dudus
JF-Expert Member
- Feb 28, 2011
- 23,213
- 52,829
Wanaukumbi.
Jana kwa macho yangu kupitia BBC nilishuhudia wazee, wake kwa waume, huko Zanzibar wakitia madole gumba na kukabidhiwa posho zao za kujikimu ambao ni utaratibu mpya na utakuwa ukifanyika kila mwezi kama sehemu ya kuwasaidia wazee kujikimu kimaisha.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya BBC, utaratibu huo ni kwa wazee wote wenye umri wa miaka 70 na kuendelea na watakuwa wakipatiwa kiasi cha USD 9 (tisa) kwa ajili hiyo.
Kwa kweli wazee niliowaona walikuwa na nyuso za bashasaha tele mara baada ya kukabidhiwa vitita vyao.
Kwa maoni yangu huu ni mwanzo mzuri katika kuwajali na kuwathamini wazee wetu waliotumia nguvu zao nyingi kulitumikia taifa.
Hopefully, utaratibu huu utaenea hadi bara kwani matatizo ya wazee wetu ni yale yale - vipato duni pasi na msaada.
La ajabu, pamoja na uzito na umuhimu wa tukio hili la kihistoria sijaona chombo chochote cha habari cha ndani hususan magazeti yaliyotoka na habari hii - sijui waandishi wetu habari kwao ni nini hasa.