OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 52,073
- 114,572
Wazee mbalimbali nchini wameeleza kufaishwa na kusikitishwa sana na kauli ya Rais Magufuli kwamba atafanya kazi na vijana kwani wazee wameifikisha nchi pabaya.Wazee wamekasirishwa na kauli hiyo kwani ni ya kibaguzi na haina nia njema.Wanahoji nini nafasi ya Mzee Mkapa na Mzee Kikwete,Mangula,Warioba na hata Mzee Karume katika kauli hiyo.Wazee wanahoji utamaduni wa kuwaalika wazee wa Dar es Salam kama ni kejeli kwao?Wazee wameshauri kuwa ni vyema watu wakapatiwa nafasi kwa uwezo na weledi wao na sio kigezo cha umri.Busara itumike kuepuka kauli zenye dalili za ubaguzi.Hata hivyo wamesisitiza kwamba viongozi wa sasa wafanye kazi kwa bidii na sio kuendelea kulaumu kwani waliomba nafasi wakizijua changamoto hizi