Wazee wa Dar es salaam

mpigilie

JF-Expert Member
Sep 14, 2011
310
136
Wamejaa hekima kuliko wazee wote wa Tanzania
Ni wasikivu hata raisi wetu anajivunia
Sio wabishi kila wanachoambia wanasikia
Ni wataratibu hata ukiwatukana watakushangilia
Watakupigia makofi bila kujali unachoongea
Hata kama unataka kuua baraka watakupatia
Wana uelewa mkubwa wa kila jambo linalotokea
Wanatumika kama chombo matamko kuyatolea
Busara na hekima zao hakuna mfano wa kupigia
Akili za kuambiwa pia zao wamechanganyia

Wazee wa mikoani usia nawapatia
Msiwe wabishi mtazidi kujiaribia
Hasa nyinyi wa kaskazini na wenzenu wa mbeya
Hizo people people wakuu hawataki kuzisikia
Mmevuka mipaka mmewaambukiza na wa kanda ya ziwa
Mnatuharibia vijana rangi zetu wanazichukia
naomba niishie hapa tamati nimefikia
Mwenye akili timamu ashaelewa nnachoongea
 
Hivi hawa wanaoitwa wazee wa Dar ni akina nani? Nafikiri sasa tuanze kutumia wazee wa East African Community kunapotokea majanga ya kitaifa.
 
Hivi hawa wanaoitwa wazee wa Dar ni akina nani? Nafikiri sasa tuanze kutumia wazee wa East African Community kunapotokea majanga ya kitaifa.

Hawa wazee kwa jinsi walivyopinda si wanaweza mzuia mkulu kuingia ukumbini na mambo ya hotuba yakaishia hapo, manake akikosea kuingilia mlango tofauti kinachofuata wanavua nguo woote ukumbini!!!! aaalah! mtashauriana wenyewe muwapige mabomu ya kuwavalisha nguo au mabomu ya kuwatawanya bila nguo. sasa unacheka nini!!!!! ni pm nini kinakuchekesha.
 
inabidi tujue sifa stahiki za kua mzee wa dar es salaam.
inawezekana ukawa unaishi mkoa mwingine lakini ukawa mzee wa dar es salaam.
 
Kwan ili kufika mkutanoni nauli nan anawapa ndo ujue kama wanalipiwa nauli kupga makof haki yao
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom