Wazee wa Dar es Salaam wawataka ukawa kurudi bungeni

Wazee wa Dar es Salaam wawataka ukawa kurudi bungeni

Wazee wa CCM,maskini hawaelewi chochote!Warudi tu vijijini maana jaza jiji tu bila manufaa.Huwa wanalipwa?

Ukisema wazee warudi kijiji unajumlisha na katibu mkuu, ni mmoja wapo kati ya wazee ukizingatia sasa ana kilema cha maisha inambidi akapumzike.
 
Mbona ni Ma-Alhaji watupu...au ni ma-alhaji wa mkoa wa Dar.
 
Mbona mzee wangu (baba) sijawahi sikia anaongerea umoja wao wa dar es salaam!huwa wanavikaovyao na wanakutana baada ya muda gani???wanakutana wapi?nani mwenyekiti wao?je wanakatiba yao???naomba kujuzwa ili niweze mshawishi mzee wangu akajiunge.
 
Ukisema wazee warudi kijiji unajumlisha na katibu mkuu, ni mmoja wapo kati ya wazee ukizingatia sasa ana kilema cha maisha inambidi akapumzike.

Waambie hao wazee wako wa Dar kwamba wazee wa Arusha hawataki kusikia hilo la ukawa kurudi Bungeni!!!!
 
Hivi siku chache hizi tumeshasahau mikutano ya nape na kinana? Walipita huku na kule wakieleza msimamo wa chama na flana za mbili zatosha tatu za nini. Jibu liko wazi hapa acheni kuchezea kodi zetu bana.
 
WAZEE wa Mkoa wa Dar es salaam wamewaomba Umoja wa Katiba wa Wananchi (UKAWA) kurudi Bungeni ili kuendelea na mchakato wa majadiliano ya Rasimu ya Katiba Mpya yanayoendelea.-

-Wazee hao wamesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wakizungumza na waandishi wa habari kuhusu hali ya siasa nchini pamoja na Bunge la Katiba Mpya linaloendelea mjini Dodoma. Akizungumza kwa niaba ya Wazee wenzake Kepteni Mstaafu Alhaji Mohamedi Ligora , amesema kuwa Tanzania ni nchi nzuri na watu wake ni wazuri ni vema UKAWA na wenzao wakarudi Bungeni kujadiliana ili watimize matakwa ya kidemokrasia.-

-Amesema kuwa wananchi wa Tanzania hawataki kufananishwa na nchi zingine zilizofanya makosa na kupata matatizo kutokana na mambo kama haya ambayo yalisababisha wananchi wao kuzikimbia nchi zao kwa mambo ambayo wangeweza kukaa chini na kumaliza wenyewe kwa ajili ya maslahi ya umma. Kapteni Mstaafu Alhaji Ligora amesema kuwa suala la mchakato ni suala la kidemokrasia, hivyo ni vyema UKAWA wakatumia fursa hiyo waliyonayo kwa kurudi Bungeni na kuendelea na majadiliano kuhusu Rasimu ya Katiba hali itakayosaidia kupatikana kwa Katiba Mpya ambayo itakuwa na manufaa kwa wananchi wa Tanzania.

-Aidha, amewaomba wajumbe walio Bungeni na wale walio nje ya Bunge kuacha kuwazomea UKAWA badala yake wawasihi warudi katika chombo rasmi cha kuboresha Rasimu ya Katiba Mpya.

-Naye Mzee Ali Bakari Muki, amewataka UKAWA kuheshimu misingi ya demokrasia lakini pia amewapongeza wabunge walioitikia wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kurudi Bungeni na kuendelea na majadiliano kuhusu Katiba kwani ndio Jukwaa pekee la kuwapatia wananchi Katiba bora.

-Kwa upande wake Mzee Yahaya Ngoma amewataka viongozi wote hasa UKAWA kuheshimu na kudumisha jitihada zilizofanywa na waasisi wa Taifa hili akiwemo Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere pamoja na Sheikh Abeid Amani Karume kwa kuzingatia misingi na kanuni za uongozi bora kwa kutumia njia ya majadiliano pale panapokuwa na mawazo tofauti baina yao. Halikadhalika, Alhaji Sheikh Bakari Chikawa amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuridhia kuanza kwa mchakato wa Katiba Mpya na kusisitiza ni moja ya tunda la uongozi bora na demokrasia nchini.

-Aidha, ameongeza kuwa UKAWA ni vema wakatumia fursa hiyo ya demokrasia kwa kuwawakilisha vema wananchi wa Tanzania ili kuhakikisha wanapata Katiba Bora. Alhaji Chikawa amewaomba UKAWA kurudi Bungeni kwani kunyume na hivyo ni watakua wametenda dhambi na madhara yake ni makubwa sana, na kusisitiza kuwa mazungumzo ni muhimu na yakipuuzwa basi kuna madhara.



Wazee Dar wailipua UKAWA


​


CHANZO: Majira

Wao ni nani? Na kwanini hawa waombi CCM kuachana na msimamo wao wa serikali mbili?
 
mfano wazee wa mahakama huwa ni wazee wa nani?

Wazee wa mahakama hua ni wazee walioteuliwa na ambao hufanya kazi kwa mkataba na kulipwa kutokana na kesi zilizosikilizwa mbele yao.
 
wazee njaaa hao,kwanza wapumbavu sana,mzee ataniambia nini mimi kijana,wale akili zimelala tayari wakae tu home wanywe chai na kahawa,pumbavu kabisa,tena shenzi vizee vyote vya ccm
 
Wametumwa hao, wanaudhalilisha umri wao. Kesho tutasikia wabibi wa Dar nao wametoa tamko, maana nchi hii ni full matamko
 
Wazee wa Dar es salaam = Wazee wa CCM

Kama unabisha tafuta Mwenyekiti na Katibu wao ujiridhishe!!
Hawa ni wazee wa ccm wa dar es salaam wanaorubuniwa na vikombe vya kahawa....
 
mfano wazee wa mahakama huwa ni wazee wa nani?
Jibu swali kwanza.....acha kuzunguka mbuyu!
Hata hivyo kwa kukujibu swali lako, wazee wa mahakama ni wazee wa wahalifu na wanaopindisha sheria kuwaongezea wanyonge maumivu!
 
kwann ni wazee wa dar tu? kwann wasiwashauri ccm wakubali serikali tatu? au wametumwa?
 
Kwani Dar kuna wazeee, mbona wanasema uzee mwisho mkata?, au ni wa zee wa mkata
 
Kwanini wasiwaambie ccm wakubali kujadili rasimu halali. Uzee wao hauna kama wanaegemea upande mmoja.
 
Back
Top Bottom