Waziri Bashe: Kilimo ni biashara kama biashara zingine, serikali haitafunga mipaka

The Sunk Cost Fallacy 2

JF-Expert Member
Nov 8, 2022
7,382
8,437
Habari wadau wa Jukwaa.

Kutoka Mbeya, Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema Serikali itaendelea na juhudi za kuwaunga mkono Wakulima ili wajikwamue kwa kuwapa Mbolea ya ruzuku na kuwaruhusu kuuza Mazao Yao popote kwenye soko..

Bashe amesisitiza msimamo wa Serikali kwamba Haina mpango wa Kufunga Mipaka kwa sababu Kilimo Ni Biashara Kama zilivyo biashara zingine hivyo wakulima waondoe Shaka na wachape kazi..

My Take.
Hongera Sana Waziri Bashe na Serikali kwa Ujumla kwa kuchukua msimamo ambao utainua kilimo chetu.

Anaeona bidhaa za vyakula zimepanda Bei achukue jembe akalime.👇
 
Bashe ni akili kubwa, na mvua hizi zinanyesha watu wapo mjini wamejaza gesti, mkulima yupo shamba na tope, wakati wa kuvuna eti serikali ifunge mipaka ili wa mjini anunue kwa bei rahisi.

Halafu wanakuambia "JPM angekuwepo angefunga mipaka, wanyonge tusiumie"
 
Bashe anajifanya ana uchungu kumbe Mhuni tu, yaani hadi Mradi wa chakula(kuendesha restaurant)ya Kiwanda cha Mbolea kinachojengwa Nala,Dodoma(ITRACOM)kalazimisha Mke wake apewe na ndie anayeendeshab ni uroho tu,biashara kama hizo za kupika ubwabwa si ni vizuri kuwaachia Wananchi wa kawaida waendeshe khaaa!!!roho mbaya tu kukaba kila kona
 
Bashe anajifanya ana uchungu kumbe Mhuni tu, yaani hadi Mradi wa chakula(kuendesha restaurant)ya Kiwanda cha Mbolea kinachojengwa Nala,Dodoma(ITRACOM)kalazimisha Mke wake apewe na ndie anayeendesha,ni uroho tu,biashara kama hizo za kupika ubwabwa si ni vizuri kuwaachia Wananchi wa kawaida waendeshe khaaa!!!roho mbaya tu kukaba kila kona
So long as it yields Hakuna shida,wewe ukitaka apewe Nani?
 
Vizuri kabisa.
Kufunga mipaka ni kuharibu uchumi na biashara tu. Hakuna kanunini zozote za uchumi au biashara nyuma yake.
True 👇
 
Kwa sasa Namuunga mkono Bashe napo niliamini katika kufunga mipaka baada ya kuweka muhogo wangu store tani 30 nilionunua kilo moja 250 kaliua na nimewauzia wanyarwanda kwa 950 kwa kilo moja, Naunga hoja mipaka isifungwe , jamani mwezi wa saba nilinunua 250 nikautreat mwezi wa 11 nimeuza 950 , Bashe akili kubwa
 
Kwa sasa Namuunga mkono Bashe napo niliamini katika kufunga mipaka baada ya kuweka muhogo wangu store tani 30 nilionunua kilo moja 250 kaliua na nimewauzia wanyarwanda kwa 950 kwa kilo moja, Naunga hoja mipaka isifungwe , jamani mwezi wa saba nilinunua 250 nikautreat mwezi wa 11 nimeuza 950 , Bashe akili kubwa
Hiyo 250 ulimpa mkulima siyo?

Sas yeye hiyo 950 ameifaidi?
 
Back
Top Bottom