Wazee sasa waingilie kati suala la Katiba Mpya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wazee sasa waingilie kati suala la Katiba Mpya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kisendi, Nov 18, 2011.

 1. K

  Kisendi JF-Expert Member

  #1
  Nov 18, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 700
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  NDOTO za Watanzania kupata Katiba Mpya kwa njia ya mwafaka na maridhiano ya kitaifa sasa zinaonekana kuota mbawa kwa sababu mbili kubwa. Kwanza, mwenendo wa wabunge wengi, hasa wa chama tawala wakati wa kujadili Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011 umeonyesha pasipo shaka kwamba hawana utashi wa kisiasa kwa hofu kwamba mchakato wa kupata Katiba Mpya unaweza ukawa mwanzo wa chama chao kutoka madarakani.

  Pili, ni dhana ya wabunge hao kwamba ajenda ya kupata Katiba Mpya haikuwa ya chama chao, bali ilikuwa ya Chadema ambacho kiliifanya kama moja ya mambo muhimu katika Ilani yake katika kampeni za kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana. Ajenda hiyo ya Katiba Mpya ilionekana kuwagusa wananchi wengi na ndiyo maana baada ya uchaguzi huo, Serikali ya CCM ilikubali kuitekeleza ingawa baadhi ya watu wanasema ilifanya hivyo kwa shingo upande.

  Hivyo, kitendo cha wabunge wengi wa chama hicho kutumia muda mwingi kukibeza na kukipiga vijembe Chadema na wabunge wake wakati wakichangia muswada huo kwa siku tatu mfululizo kinaweza kutafsiriwa kuwa ni kujaribu kutumia wingi wao bungeni kama turufu ya kukitunishia chama hicho misuri kwa kukataa kila hoja inayoletwa mezani na wabunge hao wakati wa kujadili muswada huo.

  Hata baada ya wabunge hao na baadhi wa NCCR kususia mjadala huo kwa kutoka nje ya Bunge, wabunge wa CCM waliendelea kutumia lugha ya matusi, kejeli na isiyokuwa ya kibunge dhidi ya wabunge wa Chadema, huku wenyeviti wa vikao ambao wote ni wa CCM wakikaa kimya pasipo kuwakemea wala kuwataka wafute kauli zao. Bahati mbaya hakuna mbunge yeyote aliyetumia busara kulikumbusha Bunge kwamba lilikuwa linajadili muswada muhimu katika mustakabali wa taifa na kwamba hapo hapakuwa mahali pa kushindanisha itikadi za vyama au kupigana vijembe.

  Matokeo ni kwamba Bunge lilikosa mwelekeo na kupoteza muda kiasi cha Serikali na uongozi wa Bunge kulazimika kuongeza muda wa majadiliano hadi jana mchana ingawa haikuelezwa kwa nini Spika hakuitisha kura ya kuupitisha muswada huo. Hata hivyo, wananchi wengi wameonyesha wasiwasi kwamba, kura hiyo haitakuwa na maana siyo tu kama haitawahusisha wabunge wa vyama vyote, bali pia kama muswada hautakuwa umepata mwafaka wa kitaifa.

  Kupitia safu hii jana, tulionya dhidi ya hatua zozote katika mchakato huu wa kupata Katiba Mpya ambazo zitachukuliwa bila kupatikana maridhiano wala mwafaka wa kitaifa na kusema kwamba, kufanya hivyo ni kukaribisha machafuko. Tulikumbusha kwamba katika kuandika katiba mpya mahali popote duniani, wanaobeba dhima ya kusimamia mchakato huo hulazimika kuhakikisha kwamba mwafaka wa kitaifa unapatikana katika kila jambo linalojadiliwa kwa kuzingatia dhana kwamba kila wazo au pendekezo linalotolewa ni muhimu mno katika mchakato mzima.

  Kama tulivyosema jana, Bunge lilifanya makosa makubwa kukataa na kubeza maoni yaliyotolewa na wanaharakati na makundi mengine ya kijamii ambayo yalilenga kuboresha muswada huo. Hatudhani kwamba hoja zao zilikuwa nyepesi kiasi cha kubezwa na kupuuzwa. Hivyohivyo, tunakubaliana na hoja zilizotolewa na makundi mbalimbali, yakiwamo majaji wastaafu, kwamba mfumo wa Bunge la Katiba uliowekwa ni mbaya kwa sababu ukipitishwa CCM itakuwa imeteka rasmi mchakato mzima wa Katiba na hakika hakuna kitakachowazuia kuuandika wanavyotaka wao.

  Ndiyo maana tulipendekeza jana kwamba, ili kuepusha machafuko Bunge liachane na dhana ya wengi wape, kwani katika kutafuta mwafaka wa kitaifa katika mambo muhimu kama kuandika katiba ya nchi, dhana hiyo huwekwa pembeni. Tunadhani wakati sasa umefika kwa wazee wenye busara nchini kuingilia kati suala hili kwa manufaa ya wananchi wote. Ndiyo maana tunasema tumetiwa moyo na kauli za baadhi ya wazee wetu waliposema juzi wakati wa kongamano la Taasisi ya Mwalimu Nyerere kwamba, muswada wa katiba lazima upate mwafaka wa wananchi.
   
 2. K

  Kisendi JF-Expert Member

  #2
  Nov 18, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 700
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  Ikishindikana tusubiri CHADEMA wakichukua nchi 2015
   
 3. K

  Kisendi JF-Expert Member

  #3
  Nov 18, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 700
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  Wazanzibar wanahofu nini muungano ukivunjwa. Maana wao wanafaida sana, Urais wanataka huku bara, lakini kwao hawataki mtu wa bara, Bungeni kwetu wapo kwao hawataki, wanabendera, wanawimbo sisi bara/tanganyika hatuna wimbo wetu wa taifa letu la bara, hatuna rais wao wana rais, JK ni rais wa muungano sio wa Watanganyika. Tutafakari kwa hili pia mambo ni mengi sana wazanzibar wananufaika kupitia muungano. Tanganyika tuamke
   
 4. M

  Malova JF-Expert Member

  #4
  Nov 18, 2011
  Joined: Apr 21, 2011
  Messages: 777
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Wazee wengi ni sawa na wabunge wakijani. Mawazo yao yanawezakuwa sawa na mawzo ya wale jamaa wakijani.
   
 5. F

  Fred Otieno Member

  #5
  Nov 18, 2011
  Joined: Apr 8, 2007
  Messages: 17
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 5
  Wazee wengi sasa hivi wana njaa sana wataangalia upepo ili waweze kunusuru matumbo yao kwa muda wao uliabaki kuishi,usitegemee jipya kutoka kwao.
   
 6. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #6
  Nov 18, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Wazee wenyewe ndiyo wale wa type ya Sheikh Yahya?
   
Loading...