Wazir: Marekani imeridhika Tanzania inavyotumia misaada

Kasheshe

JF-Expert Member
Jun 29, 2007
4,694
787
SOURE: Habari Leo
Shadrack Sagati
Daily News; Wednesday,September 03, 2008 @00:02

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amesema majasusi wa Marekani wamechunguza misaada inayotolewa na taifa lao na kugundua kuwa Tanzania inatumia vizuri misaada hiyo kwa ajili ya maendeleo.

Alisema kutokana na hali hiyo, ndiyo maana Rais George W. Bush katika kipindi cha utawala wake amekuwa anazidisha misaada kwa Tanzania kuzidi kuendeleza Watanzania katika sekta za elimu, kilimo, afya na utalii.

“Wamechunguza kwa undani zaidi kwa kutumia majasusi wao, wakagundua kuwa fedha zao wanazotoa kwa Tanzania zinatumika vizuri kwa maendeleo ya nchi…na hii ni sifa nzuri kwa Rais Bush,” alisema Membe jana alipozungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam.

Membe aliyekuwa anatoa taarifa ya ziara ya Rais Jakaya Kikwete nchini Marekani iliyomalizika Ijumaa iliyopita, alisema Rais Kikwete ameahidi kuendeleza uhusiano wa karibu na taifa hilo hata Rais Bush atakapoondoka madarakani. Ataondoka Novemba mwaka huu.

Akizungumzia misaada zaidi itakayotolewa na Marekani, Membe alisema taifa hilo limekubali kutoa walimu na kuanzisha mpango wa kufundisha kwa kutumia mtandao wa mawasiliano (Tekinohama) hali itakayosaidia kupunguza tatizo la walimu nchini. Alisema walimu 350 watatoka Marekani kuja kufundisha nchini masomo ya Sayansi, Hisabati na Lugha katika shule za sekondari.

Pia alisema kupitia mpango wa Tekinohama shule 200 za mfano kutoka wilaya za Bagamoyo, Mkuranga, Lindi na Temeke ambazo hazina huduma ya umeme, zimeteuliwa kuendeshea mpango huo na shule hizo zitawekewa umeme wa jua, kompyuta pamoja na televisheni.

Katika mpango huo, mwalimu mmoja atafundisha kutoka katika kituo kimoja na atafundisha wanafunzi wengi ambao nao watakuwa wanaelekezwa na mwalimu wa kawaida na kisha kuwapatia mitihani. Alisema Marekani itakachofanya ni kuwafundisha walimu wa Tanzania ambao nao baadaye watakuwa walimu wa wenzao wa namna ya kuendesha mpango huo wa kufundisha wanafunzi wengi kwa wakati mmoja kwa kutumia tekinohama.

“Tunaamini kuwa mpango huu utasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza tatizo la walimu nchini,” alisema Membe ambaye alisisitiza kuwa ni mpango wenye manufaa makubwa katika sekta ya elimu. Alisema Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi ndiye atakayetangaza lini mpango huo utaanza.

Pia alisema Chuo Kikuu cha South Caroline kitachapisha vitabu milioni 1.4 vya kiada na ziada kwa ajili ya kuvisambaza katika shule mbalimbali za sekondari. Vitabu hivyo vya masomo ya Sayansi, Hisabati na Kiingereza vinagharimu dola za Marekani milioni 1.5. Kuhusu malaria, Membe alisema Marekani imetoa dola za Marekani 34 kwa ajili ya kudhibiti ugonjwa huo nchini.

Alisema fedha hizo zitatumika kununulia vyandarua vya dawa, kununua dawa za malaria, kunyunyizia sehemu ambako mbu wanataga mayai na dawa za kuwatibu wajawazito. Pia taifa hilo limetoa dola za Marekani milioni 45 kwa ajili ya kudhibiti maambukizi ya Ukimwi. Membe pia alisema Shirika la Fedha Duniani (IMF) limeridhika na namna ambavyo Tanzania inatumia fedha vizuri zikiwamo fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA).

Kutokana na hatua hizo shirika hilo limeamua kufanyia mkutano wake wa kujadili matatizo ya shirika hilo nchini Machi mwakani. Alisema Marekani imetoa dola za Marekani milioni 20 kwa ajili ya kuanzisha mtajiWaziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amesema majasusi wa Marekani wamechunguza misaada inayotolewa na taifa lao na kugundua kuwa Tanzania inatumia vizuri misaada hiyo kwa ajili ya maendeleo.

Alisema kutokana na hali hiyo, ndiyo maana Rais George W. Bush katika kipindi cha utawala wake amekuwa anazidisha misaada kwa Tanzania kuzidi kuendeleza Watanzania katika sekta za elimu, kilimo, afya na utalii.

“Wamechunguza kwa undani zaidi kwa kutumia majasusi wao, wakagundua kuwa fedha zao wanazotoa kwa Tanzania zinatumika vizuri kwa maendeleo ya nchi…na hii ni sifa nzuri kwa Rais Bush,” alisema Membe jana alipozungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam.

Membe aliyekuwa anatoa taarifa ya ziara ya Rais Jakaya Kikwete nchini Marekani iliyomalizika Ijumaa iliyopita, alisema Rais Kikwete ameahidi kuendeleza uhusiano wa karibu na taifa hilo hata Rais Bush atakapoondoka madarakani. Ataondoka Novemba mwaka huu.

Akizungumzia misaada zaidi itakayotolewa na Marekani, Membe alisema taifa hilo limekubali kutoa walimu na kuanzisha mpango wa kufundisha kwa kutumia mtandao wa mawasiliano (Tekinohama) hali itakayosaidia kupunguza tatizo la walimu nchini. Alisema walimu 350 watatoka Marekani kuja kufundisha nchini masomo ya Sayansi, Hisabati na Lugha katika shule za sekondari.

Pia alisema kupitia mpango wa Tekinohama shule 200 za mfano kutoka wilaya za Bagamoyo, Mkuranga, Lindi na Temeke ambazo hazina huduma ya umeme, zimeteuliwa kuendeshea mpango huo na shule hizo zitawekewa umeme wa jua, kompyuta pamoja na televisheni.

Katika mpango huo, mwalimu mmoja atafundisha kutoka katika kituo kimoja na atafundisha wanafunzi wengi ambao nao watakuwa wanaelekezwa na mwalimu wa kawaida na kisha kuwapatia mitihani. Alisema Marekani itakachofanya ni kuwafundisha walimu wa Tanzania ambao nao baadaye watakuwa walimu wa wenzao wa namna ya kuendesha mpango huo wa kufundisha wanafunzi wengi kwa wakati mmoja kwa kutumia tekinohama.

“Tunaamini kuwa mpango huu utasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza tatizo la walimu nchini,” alisema Membe ambaye alisisitiza kuwa ni mpango wenye manufaa makubwa katika sekta ya elimu. Alisema Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi ndiye atakayetangaza lini mpango huo utaanza.

Pia alisema Chuo Kikuu cha South Caroline kitachapisha vitabu milioni 1.4 vya kiada na ziada kwa ajili ya kuvisambaza katika shule mbalimbali za sekondari. Vitabu hivyo vya masomo ya Sayansi, Hisabati na Kiingereza vinagharimu dola za Marekani milioni 1.5. Kuhusu malaria, Membe alisema Marekani imetoa dola za Marekani 34 kwa ajili ya kudhibiti ugonjwa huo nchini.

Alisema fedha hizo zitatumika kununulia vyandarua vya dawa, kununua dawa za malaria, kunyunyizia sehemu ambako mbu wanataga mayai na dawa za kuwatibu wajawazito. Pia taifa hilo limetoa dola za Marekani milioni 45 kwa ajili ya kudhibiti maambukizi ya Ukimwi. Membe pia alisema Shirika la Fedha Duniani (IMF) limeridhika na namna ambavyo Tanzania inatumia fedha vizuri zikiwamo fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA).

Kutokana na hatua hizo shirika hilo limeamua kufanyia mkutano wake wa kujadili matatizo ya shirika hilo nchini Machi mwakani. Alisema Marekani imetoa dola za Marekani milioni 20 kwa ajili ya kuanzisha mtaji wa Benki ya Wakulima ili wakopeshwe. Alisema benki nyingi kwa sasa haziwakopeshi wakulima, lakini kwa juhudi za Rais Kikwete benki hiyo kwa sasa imepata mtaji wa kuanzia. wa Benki ya Wakulima ili wakopeshwe. Alisema benki nyingi kwa sasa haziwakopeshi wakulima, lakini kwa juhudi za Rais Kikwete benki hiyo kwa sasa imepata mtaji wa kuanzia.
 
Bw Membe;

Sidhani kama wewe ni msemaji wa serikali ya US. Wameshindwa kutoa hata press conference kuzungumzia hili? I can not trust you at all.

Kuna kingine ungependa tusikie?
 
Guys
Am little bit nervous
since independent we are using Europian tax-payers money and yet african leaders ate them without shame.
Dont be proud to receive because you'll have to give in otherway.
Mr. Membe be creative, there comes a day when western will get tired to put their money in (your pocket)....
 
niliposikia stansaus yule mtu wa imf amesifia hatua alizochukua kikwete sikushangaa, kwani aisifiae mvua imemnyea na anayelisifu jua limemwangaza lakini akili kichwani

kuna kitu akina bush wanatafuta hapa nchinikupitia muungwana kama siyo kwa usa interest basi kwa personal interest, nchi kama hii imejaa mali adimu za ardhini usishangae uksikia bush baada ya kustaafu urais yuko nzega kwenye machimbo ya dhahabu.

pengine aki9na membe wanasifiwa kwa,kuwa ni mandondocha wazuri wa marekani
 
Back
Top Bottom