tangu nimetoka kutibiwa nchini India sijawahi kulala nyumbani, sijawahi kwenda katika hospitali yoyote, sijawahi kumeza dawa na nafanya kazi mpaka Jumapili,” alisema Waziri Chami, ambaye kwa miezi kadhaa mwaka jana alilazwa nchini India, ingawa hadi sasa hakuna taarifa rasmi iliyotolewa kuhusiana na ugonjwa uliokuwa ukimsumbua.

  Huku akionyesha tumbo lake na mwili wake kwa ujumla, aliwaambia waandishi wa habari kwamba yeye ni mzima kama walivyo watu wegine na wale wanaosema yeye anaumwa wanasema uongo kwa kuwa wao sio madaktari na hawajampima.

  Dk. Chami alihoji kwamba wanaosema yeye ni mgonjwa wanatumia kigezo gani kwa kuwa kama ni afya yupo kama walivyo watu wengine.

  “Wewe ni nani mpaka useme mimi naumwa wakati hata wafanyakazi wenzangu pale wizarani wanajua ninavyofanya kazi bila kupumzika,” alisema Dk. Chami.

  “Hapa nimekuja kiwandani nani kanisaidia kupanda hizi ngazi na mmeona nimetembea mwenyewe bila kusaidiwa hata kuwapita nyinyi waandishi wa habari,” alisema Dk. Chama huku akicheka.

  Aliwataka wapiga kura wake katika Jimbo la Moshi Vijijini mkoani Kilimanjaro kuondoa hofu kutokana na maneno ya upotoshaji ya watu wanaosema kwamba yeye ni mgonjwa.

  Hata hivyo, alikiri kwamba alikuwa anaumwa, lakini baada ya kutibiwa nchini India sasa amepona na anaendelea na kazi zake kawaida.

  Alifafanua kuwa ugonjwa wake ni suala binafsi, lakini amelazimika kutoa kauli kutokana na baadhi ya watu kuendelea kuupotosha umma.

  Dk. Chami alitoa mfano kwamba katika Mkutano wa Sita wa Bunge uliomalizika wiki iliyopita, aliweza kusimama na kujibu maswali yote aliyoulizwa na wabunge kuhusiana na mambo mbalimbali yanayohusu wizara yake bila ya kusaidiwa na mtu.

  Mawaziri wengine wanaosumbuliwa na maradhi ni Waziri wa Maji, Profesa Mark Mwandosya, aliyeanza kuugua mwaka jana. Profesa Mwandosya alifanyiwa upasuaji na kulazwa kwa miezi kadhaa nchini India.

  Mwingine ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, ambaye alipata ugonjwa wa ngozi na kulazwa nchini India.

  Baada ya matibabu hayo wote walirejea nchini na kusema kuwa afya zao ni njema. Hata hivyo, Profesa Mwandosya kwa sasa yupo India kwa ajili ya madaktari kuangalia maendeleo ya afya yake.

  Baadhi ya vyombo vya habari vimeripoti kuwa Dk. Mwakyembe anarejea India kwa ajili ya kuchunguzwa maendeleo ya afya yake.

  Wito wa kutaka mawaziri hao wapumzishwe unatokana na hoja ambayo imejengwa kuwa mawaziri wengi kwa sasa wameshindwa kutekeleza wajibu wao, wengine wakidaiwa kuwa ni wagonjwa huku wengine wakielekeza mawazo yao kwenye mbio za urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

  Baadhi ya watu, kikiwamo Chama cha Wananchi (CUF) wametaka kuvunjwa kwa baraza la mawaziri na kuundwa upya kwa kuteua watu wanaoweza kutekeleza majukumu yao.  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #2
  Feb 17, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kila anaeumwa lazima afe? Waandishi wawe makini na namna wanavyoripoti habari zao za kuunga-unga!
   
 3. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #3
  Feb 17, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Kama habari zisemwazo kuwa baraza la mawaziri litaundwa upya ili tupate mawaziri wachapa kazi ni lazima mamlaka husika isione aibu kuwapumzisha mawaziri ambao inajulikana kutumia muda wao mwingi katika kampeni zao za kutaka urais[ Sitta ,Membe etc] na pia mawaziri ambao afya zao zina mgogoro ni vyema wakapumzishwa ili watumie muda wao kuimalisha afya zao huku wakiwahudumia wapiga kura wao, kundi hili ndio wakina Sophia Simba, Celina kombani, Chami[ ingawa hakubali kuwa hajaimalika] chikawe, Mwakyembe na Mwandosya [ bahati mbaya sana huyu kuugua kwani ni mchapa kazi]. Pia wako mawaziri wenye kashfa na sio watendaji wazuri ; Ngeleja, Malima,Maige, Kawambwa,Lukuvi, Wassira[ kulala bungeni], Nkya,Ponda. Hawa waliotajwa hawawezi kuwa mawaziri katika serikali yeyote makini!!
   
Loading...