Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,498
Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, ameitaka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji kwa wakati na kuondoa urasimu usio wa lazima unaosababisha ucheleweshaji wa huduma.
Akizungumza siku ya Jumanne Machi 18, 2025 wakati wa ziara yake katika Mradi wa Maji wa Bangulo uliopo mtaa wa Bangulo Hali ya Hewa katika kata ya Pugu Station wilayani Ilala mkoani Dar es Salaam, Waziri Aweso amewataka wahudumu wa dawati la huduma kwa wateja wa DAWASA kutoka maofisini na kuwafuata wananchi moja kwa moja ili kupunguza mianya ya walaghai na vishoka wanaotumia mwanya wa ucheleweshaji kuwaibia wananchi.
"Maelekezo yangu kwa dawati hili la huduma kwa wateja mtoke ofisini mwende kwa wananchi, mkawafuate wananchi, msipowafuata wananchi wanatokea vishoka (walaghai na wadanganyifu). Mwananchi anatakiwa aunganishiwe maji badala ya kulipa fedha ndogo anaongezewa fedha nyingine, hivyo kujenga urasimu usiokuwa wa lazima," amesema Waziri Aweso.
Aidha, amewaelekeza DAWASA kuhakikisha kuwa kila mteja anayewasilisha maombi ya kuunganishiwa maji hapaswi kusubiri zaidi ya siku saba kabla ya huduma hiyo kutolewa.
"Niwaombe wateja na nyie mliounganishiwa maji, umeunganishiwa maji na umeomba kuunganishiwa maji isizidi siku 7 lazima uwe umeunganishiwa maji, na hakuna kutoa chochote cha ziada kwamba mpaka upite mlango mwingine ndiyo uunganishiwe maji, wewe toa taarifa," amesisitiza.
Katika hatua nyingine, Waziri Aweso ametoa maagizo kwa DAWASA kubuni utaratibu wa kuwaunganishia maji wananchi ambao hawana uwezo wa kulipa gharama za mara moja, kwa kuwaletea mpango wa malipo ya mkopo kupitia bili zao. Amesisitiza kuwa viwanda na wananchi wanahitaji maji kwa maendeleo yao, hivyo ni muhimu kuweka utaratibu mzuri wa malipo.
"DAWASA tengenezeni utaratibu mzuri, wadau wapo wa viwanda, mtu ukimuunganishia maji maana yake atalipa, wekeni utaratibu mzuri, mkateni katika bili yake kwamba utalipa muda fulani, utalipa muda fulani ili anufaike na matunda ya Rais Samia Suluhu Hassan," amesema.