Waziri aagiza kampuni zenye hati ya umiliki wa ardhi uwanja wa ndege Dar kunyang’anywa

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye ameuagiza uongozi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) kufuatilia na kufuta hati za umiliki wa ardhi za kampuni za Puma Energy na Tanzan air zilizopo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).

Akizungumza baada ya kutembelea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) Nditiye amasema haiwezekani kampuni binafsi kuwa na hati za kumiliki ardhi katikati ya uwanja wa ndege wa Serikali.

"Hati hizi zinapaswa kufutwa haraka sana na hizi kampuni zinapaswa kupangishwa katika uwanja huo, kuna madhara makubwa mtu binafsi kuwa na hati katikati ya uwanja, anaweza kuchukua mkopo katika benki na akashindwa kulipa je itakuwaje?" amehoji.

Amesema TAA inapaswa kuhakikisha inalifikisha suala hilo Wizara ya Ardhi na taasisi nyingine za Serikali ili hati hizo zifutwe.

Amesema haiwezekani Rais John Magufuli anautangaza uwanja wa JNIA kuwa ni mali ya Serikali kumbe katikati kuna watu binafsi.
 
kwani uwanja ,unatumia Ndege za serikali pekee.!?
 
Ardhi ni mali ya serikali na msimamizi mkuu wa ardhi ni Rais. Watu wengine wote ni wapangaji tu kwenye ardhi ya TZ. Hivyo hati inaweza kuwa revolked wakati wowote na serikali inakulipa mali zako kama umeshakiendeleza kiwanja hicho
Hilo wamelijua leo?
 
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye ameuagiza uongozi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) kufuatilia na kufuta hati za umiliki wa ardhi za kampuni za Puma Energy na Tanzan air zilizopo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).

Akizungumza baada ya kutembelea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) Nditiye amasema haiwezekani kampuni binafsi kuwa na hati za kumiliki ardhi katikati ya uwanja wa ndege wa Serikali.

"Hati hizi zinapaswa kufutwa haraka sana na hizi kampuni zinapaswa kupangishwa katika uwanja huo, kuna madhara makubwa mtu binafsi kuwa na hati katikati ya uwanja, anaweza kuchukua mkopo katika benki na akashindwa kulipa je itakuwaje?" amehoji.

Amesema TAA inapaswa kuhakikisha inalifikisha suala hilo Wizara ya Ardhi na taasisi nyingine za Serikali ili hati hizo zifutwe.

Amesema haiwezekani Rais John Magufuli anautangaza uwanja wa JNIA kuwa ni mali ya Serikali kumbe katikati kuna watu binafsi.
Kwani hati shirikishi zimefutwa tena? Mbona tunauziwa apartment nhc na bado gorofa linaendelea kuwa mali ya nhc? Puma akikopa bank anaweka dhamana uwanja mzima au eneo lake pekee?
 
Kwani Puma serikali si inayo hisa au miki sielewi
Serikali inahisa kwenye kampuni lakini kampuni imemilikishwa sehemu ya uwanja kwenye eneo la JNIA na hao Tanzan Air wako ndani kabisa ya uwanja nadhani kuna watu walipiga baada ya kuwa hawa jamaa wamepangishwa kwa muda mrefu
 
Aisee ccm imetufikisha pabaya sana, yaani watu binafsi wana hati miliki katikati ya uwanja wetu wa ndege, haingii akilini kabisa
 
Puma waende mhakamani hii serikali invunja miktaba na haifuati sheria!
Mkuuu jitahidi japo umiliki ardhi japo 10×10 basi ili huu ushamba wa ukuishe maaana unapaniki sana, halafu tambua kuwa Ugumu wa maisha ulionao kisababishi sio Serikali bali kichwa chako maaana post zako zooote unalalamika tuuuuuu. UZA HIYO TECNO ULIYOHONGWA NA BASHA WAKO uanze kuuuza mkaaa wa Kupima utatoboa tuu na hizi Stresss zitaondoka tuuu.
 
Shauri na waziri wako akafyeke pori ajenge kiwanja kipya aache kupora mali za wawekezaji mliowapigia magoti mlipokua na njaa wamefanya uwekezaji mkubwa watawashtaki kimataifa mporwe bombadia
 
Akizungumza baada ya kutembelea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) Nditiye amasema haiwezekani kampuni binafsi kuwa na hati za kumiliki ardhi katikati ya uwanja wa ndege wa Serikali

Kwanini habari za JNIA anakwenda kuzisemea KIA!?

Anyway, wamejifunza kutoka kwa Chavda miaka ya 1990s
 
Kwani hati shirikishi zimefutwa tena? Mbona tunauziwa apartment nhc na bado gorofa linaendelea kuwa mali ya nhc? Puma akikopa bank anaweka dhamana uwanja mzima au eneo lake pekee?
Sema waziri anashindwa kuelewa hata eneo lililopangishwa unaweza kulikopea.
 
Back
Top Bottom