Waziri athibitisha kufilisika kwa serikali ya JK | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri athibitisha kufilisika kwa serikali ya JK

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mutabora, May 27, 2011.

 1. M

  Mutabora Member

  #1
  May 27, 2011
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Wiki chache baada ya Zitto Kabwe(mb)kudai serikali ya JK imefirisika,Naibu Waziri wa mambo ya ndani Khamis Kagasheki amesema serikali ililazimika kukomba mafungu ya fedha katika halmashauri za wilaya,jiji na manispaa ili kudunduliza na kupata fedha za kuwalipa makandarasi wa barabara nchini waliokuwa wamegoma wakishinikiza kulipwa.

  Alikuwa akichangia katika kikao cha bodi ya barabara cha mkoa wa Kagera jana.Waziri wa fedha Mustapha Mkulo alikanusha vikali kauli ya Zitto.
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  May 27, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,527
  Likes Received: 19,947
  Trophy Points: 280
  JK mwenyewe si ndio kawaambia wajibu hoja kwenye semina elekezi. inabid wamwage ukweli kwani uongo ni dhambi
   
 3. F

  Froida JF-Expert Member

  #3
  May 27, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,903
  Likes Received: 1,330
  Trophy Points: 280
  Zitto alikuwa anasema anachokifahamu ni ubishi tuu wa serikali ya CCM,kuficha ficha mambo wakidhani wabunge wetu hawawezi kuibua ukweli,aibu kwa serikali kuwa serikali ya vibakuli,omba omba akina Matonya hao
   
 4. Pukudu

  Pukudu JF-Expert Member

  #4
  May 27, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 2,971
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  hivi jamani watumishi wenzangu wa serikalini mmecheka? sisi bado hadi leo ATM za NMB zimenuna je na hili linahusika na kufilisika kwa serikali na kushindwa kulipa wafanyikazi wake? Coz nilimsikia mzee wa kulialia akisema tar 23 mambo yawe safiau kuna tatizo la kiufundi

  Pukudu @Ilkiding'a, Arusha
   
 5. Ndumbayeye

  Ndumbayeye JF-Expert Member

  #5
  May 27, 2011
  Joined: Jan 31, 2009
  Messages: 4,815
  Likes Received: 1,060
  Trophy Points: 280
  mkuu upo tamisemi(kwenye neema) au central gvt?
   
 6. Mtumiabusara

  Mtumiabusara JF-Expert Member

  #6
  May 27, 2011
  Joined: Nov 18, 2009
  Messages: 473
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Ngoja tusubiri, kwa vyovyote vile hali itakuwa si nzuri serikalini
   
 7. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #7
  May 27, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,014
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135


  We acha tu, kuna haja ya kusaka malisho ya kijani.
   
 8. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #8
  May 27, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Nini maana ya kufilisika. Ni nani anaye rate serikali kwamba imefilisika? Halafu, serikali inaweza kufilisika? Kwanini treasury bills au government securities ziitwe risk free rates instruments?
   
 9. M

  Mr.Mak JF-Expert Member

  #9
  May 27, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 2,635
  Likes Received: 496
  Trophy Points: 180
  ivi kweli hili ni la kushabikia? serikali ikifulia ni yetu wote sisi ndio tutakao athirika,kwahiyo sidhani kama ni sahihi kulishabikia kama vile ni la wanamagamba tu. jamani hapa tutakuwa tunakosea ndugu zangu.tukigombea fito wakati tunajenga nyumba moja mwishowake tutaibomoa hata nyumba yenyewe.
   
 10. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #10
  May 27, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Serikali haiwezi kufilisika, mimi leo nimepeleka kodi za mishahara TRA na wengine nao watafanya hivyo. Labda useme Serikali inatekeleza mambo mengi kwa wakati mmoja hata kuzidi kiasi cha mapato yanayokusanywa.
   
 11. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #11
  May 27, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Tatizo si kufanya mambo mengi, bali kutokuwa na udhibiti katika matumizi na pia rushwa na ufisadi.
   
 12. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #12
  May 27, 2011
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,924
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280
  Mkapa: Niliangalia uchumi kuliko michezo
  Sunday, 08 May 2011 10:01
  Vicky Kimaro
  RAIS mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin William Mkapa amesema katika kipindi chake cha urais, aliweka michezo kama ziada kwani alikuwa akiangalia zaidi kutengeneza uchumi wa Tanzania na hakuwahi kwenda kwenye mchezo hata mmoja.

  Mkapa aliyasema hayo baada ya kutunukiwa Tuzo ya Heshima ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo nchini Taswa, iliyofanyika kwenye Hoteli ya MovenPick Dar es Salaam.

  "Nilipopata mwaliko nilishtuka kidogo, kwa kuwa katika kipindi changu, sikuwahi kuhudhuria mchezo hata mmoja...

  "Mnakumbuka enzi zile za 'Ukapa' michezo, niliweka sehemu ya chini kabisa, hii ni kwa sababu awamu ya kwanza ya uongozi wangu ilikuwa ni lazima tutumie tulichonacho, tulikuwa na madeni, na hapo hapo tukawa tunalazimika kuomba kusamehewa madeni yetu.

  "Nguvu nyingi zilitumika kukusanya madeni yetu ya ndani na tutumie kwa fedha za kwetu na tulianza kulipa baadhi ya madeni...tulipata msamaha wa madeni nikasema ingawa sipendi michezo niliamua kuwaachia Watanzania wafurahi, nikajenga uwanja.

  "Namshukuru Juma Kapuya (aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo), alinihimiza sana...tuwe na uwanja wetu na kwa kutumia fedha za msamaha wa madeni, tukajenga uwanja wetu kwa kushirikiana na serikali ya China...

  "Na ndiyo maana ujenzi ulipokamilika, alikuja Rais wao, Hu Jintao akaufungua. Uwanja ule ni jasho la kodi zenu na kodi za watu wa China hivyo muutunze.

  "Nitakuwa mchoyo wa fadhila kama sitamshukuru rais wa sasa, Jakaya Kikwete ambaye ndiye aliyeniwakilisha kwenye mazungumzo na serikali ya China hadi kuwezesha uwanja ule kujengwa, naomba Watanzania muutunze uwanja huo kwani ni moja ya hazina yetu muhimu ya kujivunia, umetukutanisha na watu mbalimbali, timu mbali mbali kubwa dunia, na pia iwe chachu ya mshikamano kwa Watanzania," alisema Mkapa na kushangiliwa na wanahabari.

  Uwanja huo wa kisasa, ulifunguliwa rasmi Novemba 19 mwaka juzi na uligharimi dola za Marekani dola57mil ukiwa na una uwezo wa kubeba watazamaji wasiopungua 65,000 walioketi ulijengwa kuanzia mapema mwa miaka 2003 na Kampuni ya China, Beijing Construction.

  Katika hafla hiyo, Mkapa alitunukiwa tuzo hiyo kutokana na kufanikisha ujenzi wa uwanja huo wakati wa uongozi wake, na kutokana na uwanja huo wenye hadhi ya kimataifa.

  Timu mbalimbali zikiwemo na wachezaji wa kimataifa zilikuja nchini kucheza na timu ya taifa ikiwemo Brazil, Ivory Coast, New Zealand, Cameroon, Ghana, Cape Verde, Morocco na Tunisia.

  Mechi ya kwanza kuchezwa kwenye uwanja huo ilikuwa Septemba Mosi kati ya Tanzania na Uganda na Stars iliibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Abdi Kassim akiwa mchezaji wa kwanza kutikisa nyavu za uwanja huo.
   
 13. Jeremiah

  Jeremiah JF-Expert Member

  #13
  May 27, 2011
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 642
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Mficha ficha ugonjwa hufichuliwa na kilio. Huyo mkulo alisema eti kusema serikali haina hela si uzalendo. Kwa hiyo alitaka wafadhili waendelee kuwaamini wakati hawaaminiki. Alitaka watoe pesa nyingine wagawane kimya kimya . Chama cha msimu kinawavua nguo sasa. tatizo mlilonalo hamtaki kusikia ukweli mlishazoea kusifiwa . Shauli yenu ngoja tuone kwenye budget mtasemajekama au mtaendelea kuwazomea CDM.
   
 14. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #14
  May 27, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kuna vitu havitofautishiki. Hivi michezo si sehem ua uchumi? Nchi kama Uingereza, Brasil etc. Michezo imewasaidiaje? Employment na consumption inakuwaje kama hakuna maeneo ambayo watu wataweza kutumia income zao? Kujenga afya je kuondoa ubaguzi nk.
   
 15. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #15
  May 27, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,654
  Likes Received: 1,439
  Trophy Points: 280
  nchi ya kusadikika..
   
Loading...