Waziri atoa rai kwa wanaoishi karibu na mbuga na hifadhi washauriwa wasilime maboga na matikiti kuepuka tembo

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,016
9,885
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja amesema wananchi wanatakiwa kulima mazao ambayo hayatawavutia tembo na wanyama wengine kufanya uharibifu. Tembo huvutiwa na maboga na matikiti.

Ili kuepuka changamoto ya wanyamapori kuvamia mashamba na vijiji, vilivyo karibu na hifadhi za wanyamapori waziri Masanja ametoa rai wananchi walime mazao kama pilipili na pia kuwa na miradi ya ufugaji nyuki.

Njia nyingine ni kutumia Oil chafu iliyochanganywa na Pilipili na majivu pia kutoa taarifa haraka wanakuwa wamevamiwa na wanyamapori.
 
Waliovamiwa juzi namtumbo kumbe kwa ajili ya maboga, kwa songea uwaambie wasilime hayo makitu sijui kama watakuelewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…