Wazee wa Dar: Tulitaka kumuuliza Rais

Wazee wa Dar: Tulitaka kumuuliza Rais

Afadhali hawakupewa nafasi ya kuuliza manake wangepewa hiyo nafasi wangeuliza hata suala la nauli ya kurudia nyumbani...
 
Wazee wa Dar watu wa ajabu, wanatumiwa vibaya na watawala.
 
when you go deep JK amepotosha na still ameibua maswali mengi sana badala ya majibu
Mbona hakuzungumza hela yetu tutaipataje tena???TZ siku hizi watu wana akili zao mjipange tena
 
Hakuna kitu kibaya katika nchi yeyote Rais au mkuu wa nchi aliyewekwa kulinda rasilimali za nchi akaanza kuhisiwahisiwa kuwa anahusika na dili za kuhujumu nchi anayoiongoza. Jee wa kwetu ameanza kuhisiwa hivyo kutokana na utetezi wake katika pigi hili?
 
kivip wawe nuksi mkuu?





hao walifunga barabara ya sokoine kwa masaa sita. bibi titi wakaifunga masaa matano wakidai hela zao hao huwezi kuwaita kwenye mambo hayo wengi walikuwa matarishi na makuli wakikutukana unalia .wanavua nguo polisi ikiwafuata acha kabisa
 
Ngoja niende zangu kule MMU cause kuendelea kumjadiri huyu dhaifu nikujitafutie ugonjwa wa moyo, huyu ni kichwa maji, hajui hata anafanya nini ikulu haki ya nani!
 
Huyu Zombie nilijua leo ana conclude hii saga yeye kaianzisha upya sasa mfikishieni ujumbe tunataka majibu ya haya maswali. Alibembeleza wezi wa EPA sasa hawa wa ESCROW pia anataka kuwabeba safari hawa lazima adondoke nao.

Jamani yeye ndo mhusika mkuu wa hizi pesa kutoka. Gavana wa BoT aligoma kutoa pesa mpaka idhini ya rais itoke na ikatoka ikiwa imesainiwa na katibu binafsi wa rais na si katibu mkuu kiongozi. Na katika orodha ya waliochukua pesa yumo msaidizi wa rais aliyelamba milioni 800 plus sasa unafikiri hapo baba Ridhiwani si mhusika mkuu? Hatuna rais nchi hii ni mwizi fulani tu kajikalia pale Magogoni, mbaya sana.
 
Wamelalamika kuwa wao hawakuuliza. Wanasema kama kuzungumza nao,kama inavyokuwa kwa Waandishi wa Habari,walikuwa na shauku ya kurusha maswali yao kwa Rais baada ya hotuba yake.

Wanalalamika kunyimwa nafasi. Wengine wameapa kutokwenda tena watakapoitwa. Nimejaribu kuwaelewesha bila ya kueleweka na wao kuelewa. Wakatest kuniuliza maswali mawili-matatu.

La kwanza,kwanini TANESCO hawakurudi ICSID kwa miaka saba na wakuu wao,yaani Wizara ya Nishati na Madini, kutowahoji kwa kutokwenda kwao huko? La pili,mgogoro kati ya TANESCO na IPTL ulikuwa ukijulikana Serikalini?

La tatu,ni kweli kulikuwa na hukumu iliyoamuru fedha zilipwe kwa IPTL? CAG alikagua vipi fedha isiyo ya umma? La tano,kukiuka kulipa kodi kunasameheka na si jinai tena?

Kutokana na uzito wa maswali hayo,kulingana na umri na uwezo wangu,nimewaomba niwajibu kwa barua au simu baada ya utafiti ulio fiti.

Rais anaweza kufikishiwa maswali haya. Ni ya msingi!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

Ccm na viongozi wenu hamna jipya. Yaani hata rais wa nchi anatetea wizi! Inasikitisha kwa rais alie apa kuilinda na kuitetea katiba anakuwa wa kwanza kuivunja. Hivi ni kweli Kikwete hajui kama katiba inampa mamlaka ya kuwawajibisha qateulè wake? Ati anachunguza kwa muda gani??? Anaechunguzwa bado yuko ofisini!!! Hahahaaaa mambo kianunuasi haya. Ccm mmezeeka, na mawazo yenu yamekuwa na saratani.
 
hao walifunga barabara ya sokoine kwa masaa sita. bibi titi wakaifunga masaa matano wakidai hela zao hao huwezi kuwaita kwenye mambo hayo wengi walikuwa matarishi na makuli wakikutukana unalia .wanavua nguo polisi ikiwafuata acha kabisa

aisee basi hawa kweli walikuwa wanadai haki zao, kama waliweza kufanya hayo uzeeni sipat picha enzi za ujana wao!
 
aisee basi hawa kweli walikuwa wanadai haki zao, kama waliweza kufanya hayo uzeeni sipat picha enzi za ujana wao!

mapambano ya uhuru wa tanganyika yalianzia bandarini huko kama mapambano ya wafanyakazi. baada ya uhuru hawa jamaa wa bandari walindelea kumpa jambajammba mwalim nyerere na aliwaweka viongozi wao vizuizini sana tu.Kitabu cha kuli kina ujumbe wa mapambano haaya japo upande wa zanzibar kimeandikwa na shafi adam. hao wazee walisema kama hawatalipwa wengelifanya kitu kingine cha ajabu zaidi hatimaye wakalipwa. walikuwa wakifika mahakama kuu wanasali kwenye lami pale na shehe wao ni balaa si unajua inavokuwa.wanaenda mahakamani mchana sa saba wanaingia kwenye lami wanapiga sala ffu wanabaki kuduwaa
 
Back
Top Bottom