Wazee wa Zanzibar waelezea athari za SMZ kubakia katika Muungano

abdulahsaf

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
858
130
img_2798.jpg

Baadhi ya wazee ambao walishiriki katika kongamano la kutathmini matokeo ya mtihani yaliotangazwa na baraza la elimu Tanzania (NECT) ambalo limewafutia jumla ya wanafunzi 3303 kwa madai ya udanganyifu wengi wao wakielezwa ni kutoka Zanzibar

Na Ally Saleh

Wiki iliyopita ilikuwa ni kubwa kwa habari za matokeo ya mtihani wa Kidato cha Nne kwa taifa lakini zaidi kwa upande wa Zanzibar. Ni hizo zilitikisa bahari ya Hindi hadi visiwa vikawa vinatetemeka. Ilibidi Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) Joyce Ndalichako afanye ziara ya kuja Zanzibar kuelekezea nini kimejiri mpaka yakatokea yaliotokea ambayo wazee na wanafunzi bado hawajaamini.

Chanzo ni habari za kufutiwa na matokeo na kufungiwa kufanya mitihani kwa wanafunzi zaidi ya 3,000 kote Tanzania kwa sababu ya kile kilichoelezwa kuwa ni udanganyifu unaotokana na mfanano usio wa kawaida.

Lakini pia ikaelezwa kuwa kuna mambo mengine yasio ya kawadia yaliotokea kama vile wanafunzi kuandika matusi, kuchora picha kadhaa lakini pia kuandika nyimbo za Bongo Fleva, si matunda ya kizazi kipya bwana. Basi hiyo ikawa ndio habari.

Ila kwa Zanzibar, kama mshirika kamili katika Muungano, wazee, wanafunzi na wamiliki wa skuli za sekondari wakaona maelezo ya Mama Ndalichako hayakutosha na nafikiri habari hii akaijua na akaamua kuja Unguja, lakini basi hapa akaonana na waandishi wa habari, waalimu na maafisa wa Serikali.

Katika kongomano la siku moja liloitishwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Maendeleo WAHAMAZA wazee, wanafunzi na wamiliki wa skuli walisema wangefurahi wangekutana nae wao Mama Ndalichako na mzee mmoja akasema "angetafuta mahala pa kukimbilia."

Kwa nini akasema hivyo? Amesema hivyo kwa sababu anaamini kuwa Mama Ndalichako hakutoa ushahidi wa kutosha kuonyesha kuwa kumekuwa na udanganyifu na baya kuliko yote ametoa maelezo aliyoyaita kuwa ni ya jumla jumla, mzazi Ahmed Ali alisema.

Mzazi Ahmed kama watu wengi katika kongamano hili alisema Mama Ndalichako ametoa maelezo mengi ya kujilinda na akikwepa kabisa kukubali ukweli kuwa mtihani ulivuja na hicho ndio sababu ya yote yaliotokezea ambayo yeye anadai hajui chanzo chake.

"Nasema mtihani ulivuja kwa hakika. Mimi mwenyewe niliupata nikiwa katika cyber café moja mjini Dar es Salaam. Na nakala ya mtihani huo ambao ulikuwa kwa Kiingereza na uliokuwa ukisambazwa kwa internet ninayo mpaka leo."

Washiriki wengi walisema Mama Ndalichako anapaswa kuwajibika au kuwajibishwa kwa sababu mtihani ulivuja na kadri anavyojitetea na kutoa maelezo ndivyo ambavyo anazidi kujizonga na kujikaanga.

Moja katika maelezo ya Katibu Mtendaji ya kuwepo kwa udanganyifu ni kule kutokea kuwa kumekuwa na karatasi za majibu ya wanafunzi zikiwa zimeandikwa na watu kadhaa na akisema anashindwa kuelewa hilo limetokezeaje wakati wanafunzi wanaodaiwa kuhusika hawakuwa wamekaa jirani kwenye vyumba vya mitihani au chumba cha mithani kwa sababu hakueleza kuwa hilo limetokea shule moja au shule kadhaa.

Kisha akatoa mifano kadhaa iliyoonyesha kuna baadhi ya karatasi za maiibu ambazo wanafunzi waliandika neno kwa neno jambo ambalo halina jawabu nyengine zaidi ya kuwa kulikuwa na udanganyifu tena wa hali ya juu.

Wazee na waalimu walikiri na wala kuwa kulikuwa na udangayifu lakini hoja yao ni kuwa udanganyifu huo ulitokana na kuvuja kwa mitihani ambao sio tu iko chini ya dhamana ya Mama Ndalichako lakini pia inalindwa chembilecho mtu mmoja " kuliko hata ulinzi anaoupata Rais Kikwete au Dk. Shein."

Kwa hivyo hoja ya wazee ni kuwa mitihani ilipatikana mitaani. Wanafunzi wakaifanyia kazi. Vitabu vya majawabu vilipatikana mitaani. Wanafunzi wakavitumia kuandika jawabu zao. Na kwa bahati mbaya kila eneo la jawabu akapewa mtu mmoja na ndio maana kitabu kimoja kikaonekana na hata za watu tofuati lakini hati hizo hizo zikaonekana kwenye vitabu vyengine.

Inawezekana kabisa kuwa baadhi ya waalimu na shule zilishiriki katika mchezo huo, walisema washiriki na kwa hivyo ni muhimu kutoa maelezo ya shule kwa shule na mwanafunzi kwa mwanafunzi ili kila mtu ajiridhishe na sio maelezo ya jumla kama aloyatoa, walisema washiriki. " Kila mzazi anataka kuona mwanawe alishiriki katika visa hivyo au la. Na kila shule inataka kujua shutuma dhidi yake," alisema Mzee Ali Hassan, Mlezi wa Laurette International.

Walimu na wamiliki wanasema wanajua mitihani ilivuja kwa sababu waliona jinsi ambavyo maafisa wa usalama walivyopekua wanafunzi wao na Mama Ndalichako akikataa hilo ni "kwa sababu ya kulinda kitumbua chake. Lakini kwa hili kitumbua hicho kimeshaingia mchanga na hakiliki" alisema Mwalimu Ameir Hassan.

Wazee na waalimu walishangaa kwa nini Mama Ndalichako alikuja Unguja bila kujitayarisha kujua idadi kamili kuhusu wanafunzi waliohusika kwa upande wa Zanzibar na walikasirishwa na jawabu yake nyepesi tu, " Sijafanya hesabu ya mkoa kwa koa," na washiriki wakasema yale yale ya kuona Zanzibar kama mkoa au mikoa mengine tu.

Na ndipo hapo hisia za Muungano zilipokuja na watu wakajaribu kunasibisha tukio hilo na matatizo na kero za Muungano. Walifika hata kuhoji idadi ya Wazanzibari katika Bodi ya Baraza la Mtihani na wakaenda mbali zaidi kuhoji iwapo chombo hicho kikiwa ni cha Muungano kimetoa ajira ngapi kwa Wazanzibari leo au hata jana na juzi kwa sababu kimeundwa tokea 1973 pale jambo hilo lilipofanywa kuwa la Muungano.

Litolewe katika Muungano watu walisema, Tuwe na Baraza la Mitihani letu watu wakapiga kelele suala hili lazima liwe katika ajenda wakati wa Mjadala wa Taifa wa Mabadiliko ya Katiba ambao uko njiani unakuja.

Wengine wakasema tukio hilo lina udini. Matokeo mengi yaliofutwa hapa Zanzibar yanahusu vyuo vya Kiislamu na kudai shule kadhaa za Kikristo huko Bara zinapasisha hadi mwanafunzi mmoja kuwa na kikapu cha alama za "A" lakini hapatiwi shaka au baadhi ya shule kupasisha darasa zima lakini hapatiwi ila katika matokeo kama hayo.

Halili kadhalika walizungumzia juu ya kutokuwepo hatua zinazofanana kwa kesi za aina moja ambapo mwaka jana baada ya kufutwa matokeo ya Darasa la Saba wanafunzi iliamriwa warudie mitihani, lakini pia kuukubwa wa adhabu ya wanafunzi na Professa Abdul Sheriff akiandika katika mtandao alisema, " Haiingii akili utoe adhabu sawa kwa aliyeandika matusi, aliyechora picha na aliyedaiwa kudanganya katika mtihani."

Pia yalikuwa ni maoni ya wadau kuwa kufungia wanafunzi kufanya mithani kwa miaka mitatu ni kuwahujumu kisaikolojia lakini pia wakasema ni mbinu za makusudi kuwakosesha Wazanzibari fursa ya kukuza wataalamu wake, maana kitachotokezea athari ya muda mrefu kwa Zanzibar kielimu lakini pia kijamii.

Hivyo wito ukawa kwamba hilo ni janga la taifa. Kama si kwa Tanzania basi kwa hakika ni kwa Zanzibar na kwa hivyo washiriki wakataka hatua za haraka zichukuliwe ikiwa ni pamoja na Rais Kikwete kumuwajibisha Mama Ndalichako, kuunda tume kuchunguza tukio hilo na kutafuta suluhu ya kudumu ya kuvuja mitihani.

Lakini pia waliitaka Serikali ya Zanzibar kuchukua hatua kwa upande wake na sio kulaza shingo kwa maamuzi ambayo yanaathari kubwa kwa Zanzibar kama nchi. Lakini kubwa zaidi waalimu na wazee hao wamemtaka Mama Ndalichako aje Zanzibar kukutana nao uso kwa uso wakisema hawakutendewa haki kwa yeye kupita katika vyombo vya habari. " Yeye ni mzazi na aje kwa wazazi wenziwe."
 
Jamani hii ni kweli kabisa baada ya kuwepo kwa failure wengi waliomaliza form IV na Form VI Mwaka jana,
Kwa Zanzibar imekuwa ni janga mara mbili kwani wengi wamefutiwa mitihani kwa sababu za wazi kabisa ukizingatia wasimamizi walikuwa ni wazanzibar wenyewe, Sasa wanalalamilka sana wanataka Wizara ya Elimu ijitoe kwenye Muungano.
Hapa mimi kama Mzanzibara, Sina shaka na kujitenga, ila ndugu zangu elimu ya Huku itachakachuliwa kumlazimisha mtoto awe na Elimu ya Sayansi kumbe bongo lala kebebwa tuu na baba mkubwa Waziri, shemeji afisa elimu, Kaka Anafanya Ikulu au anajuana na Rais, Ili mradi Mtu asome bila kuwa na upana wa fikra kwa lile alilolisomea.
Sasa nimeweka Radio Clip nimeisikia kidogo asubuhi kabla ya simu yangu kuisha charge msikie Radio imani na jjinsi watu walivyokuwa wakitoa maoni yao kuhusu failure za mwaka huu.
Aibu kutaka kujitenga ili kuhalalisha madhambi.

Kama haiwahusu sana Msi comment
 

Attachments

  • Radio001.mp3
    1.9 MB · Views: 50
  • Radio002.mp3
    3.2 MB · Views: 40
Hivi hili suala la Elimu katika Muungano likoje? Mimi nadhani elimu ya juu ndio suala la muungano kumbe hata elimu ya msingi na sekondari. Ile Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali huko ZNZ ni ya kazi gani?
 
Kwa hiyo wakijitenga ndiyo watoto wao watafaulu? Kwamba wanasahihishiwa vibaya au? Kwamba madesa ya Muungano ni magumu kwa wazenji au? Kweli akili ya mjinga ni Zero!
 
Simply-kama huna akili lazima ufeli mtihani,
kama husomi unachofundishwa lazima ufeli mtihani
HIKI NDIO KILICHOWATOKEA WALIOFELI WOTE
 
Jamani hii ni kweli kabisa baada ya kuwepo kwa failure wengi waliomaliza form IV na Form VI Mwaka jana,
Kwa Zanzibar imekuwa ni janga mara mbili kwani wengi wamefutiwa mitihani kwa sababu za wazi kabisa ukizingatia wasimamizi walikuwa ni wazanzibar wenyewe, Sasa wanalalamilka sana wanataka Wizara ya Elimu ijitoe kwenye Muungano.
Hapa mimi kama Mzanzibara, Sina shaka na kujitenga, ila ndugu zangu elimu ya Huku itachakachuliwa kumlazimisha mtoto awe na Elimu ya Sayansi kumbe bongo lala kebebwa tuu na baba mkubwa Waziri, shemeji afisa elimu, Kaka Anafanya Ikulu au anajuana na Rais, Ili mradi Mtu asome bila kuwa na upana wa fikra kwa lile alilolisomea.
Sasa nimeweka Radio Clip nimeisikia kidogo asubuhi kabla ya simu yangu kuisha charge msikie Radio imani na jjinsi watu walivyokuwa wakitoa maoni yao kuhusu failure za mwaka huu.
Aibu kutaka kujitenga ili kuhalalisha madhambi.

Kama haiwahusu sana Msi comment
Bora wapate baraza lao la mitihani coz wanawaonea sana!


...
 
waruhusiwe kuwa na baraza lao bwana, zanzibar ni nchi bwana.
hizi hata wizara ya elimu si wanayo?
 
Tumewazoea wapiga kelele tu hao na mwakani wote watapewa zero. Kama wao wajanja wavunje muungano
 
hawa piga wote iv ya 26 kama ya mwanaasha jk.wakafie mbele mijitu haisomi ikifika saa 7 hamna mtu wote madrasa sa watafaulu wap.km vp nenden na znz yenu mtuache tngka yetu.
 
hawa piga wote iv ya 26 kama ya mwanaasha jk.wakafie mbele mijitu haisomi ikifika saa 7 hamna mtu wote madrasa sa watafaulu wap.km vp nenden na znz yenu mtuache tngka yetu.
 
Wakuu?
Nilidhani kama mtu asiporidhika na adhabu ya Baraza la Mitihani anatakiwa akate rufaa (sina uhakika ni wapi) ndani ya muda fulani! Hapa naona suala hili linakuwa treated kijumlajumla!
 
Wakuu,
Nilidhani kama mtu asiporidhika na adhabu ya Baraza la Mitihani anatakiwa akate rufaa (sina uhakika ni wapi) ndani ya muda fulani! Hapa naona suala hili linakuwa treated kijumlajumla!
 
Tumewazoea wapiga kelele tu hao na mwakani wote watapewa zero. Kama wao wajanja wavunje muungano[/QUOTE
'Watapewa zero!!!?' kwa maana hio kumbe ni kweli kuna hujma za waziwazi?
Lisilokufika na ukawa hujaijua athari yake, bora uombe nusra kwa Mungu mana bado unaishi na anything can happen to u
 
Back
Top Bottom