Waziri Angela Kairuki akabidhi vifaa vya michezo jimbo la Same

comrade igwe

JF-Expert Member
Jan 12, 2015
7,295
3,950
Waziri wa nchi ofisi ya Rais utumishi na utawala bora Mh Angellah j.Kairuki ameanzisha mashindano yatayojulikana kama Angellah Kairuki Cup yanayotegemewa kuanzia tarehe 7.1.2017 katika wilaya ya Same, akibidhi vifaa hivyo jezi na mipira kadhaa waziri kairuki amesema wanamichezo wadumishe nidhamu katika kuendeleza michezo nchini

Chanzo: ITV Sauda Shimbo Kilimanjaro
 
Huyu mama mwehu anafikri michezo ndoo ajira ? Amesahau matamko yake mwache achanganyikiwe
 
Hongera Kairuki, wakupingao ni gubu na wivu.... Ukisema watasema unawaonea na ukikaa kimya watadai unawaogopa
 
Waziri wa nchi ofisi ya Rais utumishi na utawala bora Mh Angellah j.Kairuki ameanzisha mashindano yatayojulikana kama Angellah Kairuki Cup yanayotegemewa kuanzia tarehe 7.1.2017 katika wilaya ya Same, akibidhi vifaa hivyo jezi na mipira kadhaa waziri kairuki amesema wanamichezo wadumishe nidhamu katika kuendeleza michezo nchini

Chanzo: ITV Sauda Shimbo Kilimanjaro
Same kuchele 2020
 
Hayo ni maandalizi ya 2020 Mathayo kaa mkao wa shughuli.Siasa ni nyoko dah
 
watu wanataka ajira,kuboreshewa mishahara,pensheni kwa wakati nk mmesababisha watumishi washindwe kusherehekea mwaka mpya unacawa mipira...what z it with u viongoz? Wawezeshe vijana wasame na tangawizi,kilimo cha mirungi,vitunguu nk. Mipira haitobadili vipato vya wananchi chyaa hali nimbaya atii!! Natamani wachimbeshimo wafukie ivovitu michezo bila kula ndonini??
 
Sasa atafanyaje hivyo mbele mbunge wenzake wa ccm? Mathayo upo?? Nasikia ulipata ushindi mwembaba sanaa kaa chonjo
 
Kwan huyu mama ni mbunge wa jimbo gan?
Huyu Mama ni Mbunge wa Viti Maalumu kupitia Umoja wa Vyama vya Wafanyakazi(Yaani anawakilisha wanawake wafanyakazi Bungeni)Lkn ndio huyohuyo kapewa Wizara ya Wafanyakazi anaooaswa kuwatetea huko Bungeni.Maajabu haya!!!

Huyu kwao ni Chome-Same kule Upareni juu milimani.Unapitia hii njia ya Mkomazi National Park hadi huko mbele.Mama kaanza kujiandaa kwa ajili ya Jimbo la Same Magharibu 2020 ili kumuondoa Mathayo David Mathayo ambaye ushindi wake 2015 dhidi ya MBANJO wa CHADEMA ulikuwa ni wa "FFU".

Mama kaanzisha Mashindano ya Mpira ya Wilaya Nzima ya Same...Yanaweza kuchukua hata mwaka mzima kwa jinsi team zilizvyo nyingi.Shughuli zote zilifanyika kwenye ukumbi wa kanisa katoliki pale jimbo la Same.Na ndio huyu Mama hufika hapo mara nyingi...Na alitoa mchango kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya Mapadre pale Jimboni Same.

Mathayo akae macho;lkn nitashangaa sana hawa watu wa Same....Toka Uhuru wao maji ya bomba ni anasa,dumu la maji linauzwa 500 hadi 1000 wakati wa ukame,na tena maji ya chumvi halafu bado wameikazania tu hiyo "Iyena iyena".
 
Back
Top Bottom