Herbalist Dr MziziMkavu
Platinum Member
- Feb 3, 2009
- 43,091
- 34,899
Ujumbe unaosema wote 33 tuko salama
Wachimba madini wa Chile wamenasa mita 700 chini ya ardhi baada ya mgodi wa dhahabu waliokuwemo kuporomoka, wote wako hai lakini wataendelea kukaa huko hadi mwezi disemba mwaka huu wakati taratibu za kuwaokoa zitakapokamilika. Juhudi zinaendelea kuwaokoa wachimba madini 33 wa nchini Chile ambao wamenasa kwenye shimo lililopo mita 700 chini ya ardhi.
Hata hivyo wachimba madini hao wataendelea kuishi kwenye shimo walilonasa kwa miezi minne ambapo inategemewa taratibu za kuwaokoa zitakuwa zimekamilika.
Wachimba madini hao walikuwa wakichimba dhahabu kwenye mgodi wa San Jose,karibu na mji wa Copiapo, wakati wa jiwe lililokuwa juu yao liliporomoka.
Baada ya siku 17, huku matumaini ya kuwaokoa yakiwa yamefifia, waokoaji walisikia kelele za wachimba madini hao walipotuma kifaa cha uchunguzi kwenye mgodi huo.
Wachimba madini hao waliandika ujumbe kwenye karatasi walioubandika kwenye kifaa hicho ukisema: "Sisi sote 33 tuko salama".
Walituma ujumbe wa pili baadae wakisema kuwa walitumia tingatinga walilokuwa wakilitumia kuchimbia madini kujitengenezea sehemu ya kulala na kuchimba kisima ambacho kimewawezesha kupata maji salama. Wanatumia umeme wa injini ya tingatinga kuwasha taa zinazowawezesha kupata mwanga kwenye shimo hilo lenye giza nene.
Kazi ya kuwaokoa imeanza lakini kutokana na umbali mkubwa waliopo nchini ya ardhi mashimo mawili madogo yamechimbwa ili kuweza kuwapelekea chakula na maji huku shimo kubwa likichimbwa kuweza kuwaokoa mmoja mmoja.
Uchimbaji wa shimo hilo kubwa lenye upana wa sentimeta 66 utatumia miezi minne kuweza kuwafikia wachimba madini hao.
Wachimba madini hao wamenasa chini ya ardhi tangia tarehe tano mwezi huu na kwa muda waliokaa huko hadi leo tayari wameishavunja rekodi ya dunia ya watu walionasa chini ardhi kwa muda mrefu.
Source: NIFAHAMISHE Tanzania news portal .: Habari za Tanzania :.