Wazee wa Kigoma waliolipwa pesa kuchafua CHADEMA wachelewa kufika Dar

why

JF-Expert Member
Jun 23, 2012
203
82
Wazee wa Kigoma waliopangwa kuchafua uchaguzi wa CHADEMA kwa bahati mbaya wameshindwa kufika ndani ya muda wa kurudisha fomu kutokana na umbali wa safari ya kutoka Kigoma.

Wazee hao ambao waliandaliwa kutoa tamko la kupinga wazee waliotoka Kigoma na kumchulkulia fomu mheshimiwa Mbowe imefahamika kuwa wameshindwa kufika ndani ya muda na kurejesha fomu ya kugombea uenyekiti na hivyo mkakati wao hadi sasa ni kutafuta mgombea nje na Mbowe ili waweze kumuunga mkono na kumpinga Mbowe kwa maslahi ya chama fulani.

Mbowe ambae anatetea nafasi yake ya uenyekiti alichuliwa fomu na wazee wa Kigoma na kuungwa mkono na makundi mbalimbali ndani ya chama, hadi kufikia saa kumi muda wa mwisho wa kurudisha fomu wanachama maarufu walionekana makao makuu ya CHADEMA wakirejesha fomu mbalimbali na kuomba nafasi tofauti.

Prof. Safari alikuwa amejaza fomu ya kuomba nafasi ya makamu mwenyekiti, prof. Baregu ameomba ujumbe wa kamati kuu lakini pia Mabere Marando ameomba ujumbe wa kamati kuu.

CHADEMA ni mti wenye matunda Mbowe ni mti wa kupigwa mawe daima kwani una mereremeta marunda.
 
Treni lilikwama nini? maana wabongo hatuchelewi kung'oa mataruma.
 
Hawa wazee ndo waliandikwa kwenye gazeti la uhuru la leo, wameula wa chuya. Binadamu anapanga na Mungu anapanga. Jitihada haiondoi kudura.
 
Pumbavu zako hawo cdm mafisadi au mungu anapenda wizi tena kama huu wa cdm

Pumbavu ni wewe unayeshabikia wanyonyaji wa nchi hii ccm,ccm si wazalendo hata kidogo,ni wabinafsi wasiojali wananchi,yaani hawana kabisa habari na mwananchi,ndiyo maana hujiongezea posho na mishahara kila mwaka bila kujali mwananchi anakulaje,analala wapi,anatibiwa wapi akiugua,wao hutibiwa ulaya,kwahiyo hawana habari kabisa kuboresha huduma za hapa nikujilimbikizia mali kwenda mbele,sasa nyinyi misukule mnashabikishabikia utadhani ni vipofu na viziwi.nyambafu.
 
Hawa wazee ndo waliandikwa kwenye gazeti la uhuru la leo, wameula wa chuya. Binadamu anapanga na Mungu anapanga. Jitihada haiondoi kudura.
star TV na radio yao asubuhi tu cha kwanza wamesoma Uhuru... unajua imekuww tawi la ccm....

nkajua tu hii chenga Tupu
 
zitto alitaka uongozi iweje ashindwe kujitokeza kuchukua fomu? huyu kijana mpuuzi sana
 
ZZK apange mipango mingine. Ya leo imeingia mdudu luba. Punga halivuniki hilooo. Mungu bwana angekuwa Asumani, wengi tungesha pelekwa ahera. Mungu wa CDM si mchezo. Kila mnapo iombea CDM dua mbaya ndivyo wao wanashamiri atiiii.
Wazee mlonunuliwa, rudini kundini, Kigoma yetu hiyoooo msiwape hao ACT, hao ni mafisadi yale yale, wamekuja kwa mlango mwingine tu.
Bado CDM tunawapenda na tutamchagua mwingine kuziba pengo la huyo wa mahakama.
 
Hao ndio wazee Orijino kutoka kigoma na sio wale wachumia tumbo waliopewa vijipesa na Mbowe ili waigize kumuunga mkono ili agombee.
Wazee wa Kigoma waliopangwa kuchafua uchaguzi wa CHADEMA kwa bahati mbaya wameshindwa kufika ndani ya muda wa kurudisha fomu kutokana na umbali wa safari ya kutoka Kigoma.

Wazee hao ambao waliandaliwa kutoa tamko la kupinga wazee waliotoka Kigoma na kumchulkulia fomu mheshimiwa Mbowe imefahamika kuwa wameshindwa kufika ndani ya muda na kurejesha fomu ya kugombea uenyekiti na hivyo mkakati wao hadi sasa ni kutafuta mgombea nje na Mbowe ili waweze kumuunga mkono na kumpinga Mbowe kwa maslahi ya chama fulani.

Mbowe ambae anatetea nafasi yake ya uenyekiti alichuliwa fomu na wazee wa Kigoma na kuungwa mkono na makundi mbalimbali ndani ya chama, hadi kufikia saa kumi muda wa mwisho wa kurudisha fomu wanachama maarufu walionekana makao makuu ya CHADEMA wakirejesha fomu mbalimbali na kuomba nafasi tofauti.

Prof. Safari alikuwa amejaza fomu ya kuomba nafasi ya makamu mwenyekiti, prof. Baregu ameomba ujumbe wa kamati kuu lakini pia Mabere Marando ameomba ujumbe wa kamati kuu.

CHADEMA ni mti wenye matunda Mbowe ni mti wa kupigwa mawe daima kwani una mereremeta marunda.
 
Hawa ni wazee wachumia tumbo waliotumwa na CCM kwenda kuharibu mchakato. Hawa wazee wana laana na pia hawajielewi. Ni wazee wa kupuuzwa mbali, Akili zao zina Kwashakoor.
 
Back
Top Bottom