Wazee Kirua Vunjo Kusini wakoshwa uchapakazi wa Dkt. Kimei jimboni Vunjo

SautiYaMnyonge

JF-Expert Member
May 13, 2018
439
742
Kirua Vunjo Kusini.
Koresa.
Tarehe 10/12/2021.

Mbunge wa Jimbo la Vunjo Mhe. Dkt. Charles Kimei amekutana na Wazee mashuhuri kutoka Kata ya Kirua Vunjo Kusini waliomualika kuzungumza nao.

Wazee hao wakiongozwa na Mzee Gasper Ngowi walimweleza Mhe. Mbunge dhamira yao ya kuanza kujenga Kituo cha Afya kwa michango yao binafsi ili kuhudumia wananchi. Mzee Ngowi kwa niaba ya wazee wenzake wamemtaka Mhe. Mbunge kuendelea kuchapa kazi ili kumsaidia Mhe. Rais na kumtaka aendelee kutenda zaidi aliyotumwa na wananchi wake.

Wamemhakikishia kumuunga mkono katika dhamira yake ya kuleta Maendeleo Jimbo la Vunjo na wanaridhishwa na kazi kubwa anayoifanya kwa sasa. Wamemueleza asihofu wala kukata tamaa maana wao waliompa dhamana hiyo wanaridhishwa na kazi waliyomtuma.

Mhe. Mbunge, amewashukuru kwa kuendelea kumpa imani, amewaahidi kutowaangusha katika kuleta Maendeleo ya Jimbo la Vunjo. Mhe. Mbunge amewataka kuendelea kumuombea kwa Mungu ili kazi hii ya kuwatumikia wananchi aifanye vizuri zaidi.

Mhe. Mbunge amewachangia Tsh Milioni 2 ili kumalizia Ujenzi wa Ofisi ya Kijiji.


VUNJO KAZI INAENDELEA.
IMG-20211211-WA0019.jpg
IMG-20211211-WA0017.jpg
IMG-20211211-WA0012.jpg
IMG-20211211-WA0012.jpg
IMG-20211211-WA0011.jpg
IMG-20211211-WA0012.jpg
IMG-20211211-WA0016.jpg
IMG-20211211-WA0010.jpg
IMG-20211211-WA0014.jpg
IMG-20211211-WA0013.jpg
 
Kwahiyo kwako kupiga picha na wana kijiji ndiyo uchapaji kazi wa kupongezwa?
 
We si juzi tu hapa walimtaka ajieleze kwa Nini aliwataja wananchi wake hawapendi kulipa Kodi bungeni?
Kwa hiyo Leo Tena wamemuona mpiga kazi! Mmmm maajabu ya Tanzania huwa hayaishi.
 
Back
Top Bottom