Rich Pol
JF-Expert Member
- Oct 11, 2013
- 7,880
- 5,725
WAZEE wa Mkoa wa Dar es salaam wamewaomba Umoja wa Katiba wa Wananchi (UKAWA) kurudi Bungeni ili kuendelea na mchakato wa majadiliano ya Rasimu ya Katiba Mpya yanayoendelea.-
-Wazee hao wamesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wakizungumza na waandishi wa habari kuhusu hali ya siasa nchini pamoja na Bunge la Katiba Mpya linaloendelea mjini Dodoma. Akizungumza kwa niaba ya Wazee wenzake Kepteni Mstaafu Alhaji Mohamedi Ligora , amesema kuwa Tanzania ni nchi nzuri na watu wake ni wazuri ni vema UKAWA na wenzao wakarudi Bungeni kujadiliana ili watimize matakwa ya kidemokrasia.-
-Amesema kuwa wananchi wa Tanzania hawataki kufananishwa na nchi zingine zilizofanya makosa na kupata matatizo kutokana na mambo kama haya ambayo yalisababisha wananchi wao kuzikimbia nchi zao kwa mambo ambayo wangeweza kukaa chini na kumaliza wenyewe kwa ajili ya maslahi ya umma. Kapteni Mstaafu Alhaji Ligora amesema kuwa suala la mchakato ni suala la kidemokrasia, hivyo ni vyema UKAWA wakatumia fursa hiyo waliyonayo kwa kurudi Bungeni na kuendelea na majadiliano kuhusu Rasimu ya Katiba hali itakayosaidia kupatikana kwa Katiba Mpya ambayo itakuwa na manufaa kwa wananchi wa Tanzania.
-Aidha, amewaomba wajumbe walio Bungeni na wale walio nje ya Bunge kuacha kuwazomea UKAWA badala yake wawasihi warudi katika chombo rasmi cha kuboresha Rasimu ya Katiba Mpya.
-Naye Mzee Ali Bakari Muki, amewataka UKAWA kuheshimu misingi ya demokrasia lakini pia amewapongeza wabunge walioitikia wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kurudi Bungeni na kuendelea na majadiliano kuhusu Katiba kwani ndio Jukwaa pekee la kuwapatia wananchi Katiba bora.
-Kwa upande wake Mzee Yahaya Ngoma amewataka viongozi wote hasa UKAWA kuheshimu na kudumisha jitihada zilizofanywa na waasisi wa Taifa hili akiwemo Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere pamoja na Sheikh Abeid Amani Karume kwa kuzingatia misingi na kanuni za uongozi bora kwa kutumia njia ya majadiliano pale panapokuwa na mawazo tofauti baina yao. Halikadhalika, Alhaji Sheikh Bakari Chikawa amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuridhia kuanza kwa mchakato wa Katiba Mpya na kusisitiza ni moja ya tunda la uongozi bora na demokrasia nchini.
-Aidha, ameongeza kuwa UKAWA ni vema wakatumia fursa hiyo ya demokrasia kwa kuwawakilisha vema wananchi wa Tanzania ili kuhakikisha wanapata Katiba Bora. Alhaji Chikawa amewaomba UKAWA kurudi Bungeni kwani kunyume na hivyo ni watakua wametenda dhambi na madhara yake ni makubwa sana, na kusisitiza kuwa mazungumzo ni muhimu na yakipuuzwa basi kuna madhara.
Wazee Dar wailipua UKAWA
CHANZO: Majira

Jumatatu, August 18 2014
WAZEE wa Mkoa wa Dar es Salaam, wamesema sababu zilizotolewa na wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kutoka kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) na kuwafanya watoke nje ya vikao vya Bunge hilo ni za uongo bali wanataka kuvuruga amani iliyopo.
Walisema hoja ya UKAWA kuwa wanachokifanya ni kutetea maslahi ya Watanzania haina mashiko bali dhamira yao ni kuvuruga amani iliyoachwa na Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere.
Kapteni mstaafu Alhaji Mohamed Ligora, aliyasema hayo Dar es Salaam jana kwa niaba ya wazee hao wakati akitoa msimamo wao kuhusu mchakato wa kutengeneza Katiba Mpya nchini.
"Amani tuliyoachiwa na Mwalimu Nyerere, imeendelezwa na marais wengine akiwemo Rais Jakaya Kikwete ambaye ndiye yupo madarakani kwa sasa...UKAWA si kwamba hawana uzalendo ila kuna shetani anaingilia kati," alisema.
Alhaji Ligora alisema, vyama vya upinzani ndivyo vilivyokuwa vikililia Katiba Mpya hivyo havipaswi kuukimbia mchakato huo bali vinapaswa kushiriki vikao vya Bunge la Katiba ili kuleta maridhiano ambayo yatasaidia kuwapatia wananchi Katiba bora inayoweza kuwaletea maendeleo.
"Hatutaki waje mitaani kutudanganya kwani Katiba haipatikani nje ya Bunge, sisi hatudanganyiki na shetani anayetaka kutuvuruga Watanzania bali tunataka Katiba bora yenye kuleta maendeleo kwa wananchi na Taifa kwa ujumla," alisema Alhaji Ligora.
Aliongeza kuwa, mtu anapopewa fursa ya kutengeneza jambo ulilokuwa unalilia muda mrefu, ndio muda anaopaswa kuonesha uwezo wake juu ya jambo hilo badala ya kulikimbia kwani hiyo ni dalili ya kuonesha uoga wa jambo husika.
Alisema kuendeleza migogoro ndani ya nchi kunaweza kusababisha nchi ikaingia kwenye machafuko kama yaliyozikumba baadhi ya nchi nyingine za Afrika kutokana na kutokuwepo kwa maridhiano.
"Kama Tanzania itaingia katika machafuko kutokana na mchakato huu, watu ambao wataathirika ni wananchi si viongozi...kutofikia maridhiano kumewafanya majirani zetu Kenya, kuingia katika matatizo na sisi hatutaki kufika huko kwani Tanzania ni nchi ya amani, umoja na upendo," alisema.
Naye mmoja wa wazee hao, Omary Chiwaka, alisema kitendo cha UKAWA kutoka nje ya Bunge la Katiba ni kutowatendea haki wananchi waliowapa mamlaka ya kuwawakilisha wao ili ipatikane Katiba bora.
"Maendeleo hayaji kwa malumbano bali yanakuja kwa maridhiano, jambo la msingi ni wajumbe wote wa Bunge hili washirikiane ili tuweze kupata Katiba ambayo itatuletea maendeleo, kundi moja likienda kinyume maendeleo hayawezi kupatikana," alisema.
Alisema UKAWA wanatengeneza dhambi ambayo itakosa mtu wa kuibeba na tamaa haiwezi kumnufaisha mtu bali itamwangamiza mwenyewe.
CHANZO: Majira