Waziri akuta mifuko ya plastiki ikitumika kariakoo

Nanunua Mifuko ya RAMBO mwenye nayo anifate PM..ile mikubwa kubwa iliyokua inauzwa sh 200 kwenda mpk 500 sio vile vya sh.100.
 
c2c7b3495c4818465a47e818cd8d9cb3

Dar es Salaam. Wafanyabiashara wa soko dogo la Kariakoo, Dar es Salaam nchini Tanzania wanaojihusisha usambazaji na uuzaji wa mifuko ya plastiki laini yenye rangi nyeupe inayotumika kama kifungashio wamepewa siku 14 kuiondoa sokoni mifuko hiyo.
Kauli hiyo imetolewa jana Alhamisi Agosti 15, 2019 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) George Simbachawene baada ya kufanya ziara katika soko hilo na kubaini uwepo wa mifuko hiyo kinyume cha utaratibu.
Katika ziara hiyo, Simbachawene aliambatana na maofisa wa Baraza la Taifa la Usimamizi na Uhifadhi wa Mazingira (NEMC), alijionea namna mifuko hiyo iliyopigwa marufuku ikitumika kama kifungashio cha bidhaa za nyanya, karoti, vitunguu ambavyo vinaweza vikabebwa kwenye mifuko mbadala.
Juni Mosi 2019, katazo la marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki lilianza kutumika rasmi, hata hivyo bado kumekuwa na changamoto kwa baadhi ya wamiliki wa viwanda vya plastiki kuendelea kutengeneza mifuko hiyo kinyume cha utaratibu.
Amewaambia wafanyabiashara wanaotumia elimu imeshawafikia lakini kitendo cha wao kuendelea kuiuza mifuko hiyo, kinawapa morali wazalishaji kuendelea na shughuli hiyo kinyume cha sheria.
“Kwani mmelazimishwa kununua mifuko hii kiwandani, kwa nini msichukue mifuko mbadala na kuiuza? Kuna vikapu, mifuko ya karatasi kwa nini msichukue hiyo,” anahoji Simbachawene
“Watumiaji elimu imeshawafikia lakini nyie bado mnaendelea kuiuza. Kitendo cha mifuko hii kuendelea kuwepo sokoni kinawavunja moyo watengenezaji na wazalishaji wa mifuko mbadala.”
Simbachawene alisema taarifa alizonazo kuna viwanda vinne vya plastiki vinajishughulisha na uzalishaji wa mifuko hiyo laini iliyopigwa marufuku na Serikali huku akiwaagiza NENC kuvifuatilia kuanzia kesho.
Mjumbe wa bodi ya wafanyabiashara wadogo wa soko hilo, Rajabu Ally anadai wao hawana kosa bali wenye matatizo ni wenye viwanda vinavyozalisha mifuko hiyo.
MM NINA WASIWASI KUNA KITU HAKIJAPATIWA JAWABU. JE ANAYENUNUA KITU CHENYE MAJIMAJI KAMA SAMAKI NA KUHITAJIKA KUSAFIRISHA KWA UMBALI MREFU AU KWA MUDA MREFU ATUMIE KITU GANI.NILIDHANI VITAZALISHWA AMBAVYO VINAZUIA MAJI KUCHURUZIKA LAKINI WAPI. HATUWEZI KUWA TUNATEMBEA NA KAPU NA NDOO ILI TUKIHITAJI NA SAMAKI HATA NYAMA AU KITU KINGINE CHOCHOTE CHA MAJIMAJI UWEKE HUMO. SIDHANI NDIO MAANA YA KUKATAZA HIZO PLASTIKI. MKATE UNAFUNGWA NA NINI SIO PLASTIKI. HUKO ULAYA WANATULETEA VITU VIMEFUNGWA NDANI YA KARATASI ZA PLASTIKI. MNAZIRUHUSU MFANO MASHATI NA SURUALI KWA SABABU HIYO PLASTIKI YA MKATE INA LEBO NA IMERUHUSIWA . SASA WATU WANATUMIA HIZO PLASTIKI MNAZORUHUSU KUFANYA VIFUNGASHIO. NIMEKUTA WATU WANAENDA SOKONI NA MFUKO WA MKATE AWEKE NYAMA. NYAMA INAFUNGWA NA NINI. MAGAZETI YALIYOANDIKWA KIHINDI NDIO MTASEMA SAWA. NADHANI BAD O JIBU LA VIFUNGASHIO MBADALA HALIJAANGALIWA VIZURI. HAO MLIOWAPA KUZALISHA WANAZALISHI VIFUNGASHIO VYENYE MATOBO AU VINALOWA NA KUHARIBIKA. PIA PIGA MARUFUKU KUFUNGIWA VYAKAULA KAMA NYAMA KWENYE GAZETI
 
Hili katazo bado linaukakasi kwasababu bado kuna mifuko laini myeupe inatumika kama kifungashio sehemu nyingi sana. Nenda kwa wauza matikiti na matunda mbali mbali au masoko ya jioni utakuta mifuko kibao ya plastic inatumika walichofanya ni kubadilisha rangi kutoka myeusi au blue kwenda colourless. Mimi nashauri wapige mafuku mifuko yote ya plastic ya vibebeo.
Tatizo hao wazalishaji wa hiyo mifuko ya kaki wanauza gharama sana bei ya mfuko inaanzia sh 100 badala ya sh 50 inafanya watu waendelee kutumia mifuko ya plastic hiyo meupe
mimi pia nilichukua mzigo wa kutosha hapa wenye viwanda vidogo vya mikate wataathirika na hili pia biashara ndogo ndogo kama wauza bisi
 
Back
Top Bottom